Mwanaume mwenye wake 15 asema Wanaume wenye Mke Mmoja wana Akili Ndogo Sana: "Wanaweza Kuongelea jambo moja kwa saa 3”

Hapo ukute zaidi ya watoto 10 kasaidiwa na wana
 
Nikola Teslas na Isaac Newton hawakuwai kuoa na leo wapo kwenye historia ya watu wenye akili zaidi waliowahi kuishi hapa duniani.
Kipimo cha akili hushabihiana na mazingira na utsmaduni,kwa utamaduni wao perherps walikuwa na akili ila wangekiwa huku pengine tungewaona waliochanganyikiwa,huyu mkenya kwa mazimgira yake anajiona anaakili aheshimiwe!!
 
Kama unaamini huu upuuzi inabidi ukapimwe kichwa,
Kwanza tuanzie,hapa hao wake zake Wana ubora Gani?ki elimu,au ndio wale hata darasa la Saba hawana,bado wanaamini uchawi,Wala ugoro,hawajawaji hata kuona jiko la umeme,achilia mbali simu janja,
Kama ana wake kumi wenye elimu ya shahada,graduate,heshima kwake,
Kwa ustawi wa jamii na Dunia,huyu kenge na dangote,Eron musk nani anafaida kwa Dunia?
 
akiweza kusomesha watoto hata watano tu na wakafanikiwa kielimu njoo unichape viboko nimekaa nyuma ya Samsung Tab hapa
yani ukipenda wake wengi na ukiwa na watoto wengi hausomeshi ni kulishia na kutafuta wake wengine (hela inatumika)
WAZAZI SOMESHENI WATOTO WENU
 
Ni kweli kabisa.

Hata migogoro mingi ya ndoa ni kwa wenye mke mmoja.

Hata nje ya ndoa; ukiwa na girlfriend ni rahisi sana kuteswa na mapenzi tofauti na mwenye girlfriends.

Ana hoja, asikilizwe.
Kweli kabisa hili nimeli-experince suala lakua na mke mmoja unakua unazungumzia jambo moja kwa mda mrefu sana nahuenda akakulisha matango pori.kua nawanawake wengi au girlfriends wengi huleta utulivu na kupoza akili pia.
 
Ubora wa binadamu ni "Elimu" tu? Kwamba ukioa wake wenye PhD ndo heshima?
 
Wengi wamesomesha watoto ila bado hao watoto ni tegemezi kwao pamoja na kuwa na hayo makaratasi ya vyeti.
 
Nilijua amefanya uvumbuzi fulani baada ya kua na wake wengi ndio maana anajiita ana akili kumbe ni kuongea mda mchache [emoji1][emoji1][emoji1] mimi sina mke hata mmoja ila sipendi kuongea mda mrefu kabisa kuongea ni haiba ya mtu
 
Nikola Teslas na Isaac Newton hawakuwai kuoa na leo wapo kwenye historia ya watu wenye akili zaidi waliowahi kuishi hapa duniani.
Hiyo boya linajiona linaakili kisa kuwa na wake wengi limerahisha sana maana ya kuwa na akili
 
Aje aekéze na huku Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…