SoC02 Mwanaume rudi kwenye nafasi yako!

SoC02 Mwanaume rudi kwenye nafasi yako!

Stories of Change - 2022 Competition

vholl2000

Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
12
Reaction score
12
Ni ukweli usiopingika kuwa tokea mapinduzi ya kumkomboa mwanamke kiuchumi, kisiasa na kijamii wanawake wengi wamekuwa na nguvu sana katika nyanja zote za siasa, uchumi na jamii na kuwaacha wanaume nyuma.

Tukirudi miaka ya 90 kurudi nyuma kulikuwa na dhana kwa wanawake wengi kuwa wao hawawezi pasipo mwanaume, dhana hii ilibadilika baada ya mkutano mkubwa wa wanawake uliofanyika Beigin ambapo maadhimio mbalimbali ya kumkwamua mwanamke kiuchumi, kisiasa na kijamii yalifanyika. Mashirika na nchi za kimataifa zimewekeza sana kwa mwanamke na sasa tunaona mwanamke ameanza kubeba majukumu sawa na ya mwanaume.

Jambo hili ni jema, lakini pia lina hitaji sana hekima kwani mwanaume toka anaumbwa , aliumbwa na Mungu kufanya kazi na kuiangalia familia yake yaani mke na watoto.Kuanzia miaka ya 2000, vijana wengi hapa nchini, walianza kujiaminisha kuwa wakitaka kuoa waoe wanawake wenye uwezo kiuchumi, wengine 'wanaota' kabisa ndoto za kuoa na kupewa magari, nyumba na wake au wakwe zao nk jambo ambalo limekuja kuathiri ndoa nyingi na talaka nyingi sana zimeongezeka tokea kipindi hiko kutokana na mwanaume kutoijua nafasi yake katika familia na jamii. Wazazi wengi wanalia kwa kuwa wanaume waliowazaa hawaoni kuwa wanaume tena kwani wamechukua tamaduni za magharibi na kugeuka kwa namna ya kike kwa kisingizio cha maisha magumu na kutafuta pesa..

Ni ukweli usiopingika kuwa nguvu ya mwanaume kwenye jamii na familia ni nguvu ya uchumi, hii humpa mwanaume uwezo wa kujiamini na kuyaatumia mamlaka yake ambayo Mungu amempa. Ni wakati sahihi sasa vijana wetu wafundishwe na kina baba wazee majukumu yao, mamlaka walizonazo katika familia na jamii.


Elimu ya Uchumi na Ndoa kwa wanaume na vijana wa kiume.

Wanaume wapate mafunzo kutoka kwa wanaume ambao wameinuka kiuchumi, wanaume ambao wapo vizuri katika ndoa. Tumezoe kuona semina za wanawake au makusanyiko ya wanawake wakifundwa namna ya kukaa katika ndoa zao namna ya kujikwamua kiuchumi, hili pia linaweza kufanyika kwa wanaume pia kuwarudisha katika nafasi zao.

Mimi ninaamini akitokea mtu na kualika wanaume na vijana wa kiume kujifunza kuhusiana na uchumi na changamoto zinazowakabili ninauhakika wanaume wengi sana watahudhuria semina hizo.
Wazazi wachukue jukumu kufundisha watoto wao kujitambua, kujua majuku yao na kwamba siku moja atakuwa baba na atahitajika kulea familia, yapasa awajibike kulea mtoto aliemleta duniani, wazazi wawafundishe watoto wao tokea wakiwa watoto waijue miili yao na wasikubali kuchezewa miili yao.

Wazazi wawafundishe watoto wao wa kiume toka wakiwa wadogo juu ya familia, umuhimu wa kuwa na familia na kwamba familia ni baba, mama na mtoto na kujua baba ni nani na mama ni nani. Hizi elimu sio ngeni, zilikuwa zikitolewa zamani na mababu zetu, mwanaume alifundishwa jinsi ya kuyakabili maisha na changamoto mbalimbali, namna ya kukaa na mke wake na watoto, namna ya kujitafutia chakula (kama ni kuwinda au kulima) wanaume walifundishwa hayo.


Elimu ya Jinsia (Gender) itolewe kwa wanaume

Mwanamke amepata nafasi na fursa kubwa sana kujifunza kuhusu jinsia na hii elimu kwa kuwa imepandwa kwa wanawake, wanaume wamekosa nafasi ya kuielewa vizuri. Wanaume wapewe elimu kuwa, elimu ya jinsia haimaanishi kuwa mwanamke ni sawa na mwanaume bali inamaanisha kuwa mwanamke ana haki ya kupata fursa zile azipatazo mwanaume na si kuwa mwanamke apate fursa zaidi ya mwanaume. Elimu hii inapaswa kutolewa mashuleni, makazini katika taasisi mbalimbali na mtaani.


Wanaume waunde vikundi vya kusaidiana

Hili limesaidia sana wanawake wengi kujikwamua kiuchumi. Vicoba kwa mfano, sio suala la mwanamke pekee, wanaume pia wanaweza kujumuika na wanawake katika vicoba, vicoba havikuwekwa kwa ajili ya wanawake pekee na si kweli kuwa mwanaume akiwa kwenye kikoba ni mdhaifu. Ni wakati sahihi sasa kwa wanaume kuhamasishana juu ya kuunda vicoba mitaani na maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuweka akiba na kukopeshana.


Uhamasishaji

Ni kweli kabisa kuwa uhamasishaji unafanywa sana kwa wanawake. Mataifa yenye nguvu ya fedha imewekeza sana kwenye uhamasishaji wa mwanamke kwenye siasa, uchumi na jamii pia. Lakini uhamasihwaji huu umetafsiriwa kuwa mwanamke awe juu ya mwanamme kifedha, kimamlaka n.k jambo ambalo sio kweli. Uhamasishaji huu unalenga kumpa mwanamke aliekosa nafasi katika jamii apate hiyo nafasi, na kwa kuwa mwanamke akishawezeshwa ni rahisi sana kusambaza habari (hii ni kutokana na mwanamke alivyoumbwa hawezi kunyamaza mpaka asimulie mwanamke mwenzie) imesaidia sana tone moja la wino kwenye maji kufanya maji yote kubadilika rangi. Wanaume wanapaswa kutambua hili na kukubaliana nalo na wao kutumia nafasi hiyohiyo kubaki katika nafasi zao.

Wanaume wanaweza kuchukua fursa hizo kwa kuunda vikundi au taasisi za kumuhimiza (empower) mwanaume ajue namna ya kumuweka mwanamke katika nafasi au fursa pasipo kuvunja haki ya mwanaume.

Mikopo kwa vijana

Vijana wa kiume wachangamkie fursa za mikopo inayotolewa na serikali na taasisi binafsi. Vijana wanaweza kuungana na wake zao kufanya biashara za pamoja kwa kuchukua mkopo na kusaidiana katika kuendesha biashara zao.

Elimu ya vitendo ihamasishwe

Vijana wengi hawaoni umuhimu wa elimu za vitendo, hizo ndio elimu zinazomkwamua mwanamke kiuchumi, hakuna kazi ya mwanamke na mwanaume kazi zote ni kazi sawa. Wanaume pia wanaweza kufanya kazi za saluni, uchoraji, tamaduni, upishi nk vijana wanaofanya kazi hizi wamefanikiwa sana. Hivy vijana wasichague kazi na wasidharau kazi.

Mwisho

Huu ni wito kwako mwanaume kuitambua nafasi yako ili kuokoa kizazi kijacho , yatupasa kuokoa uchumi wetu na nchi kwa ujumla. Baraka zako mwanaume zipo katika kukaa katika nafasi yako, kufanya yalio majukumu yako kwa ufanisi.Kukua kiuchumi kwa taifa letu kutafanikiwa ikiwa wanaume watazitambua nafasi zao na kurudi katika nafasi zao bila kutoa visingizio. Yakupasa upigane na yule adui anaekumaliza nguvu. Vita ya uchumi katika nchi sio vita ndogo ni vita ya siri na akili kubwa! Ukishinda wewe tutashinda wote. Wanawake kwa wanaume yatupasa kufanya kazi kwa pamoja katika kulijenga taifa letu.
 
Upvote 10
Tushaamini uongo na tuuishi uongo. Tuendelee kujitawala kupitia mitazamo ya wengine.
Tulipo Sasa Mwanamke na Mwanaume Ni sawa TU.
Ideology n Theology zao zishamea. Itatuchukua miaka 500+ KUJIJENGA upya
 
Mbususu umwachie nani?
Mbussusu bila hela upati. Ndio tunataka mikopo hiyo tuwekeze tujiajiri tupate hela tule mbususu uchumi ukuwe.

Kwa mwanaume kula mbususu inamaanisha ametumia hela ambayo huyo mwanamke ataitumia kununua chupi mpya kiweka bundle mara sijui kununua savannah. So ni muhimu vijana kupata hii mikopo
 
Mshaanza kulia mapema hivi,
Tulieni dawa iwaingie eti kuokoa kizazi kijacho hicho kizazi kinatengenezwa na Mwanaume pekee?? Mnataka muingie na leba kabisa,

Umejaribu sana kutumia lugha laini lakini ujumbe wako upo clear.
 
Mbussusu bila hela upati. Ndio tunataka mikopo hiyo tuwekeze tujiajiri tupate hela tule mbususu uchumi ukuwe.

Kwa mwanaume kula mbususu inamaanisha ametumia hela ambayo huyo mwanamke ataitumia kununua chupi mpya kiweka bundle mara sijui kununua savannah. So ni muhimu vijana kupata hii mikopo
Wewe utahonga mkopo
 
Nini kinawafanya msiamue hadi sasa?
Mlivyojaaliwa kunung'unika mtatamani mtafute sayari yenu pekee, kina mama wa zamani tu ndio walioweza kuishi maisha ya kutegemea kauli za mkuu wa boma na utekelezaji unafanyika muda mfupi tu
 
Mshaanza kulia mapema hivi,
Tulieni dawa iwaingie eti kuokoa kizazi kijacho hicho kizazi kinatengenezwa na Mwanaume pekee?? Mnataka muingie na leba kabisa,

Umejaribu sana kutumia lugha laini lakini ujumbe wako upo clear.
Mwanaume atabaki kuwa mwanaume tu, hao mnaowaonea ni wanaume suruali, na miaka kibao walikuepo hawajaanza 2000 kama anavyosema mleta uzi.

Mwanaume anaheshimika kwa huduma zake kama baba, anaposhindwa ndo hizo dharau huanza kwa mwanamke kujikuta au kujifanya anataka kuwa baba[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mlivyojaaliwa kunung'unika mtatamani mtafute sayari yenu pekee, kina mama wa zamani tu ndio walioweza kuishi maisha ya kutegemea kauli za mkuu wa boma na utekelezaji unafanyika muda mfupi tu
Ni kwasababu sie sio wa kizamani. Na hao wamama wa kizamani ndo wametulea hivi
 
Ni ukweli usiopingika kuwa tokea mapinduzi ya kumkomboa mwanamke kiuchumi, kisiasa na kijamii wanawake wengi wamekuwa na nguvu sana katika nyanja zote za siasa, uchumi na jamii na kuwaacha wanaume nyuma...
KWANI WANAUME HAMPO KUPIGA KURA HII POST?
 
Naviwanawake vinavyozaliwa kwawingi sasa huko...mbeleni hakutakuwa na 50 kwa 50 kutakuwa 70 kwa 30..natunavyoendelea kuvionea huruma ndotunazid kuteketea kilakitu sahv kinachukuliwa nahawa vijike ..navinakingiwa kifuwa na mataasisi kibao kutuaminisha vinaweza...inanikera hii wanaume tuko hatarini kutoweka
 
Back
Top Bottom