Mwanaume, Tafuta mahari Umlipie Huyo Mwanamke, Hata Kama Hana Bikra

Mwanaume, Tafuta mahari Umlipie Huyo Mwanamke, Hata Kama Hana Bikra

3. Mahari si kwa ajiri ya kumnunua mwanamke bali ni fadhira kwa wazazi walezi wa binti.
Kama ni kulipa fadhila, kwa nini unasema ni lazima?

Kulipa fadhira mtu ajisikie mwenyewe sio iwe lazima, kukishakua na ulazima maana yake unanunua.

Hata ukienda duka la mangi, unampq hela ili kulipa fadhira halafu yeye anakupa mchele
 
NIMEASOMA HEADING TU.
Naunga mkono..

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI.

USIPOLIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA.

KUNA WANAUME WAPO KUZIMU WANAUNGUA NA MOTO KWA SABABU YA DHAMBI YA KUTIKUMALIZIA MAHARI..yani unakuta KALIPA NUSU TU HALAFU KAPOTEZEA..AU HAJALIPA KABISA...

WAHUBURI WA LEO HAWAHUBIRI WATU WAJURLE UKWELI..

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA KAMA DHAMBI NYINGINE.
 
NIMEASOMA HEADING TU.
Naunga mkono..

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI.

USIPOLIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA.

KUNA WANAUME WAPO KUZIMU WANAUNGUA NA MOTO KWA SABABU YA DHAMBI YA KUTOKUMALIZIA KULIPA MAHARI WALIYOPANGIWA UKWENI..yani unakuta KALIPA NUSU TU au robo tu akaahidi atamalizia kulipa mahari iliyobaki HALAFU KAPOTEZEA kajikausha kimya ..AU HAJALIPA KABISA...mahari anakaa na mtoto wa mtu

hata kama uliyemuoa hakuwa bikira bado ni sheria kulipa mahari,usipolipa mahari ni dhambi ambayo inaweza kukupelekea ukaishia kuchomwa moto ..motoni kabisa.

JAPO WAHUBIRI HAWAHUBURI HII SANA ILA.. NI MUHIMU KUELEWA..ILI SIKU UKIJIKUTA UKO MOTONI ..kwa dhambi ya kutokumaliza kulipa mahari au kutokulipa kabisa mahari usishangae ..useme nilikuwa sijui kama ni dhambi.

KUTOKULIPA MAHARI NI DHAMBI KABISA KAMA DHAMBI NYINGINE.
 
Hivi kwenye biblia kuna mwanaume yeyote aliye oa bila kulipa mahari??..bila kulipa posa??
Kuna baadhi ya manabii na mitume haikuwekwa wazi kama walitoa mahari, mfano eliya na hosea! Wafalme kama Saul na daudi pia, kuna ndoa nyingi kwenye biblia hazizungumzii mahari! Lengo kuu lilikuwa ni kufundisha zaidi na sio kuandika kila utaratibu wa familia..
 
SWALI: Je ulipwaji wa Mahari ina ulazima wowote?..je ni Agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo Je! Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?

JIBU: Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe…Na hakukuhusika mahari wala viapo…Hiyo yote ni kwasababu Hawa hakuwa na Baba wala Mama…

Lakini sasa wake zetu wanao wazazi wao..hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa..

Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao… Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.

Hivyo sio vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu…Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu…Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari. Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke…hapana! Bali kumthaminisha Yule binti kwamba hajaokotwa tu.

Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu..hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani..**hapo mahari ina ulazima wowote?..haina ulazima kwasababu wametoka kwetu(kwenye miili yetu kama Adamu)…lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine… Hivyo ni lazima mtu upitie hatua **za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake ikiwemo mahari,

Luka 2:4 “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba”.

Hivyo hatua hiyo ikishavukwa kinachofuata sasa ni kwenda kanisani…Tulipowatoa! tumewatoa katika jamii..watu wote walikuwa wanajua binti Yule hajaolewa..hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo..Na kijana naye vivyo hivyo anatamka kwa kukiri..kuwa ushuhuda..Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.

Hivyo ndoa na mahari ni mambo ya kimaandiko kabisa hata Bwana wetu Yesu Kristo aliingia gharama ili kututoa katika ulimwengu…Ilimgharimu uhai wake ili tu atupate sisi bibi-arusi wake..

Bwana akubariki.

Je umeithamini gharama Kristo aliyoingia ili akupate wewe?..Damu yake ilimwagika pale msalabani kwaajili yako na yangu..ili sisi tuwe mali yake yeye…tuondoke katika ulimwengu tukaishi naye..Kama hujaokoka unasubiri nini?..siku ile utakuwa mgeni wa nani kule au utakuwa mfano wa wale wanawali wapumbavu tunaowasoma katika kitabu cha Mathayo 25?..Uchaguzi ni wako, mlango wa rehema bado upo wazi.
 
Niliambiwa mahari laki tatu nikawaangaliaaa wale wazeee nikajiambia kimoyo moyo hiyo mahari yanini wakati Binti Yao kashabanduliwa vyakutosha 😂
Niliamua kuwakubalia nakuwaomba nikawataftiee hiyo elaa nilipo bahatika kutoka tuu njee sikurudi tena 😂😂😂 najua webint unasoma huu ujumbe ila siwez nunua kitu used Mimi 😂😂
 
Duhh laki 3??? Kaazi kweli..🤔
 
SWALI: Je ulipwaji wa Mahari ina ulazima wowote?..je ni Agizo la kibiblia? Na kama ni hivyo Je! Adamu alitoa mahari kwa nani ili ampate Hawa?

JIBU: Ndoa ya kwanza ilifungishwa na Mungu mwenyewe…Na hakukuhusika mahari wala viapo…Hiyo yote ni kwasababu Hawa hakuwa na Baba wala Mama…

Lakini sasa wake zetu wanao wazazi wao..hatuwatoi ubavuni mwetu kama Adamu alivyompata Hawa..

Hatuna budi kuwatoa kutoka kwa wazazi wao… Na wazazi wao waliwalea na kuwatunza kwa gharama zao.

Hivyo sio vyema kuwaiba kutoka kwa wazazi wao na kuwafanya wetu…Hatuna budi kufuata taratibu za kuwatoa kutoka kwao na kuwaleta kwetu…Na taratibu hizo zinahusisha ulipwaji wa mahari. Ulipwaji wa mahari hakumaanishi kumnunua huyo mwanamke…hapana! Bali kumthaminisha Yule binti kwamba hajaokotwa tu.

Laiti kama tungekuwa tunawapata wake zetu kama Adamu kwamba Mungu anatuletea usingizi na kuwatoa kutoka ubavuni mwetu..hapo kungekuwa hakuna haja ya mahari wala ndoa kanisani..**hapo mahari ina ulazima wowote?..haina ulazima kwasababu wametoka kwetu(kwenye miili yetu kama Adamu)…lakini tulio nao hawajatoka kwetu wametoka kwa wengine… Hivyo ni lazima mtu upitie hatua **za kuposa, na kuposa kuna taratibu zake ikiwemo mahari,

Luka 2:4 “Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi;

5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba”.

Hivyo hatua hiyo ikishavukwa kinachofuata sasa ni kwenda kanisani…Tulipowatoa! tumewatoa katika jamii..watu wote walikuwa wanajua binti Yule hajaolewa..hivyo binti kwa idhini yake sasa hana budi kwenda kukiri mbele ya umati wa jamii ya watu wake na mbele ya kanisa la Kristo na mbele ya Mungu kwamba amekubali kwa idhini yake mwenyewe kuolewa na kijana huyo..Na kijana naye vivyo hivyo anatamka kwa kukiri..kuwa ushuhuda..Na hapo ndipo Mungu anapoiridhia kuwa ni ndoa takatifu ya kikristo.

Hivyo ndoa na mahari ni mambo ya kimaandiko kabisa hata Bwana wetu Yesu Kristo aliingia gharama ili kututoa katika ulimwengu…Ilimgharimu uhai wake ili tu atupate sisi bibi-arusi wake..

Bwana akubariki.

Je umeithamini gharama Kristo aliyoingia ili akupate wewe?..Damu yake ilimwagika pale msalabani kwaajili yako na yangu..ili sisi tuwe mali yake yeye…tuondoke katika ulimwengu tukaishi naye..Kama hujaokoka unasubiri nini?..siku ile utakuwa mgeni wa nani kule au utakuwa mfano wa wale wanawali wapumbavu tunaowasoma katika kitabu cha Mathayo 25?..Uchaguzi ni wako, mlango wa rehema bado upo wazi.
Hivi mwanaume anakuwa hatunzwi kwa gharama za wazazi wake? Mwanamke hapaswi kutoa shukrani kwa wazazi wa mwanaume kumtunza mtoto wao?
 
Hivi mwanaume anakuwa hatunzwi kwa gharama za wazazi wake? Mwanamke hapaswi kutoa shukrani kwa wazazi wa mwanaume kumtunza mtoto wao?
Mwanaume ndiye ANAYEOA mwanamume ndiye anayemchukua mwanamke kutokaa kwa wazazi wake .mwanamke anakuwa SEND OFF kwwnda kwa mumewe...kifupi MWANAMUME NDIYE ANAYEOA
 
Mwanaume ndiye ANAYEOA mwanamume ndiye anayemchukua mwanamke kutokaa kwa wazazi wake .mwanamke anakuwa SEND OFF kwwnda kwa mumewe...kifupi MWANAMUME NDIYE ANAYEOA

×
Search …
JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO.
Home / Home / JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO.
kabla ya kuingia huko
JIFUNZE KUELEWA MAANA YA KUOA/KUOLEWA KABLA YA KUINGIA HUKO.
Jina la Bwana wetu Yesu Kristo libarikiwe.

Kama wengi wetu tujuavyo, Ndoa ya kwanza ilifungishwa pale Edeni na Mungu mwenyewe. Na ilikuwa ndoa takatifu, iliyobeba msingi na dira ya ndoa nyingine zote zitakazofuata jinsi zinavyopaswa ziwe.

Katika ndoa ile ilihusisha Mtu mume mmoja (Adamu) na mtu mke mmoja (Hawa)..Kwa kupitia wazazi wetu hawa wawili ndio sisi sote tumetokea…ikiwa na maana kuwa ndoa kamili na takatifu inahusisha mume mmoja na mke mmoja…na si Zaidi. Hicho ni kigezo cha kwanza na cha muhimu.

Pia kabla ya ndoa ile kufungishwa, Maisha yalianza na Adamu kwanza, Mungu alimpa Adamu mimea, mashamba ya kulima, makazi na kila kitu, hapo kabla Hawa hajatokea…na Adamu akaanza majukumu yake ya shughuli pale Edeni kabla ya Hawa kutokea…Na Hawa alipotokea alikuwa kama msaidizi tu wa kazi ambayo tayari ilikuwa imeshaanza. Ikiwa na maana kuwa Mwanamume yoyote kabla hajadhamiria kuoa ni lazima angalau awe na mahali pa kujishikiza ili aweze kumhudumia huyo mkewe anayekuja kumwoa…

Na kumbuka Mungu hakumleta Hawa kwaajili ya tamaa za mwili za Adamu, hapana bali alimleta ili awe msaidizi kwake, kwa namna zote, kifikra, na hata katika kazi zake za kimaendeleo Adamu alizokuwa anazifanya…Ikiwa na maana kuwa lengo la kwanza la ndoa sio kukutana kimwili kama inavyochukuliwa sasa na wachache wasio na maarifa ya kutosha.

Hivyo mwanamke jukumu lake kubwa katika ndoa ni kushirikiana na mume wake, na kuyafanya majukumu yote ambayo mume wake angepaswa ayafanye, ikiwemo ya kihuduma na ya kiuchumi, Hawa hakupelekwa kwa Adamu kumtoa Adamu pesa!..bali awe msaidizi….Maana yake kitu ambacho hakijakaa sawa au hakijakamilika mikononi mwa mwanaume, mwanamke anakiweka sawa na kukimalizia.

Na jukumu kubwa Zaidi mwanamume na mwanamke walilopewa ni kujiepusha na Uovu…Na shetani huwa anawatumia wanawake wengi kuharibu ndoa kuliko wanaume..Kama Hawa mzazi wetu wa kwanza angekaa katika nafasi yake na kujiepusha na uovu, leo hii duniani kungekuwa ni paradiso, lakini kwa kuacha majukumu yake ya USAIDIZI na kwenda kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambayo Mungu hakumwagiza matokeo yake ndio yakawa yale…Na hata sasa mwanamke akiacha majukumu yake na kujikita katika ulimwengu huu, katika usengenyaji, umbea, katika kutoa siri za mume wake nje, katika kutomheshimu mume wake, kumdharau, kumdhalilisha, kumwaibisha, kuvaa kikahaba, kuwa mhuni, mlevi,mtu mwenye mizaha na kila aina ya udunia, anajiharibia mwenyewe na anaibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe..

Na Ndoa takatifu ni lazima ihusishe watu wawili wenye Imani moja..Ni kinyume na maandiko kuoa/kuolewa na mtu asiyeamini baada ya wewe kuamini, Kama umeshamwamini Yesu Kristo na uweza wake hupaswi hata kidogo kutafuta kuoa/kuolewa na mtu asiye mkristo. Na ndoa yoyote ya kikristo lazima iwasilishwe na kubarikiwa mbele ya kanisa la Kristo. Sio sahihi kabisa kufunga ndoa za kimila wala za kiserikali baada ya kumwamini Yesu Kristo.

Na ni lazima kulipa mahari kwa ndugu wa mwanamke kabla ya kumwoa, kama huo ndio utaratibu wa familia ya mwanamke, Adamu hakulipa mahari kwasababu mkewe Hawa ,chimbuko lake lilikuwa ubavuni mwake, hakuwa na wazazi wala ndugu…lakini sasa kila mwanamke anao wazazi/ndugu/walezi…Huko ndiko alikolelewa, hakulelewa ubavuni mwako,…kwahiyo ni wajibu kumtoa kwa wazazi wake kwa utaratibu huo maalumu wa kulipa mahari…

Hata Hawa alipotolewa ubavuni mwa Adamu, Bwana Mungu aliparudishia nyama pale palipotolewa ili Maisha ya Adamu yaweze kuendelea, hakuacha shimo pale wala kidonda!…Na hali kadhalika unapomtoa mwanamke kwa wazazi wake ni lazima uzibe pengo uliloliacha pale, na hilo unaliziba angalau kwa mahari, sio unamwiba na kuacha huzuni kule na malalamiko na laana na maumivu.

kama utashindwa kulipa mahari ya kiasi hicho kidogo cha fedha utawezaje kuitunza na kuihudumia familia yako inayokuja huko mbele, ambayo pengine itahitaji matunzo ya gharama nyingi kuliko hizo za mahari??…kama hutaki kutoa mahari, maana yake bado hujaelewa maana ya kuoa, hivyo unapaswa ungoje mpaka utakapoelewa vyema maana ya ndoa ndipo uoe.

Na mwisho biblia inatuambia kuwa wakati tuliobakiwa nao ni mchache sana…wale ambao wameoa na wawe kama hawajaoa…ili muda mwingi tuutumie katika kuutafuta Zaidi ufalme wake na haki yake kwasababu unyakuo upo karibuni, na mbinguni tuendako hakutakuwa na kuoa wala kuolewa, yatakuwa ni mambo mapya huko ambayo ni ya muhimu Zaidi kuliko haya.
 
Mwanaume ndiye ANAYEOA mwanamume ndiye anayemchukua mwanamke kutokaa kwa wazazi wake .mwanamke anakuwa SEND OFF kwwnda kwa mumewe...kifupi MWANAMUME NDIYE ANAYEOA
Kwani mwanaume hatoki kwa wazazi wake? Hii mahali wala si shukrani ni kuuziana tu ndo maana binadam anabadirishwa hadi na Ng'ombe yaan anakuwa bidhaa hata huko aendako mwanaume humfnyia vyovyote kisa katoa mahali kwao.
 
kwani wapo waliobakwa,waliozaliwa na bila bikra,wapo waliopoteza kwa bahati mbaya,wengine wapo waliopoteza kutokana na shughuli za kibinadamu,kama kuendesha baiskeli
Mada nzuri ila hii kauli haina uhusiano na mada husika. Yani hapa umeucheza mwingi ukaenda offside
 
Basi inatosha!Umelalamika sana.. Tutaanza kuwatolea ninyi sasa🫢
Nani kasema mtutolee mahari tena😀😀.Mimi tu nimehoji tu hiyo sababu ya kutolewa mahali kama ni shukrani kwa wazazi wa mwanamke kumtunza mtoto wao kwa gharama zote hizo ndo nikauliza kwani wazazi wa mwanaume hawatumii gharama kumtunza mtoto wao na hawahitaji shukrani ila wa mwanamke wanahitaji? Cause kama mpaka anakuja kukuoa na inamaanisha aligharamiwa vyema na kulelewa vyema kuliko hata wewe mwanamke kwann nyie msiwashukuru kwa kuwapa binti bure huyu tu.
 
Zamani wanaume na vijana walilipa maali kama asante kwa wazaz kwa kuzaa na kumtu bint/msichana sasa sikuiz akuna mabint/wasichana bali kuna wanawake ma wamama sasa utalipa maali uoe au unalipa ili mkasogezane maisha
 
1. Ukimlipia mahari mwanamke,huyo anakuwa mali yako,atakuheshimu na kudumisha ndoa

2. Ukimlipia mahari,watoto mtakao zaa nae wanabelong kwako si kwa upande wa mwanamke.

3. Mahari si kwa ajiri ya kumnunua mwanamke bali ni fadhira kwa wazazi walezi wa binti.

4. Mahari huleta maelewano kati ya wanandoa,na familia kwa ujumla,usipotoa mahari,kuheshimiana huwa ni kidogo sana,ugomvi usioisha kwa vile haujatoa mahari akienda kwao huwezi kumwambia lolote

5. Mahari haijaanza leo,ni jambo la toka kale,hivyo ni vema tamaduni zidumishwe

NB: kigezo cha kusema kutoa mahari ni mpaka mwanamke bikra haina mashiko,kwani wapo waliobakwa,waliozaliwa na bila bikra,wapo waliopoteza kwa bahati mbaya,wengine wapo waliopoteza kutokana na shughuli za kibinadamu,kama kuendesha baiskeli nk nk. KUTOA MAHARI NI JAMBO LA LAZIMA.
Acha ujinga wewe. Yaani katika ufala unaoweza ukafanya duniani ni kumlipia mahari mwanamke asiye na bikra. Mwanamka kama hana bikra we chapa tembea. Kama umempenda sana, basi tia mimba zaa naye mlee mtoto au watoto. Lakini sio kulipia mahari.

Wote waliolipia mahari wanawake ambao hawakuwatoa wao bikra ni mafala.

Mahari ni asante kwa wazazi kwa kukutunzia binti yao. Kinachotunzwa ni bikra.

Halafu mahari ya mwanaume kumlipia mwanamke haipo duniani kote. Iko huku Afrika, Uarabuni na China. Ila Wazungu na Wahindi jadi yao ni mwanamke ndo anayelipa mahari kwa mwanaume. Na hili ni jambo la akili sana kwa sababu mwanamke ndo mwenye shida ya ndoa. Hautakuta mwanaume hata siku moja anaenda kanisani au kwa mganga kutafuta ndoa.
 
Tena siku hizi mahari bei chee! Sana eti unakuta kabinti ka 19 kamefeli zake form four low mileage ka astadhati fulani eti wanakutoza milioni moja tu! Hapo wanakutegea utashuka shuka hadi 700k. Aisee kanatii amri tu ndani kanakuzalia watoto wazuri tu.. Aisee!
Kobaz kwa umalaya mko vzr Sana
 
Back
Top Bottom