Usalama wa Mchepuko
Ni kipaumbele namba One unapofumaniwa maana yeye ndio target ya fumanizi.
Tumeshuhudia Sana Mwanaume ukilegea,eti unakimbia unaacha msala mkubwa nyuma.
Atachaniwa nguo zake zote, kutemewa mate na kutembezwa barabarani uchi na vichapo kibao chungu mzima[emoji4]
Umenikumbusha mbali kidogo. Wife alimjua manzi ambae nilikuwa nachepuka. Akafanya umafia akamteka akiwa na njemba kama tatu hivi. Wakamtaiti yule ikiwemo na kumchapa sana.
Then wakapekua simu ya manzi wakapata ushahidi wa kutosha maana yule manzi alikuwa hafuti maujinga tuliyokuwa tunachati.
Badae jamaa mmoja wao akanipigia simu kwa namba ya yule manzi kwamba amepata ajali ya boda so niende nikamsaidie yule manzi. Mm nilikuwa mitungi nikawaambia wampe manzi niongee nae. Wakanipa sasa yule manzi akawa haongei ila analia tuu.
Wakanielekeza nikaenda hiyo mitaa. Kufika namkuta wife yale maeneo kwa nje. Nikajua leo kimenuka. Wife akanambia njoo huku umuone mchepuko wako.
Nikaingia ndani namkuta yule manzi kataitiwa na jamaa wawili, wakijifanya ni maaskari. Wife ndo kubwa la maadui akitoa amri wale miamba wanatekeleza, dah.
Kifupi pale pale nikawageuzia kibao hawakuamini. Kesi zilikuwa kama ifuatavyo.
1. Mna kesi kubwa ya kuteka mwanamke na kutishia usalama wake.
2. Hata kama ni mtuhumiwa ilibidi ajulishwe aende mwenyewe polisi au kama kukamatwa akamatwe na afande mwanamke tena mwenye RB.
3. Mna kesi kubwa ya kuingilia privacy ya mtu kwa kupekua mawasiliano yake kinguvu bila ridhaa yake.
4. Mna kesi ya kuharibu mali ya mtu maana mmemwaribia simu yake na kumpora vitu vya thamani kama vile fedha na mikufu ya thamani. Hii ya fedha na mikufu niliizusha tuu kuzidi kuwavuruga.
5. Mna kesi kubwa ya kunipotezea muda wangu nimeacha shughuli zangu kwa ajili ya ujinga wenu, itabidi wote mfidie hasara niliepoteza maani kwa muda ule niliacha dili la pesa.
Na nikawaambie wanisubiri hapo hapo naenda kituo cha jirani kuwachukua polisi ili waje wawakamate watuhumiwa.
Na nikamwambia yule demu mbele yao kwamba polisi wakifika pale aseme wamemteka pale kwa siku mbili na wamempora vitu vyake, mm nitakuwa shahidi yake.
Wale jamaa wswili waliondoka bila kuaga. Badae nikamwambia yule manzi aondoke. Then nikamwambia wife kama unabaki hapo endelea kubaki mm narudi kwenye mishe zangu tutakutana usiku nyumbani. Nikasepa.