Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Wikiend iliyopita, nilikuwa nimejichokea kiaina; nikaona bora niende zangu 'club' moja ya karibu angalau nipate kinywaji kidogo, huku nikiburudika na mziki pamoja na kuosha macho kwa watoto wazuri.
Baada ya kuingia club, mhudumu akaniongoza mpaka kwenye meza moja ambayo haikuwa na mtu; nikamwagiza kinywaji changu, na kumsisitiza anihudumie mpaka mwisho nitakapoondoka pale ukumbini.
Ilikuwa mida ya saa nne usiku, watu wanazidi kuingia na mambo ya ukumbini yanazidi kufana vizuri. Watoto waliopiga pamba kali, viuno vya nyugwi n.k wakazidi kupendezesha ukumbi.
Kwa wastani tu; warembo walikuwa wengi sana, na walikuwa wazuri. Ni wewe tu, na makali ya meno yako.
Imefika saa sita usiku pombe ikawa imeniingia vizuri kichwani, hakuna kuona aibu. Nilishangaa nimegeuka nyuma yangu, nikaona bonge la kifaa 'my type', nikajikuta nimepata ujasiri wa kumshika mkono na kumvuta karibu na meza niliyokuwepo.
Nikashika kiganja cha mkono wake na kukiweka kifuani kwangu, na kuanza kumpa sifa za hapa na pale. Baadaye nika-kiss kiganja chake, nikamwita aliyekuwa ananihudumia alete kiti kingine, na aongeze vinywaji.
Tukaanza kufahamiana, yeye ni mke wa mtu na ameajiriwa wizara R na kwa sasa yupo masomoni, hapa mkoani. Nikamwambia hakuna matata, tutakuwa tunapeana kampani pale inapobidi.
Ghafla DJ akapiga mziki wa msanii K-Ci & jojo, nikajikuta namwinua mtoto tukaanza kucheza 'zero distance' huku akikizungusha kiuno taratibu bila kuchezesha kifua. Dah... wakubwa wanafaidi sana wakuu.
Sijakaa sawa, midomo ikawa inawasiliana kwa nguvu ya sumaku; muhudumu naye analeta tu vinywaji huku naye akiwa anajihudumia.
Kuja kucheki kwenye 'wallet' pesa imekata, na kuondoka ukumbini nikalale siwezi; ikabidi nimwambie mrembo nisindikize 'home' nikaongeze mpunga.
Ikabidi niwaage mabaunsa pale mlangoni, ninarudi; ili wasinichaji gharama zingine za kiingilio.
Baada ya kufika 'home' nikamuacha mrembo sebuleni, nakwenda chumbani kwangu na kuchukua salio kidogo.
Sikupenda kuwa na papara ya kumtaka kimapenzi hapo 'home', nilitaka ajue hivyo vitu sio vigeni kwangu.
Tukarudi 'club'; baada ya kufika tukaendelea na vinywaji mpaka kwenye saa kumi usiku; baada ya hapo tukaagana na akaniahidi, atanitunuku wiki ijayo tukishafahamiana zaidi.
Nikajibu, ok hakuna tatizo.
Nilipofika nyumbani, nikajitafakari; nikaona wiki ijayo mbali, ikabidi nijifanye ninaumwa.
Palipokucha, majira ya saa nne asubuhi, nampigia simu, kumjulisha hali yangu si nzuri kutokana na uchovu wa mkesha. Namuomba aje anijulie hali nyumbani; naye akanijibu, atakuja mida ya jioni.
Kufika mida ya saa moja usiku, mtoto huyu hapa anagonga mlango. Nikamkaribisha, nikampa 'wine' kidogo huku akiwa amekaa kwenye sofa.
Tukawa tunapiga stori huku tukiendelea kupata kinywaji chetu, pamoja na kusikiliza mziki wa taratibu.
Baada ya muda, nikamsogelea kwenye sofa alilokuwa amekaa, na mambo mengine yakaanza kuendelea.
Kuja kushtuka tupo chumbani; Yale mambo ya wiki ijayo yakawa yametimizwa ndani ya siku moja.
Kwa sasa tunaitana 'honey'