Mwanaume unapotoa pesa za maelezi hakikisha watoto wanajua lasivyo hawataona umuhimu wako na kudhani mama yao ndie anaekamilisha kila kitu

Mwanaume unapotoa pesa za maelezi hakikisha watoto wanajua lasivyo hawataona umuhimu wako na kudhani mama yao ndie anaekamilisha kila kitu

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
skks.jpg


Walengwa:

1. baba alietengana na mzazi mwenzake ila anaendelea kutuma pesa ya matumizi ya mtoto

2. Baba ambae anaishi nyumba moja na familia yake lakini anampa mke wake pesa ya chakula cha familia , mavazi, elimu, n.k bila watoto kujua.

aliotengana na ambao wanakuwa nje ya nyumba kikazi kwa muda mrefu

Unapowahudumia watoto kwa kumpa mama yao hela ya matumizi, hakikisha sometimes watoto wanajua kuwa wewe ndio unahudumia! wamama wengi huficha hii taarifa muhimu kwa watoto na inakuwa rahisi kuwajaza sumu kuwa wao ndio malkia wa nguvu wnawapambania kila kitu, hata wasipowaambia ni rahisi mtoto kujenga hi picha na kumuona baba yake hana umuhimu, watoto wanaweza hata kuanza kumuona baba yao ni kama mgeni asie na msaada wowote na hata kumpandisha zaidi cheo mama yao

hakikisha unapokua na watoto out bila mama yao geuza hio hali iwe uwanja wako wa kunyakua points, watoto wanapenda sana utoto na huo ndio udhaifu inabidi wao uutumie ili wakuone wa maana, wamezoea kula ugali wewe wanunulie sambusa, wamezoea kucheza game za simu ya mama gao wewe wapeleke zile center zenye magame makubwa, wamezoea kunywa maji wewe wapeleke vibanda vya juice, wavulana wanunulie vifaa vya michezo,
 
Ukitaka kununua nguo nenda naye fulani. Ukiileta kwenye rambo mama anaiweka kama wiki hivi halafu anamvalisha -asante mamaaa
Ukituma hela ya kununua vifaa vya ujenzi anatangaza kwa mashost kesho naenda saiti nimenunua vifaa.
 
Ni mungu tu aisee ndio anajuwa Hawa mitoto hawatambui kitu wee toa kausha tu
 
Ukitaka kununua nguo nenda naye fulani. Ukiileta kwenye rambo mama anaiweka kama wiki hivi halafu anamvalisha -asante mamaaa
Ukituma hela ya kununua vifaa vya ujenzi anatangaza kwa mashost kesho naenda saiti nimenunua vifaa.
zawadi inabidi unamtegea anapotoka shuleni ndio unampa
 
Tulishalizungumzia hili kwenye kikao cha mwisho na lilipitishwa kwa kura ya wajumbe wote.
 
Tulivyokuwa watoto tulikuwa tunawapenda mama zetu lakini siku hizi ndio tunawaelewa vizuri baba zetu na kuwathamini
 
Ni mungu tu aisee ndio anajuwa Hawa mitoto hawatambui kitu wee toa kausha tu
Umaskini mbaya sana. Watu wanafikiri hela ndio kila kitu. Hao ni watoto hawajui hata thamani ya hela. Wewe toa hela halafu waimbie hela umeleta wewe halafu usiwe karibu nao utajua hujui. If you are not there, utapoteza connection na hii ndio muhimu kuliko material things. What if mama yao ana pesa kuliko wewe? Connection yako na wao ndio kitu pekee muhimu kwa uhusiano bora na watoto wako.
 
Tafuta pesa jiwekee akiba ya uzeenii na sio kusumbua watoto.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom