Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?

Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?

Kwa sisi tuliooa WACHAGA,

Suala la kulala ukweni ni MARUFUKU! Yaani SAHAU!

Kwanza binti akishaolewa, YEYE mwenyewe haruhusiwi kulala kwao, sembuse wewe??

Mimi alifariki baba mkwe, nililala lodge wiki nzima. Kila siku naenda msibani asubuhi, usiku narudi lodge kulala.
Kwa hiyo ulikuwa unalala lodge na mkeo?!
 
Mi nimeoa njombe, huwa naitwa jioni na mama mkwe naenda Kuota moto!! Ukweni ni kwenu pia!
 
Hilo neno la mwisho linaharibu utamu wa maudhui uliyotoa hapo mkuujuu yaani hapo umeonesha ww ni mwakilishi wa hao wanaokaa ukweni.

Back to the point kwakweli binafsi ukweni labda uwe ni msiba mzito ndo unaweza kuniweka siku3 kinyume cha hapo ni siku mbili au moja nasepa tena nitarudi huko baada ya muda mrefu kupita kama hakuna shida yoyote
Mkuu kukaa ukweni hata mie siwez kabisa... Sijui kwanini huwa sipendi...nikikaa sana massa matatu
 
Sasa afanyejeee? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Avae bukta ndefu au suruali. Aweke taulo begani.
Sasa yeye anafunga taulo halafu kifua wazi.
Mama mkwe yupo na mashemeji wa kike. Inatia kinyaa
 
Avae bukta ndefu au suruali. Aweke taulo begani.
Sasa yeye anafunga taulo halafu kifua wazi.
Mama mkwe yupo na mashemeji wa kike. Inatia kinyaa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamaniiiii
 
Mimi ukimuoa Dada yangu alafu uje kulala kwetu siku 1 tu nikikukosakosa sana nakupiga mitama siyo chini ya 15 na makofi ya kutosha.

Ila nikija kuoa kwenu nakuja kulala hapohapo kwenu na ukileta mazoea nakukanda mbele ya dada yako
 
SIjui mila desturi na taratibu za makabila mengine. Ila ukweli hata kama umeoa kwenye familia ya kitajiri kwenda kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili aisee unajidhalilisha.

Mzee wangu aliniambia ukikaa ukweni siku mbili zinataosha sana ya tatu unaondoka hii ni kwamba usijue maisha yao na wao wasijue mipango yako. Ukikaa sana ukweni kuna siku utatumwa chumvi dukani uone wanakudharau kumbe mipango yako sio.

Chini ya hili jua kuna wanaume achilia mbali kwenda kusalimia ukweni, wapo ambao wanaishi ukweni. Na hapo mtu anahitaji haishimike. Aisee ukiona unaishi ukweni na mwanamke anakuheshimu wee jamaa hata mbingu ni yako. Nawasilisha.
Kuwa uyaone baba watu mwaka wa kumi huu na kazini unapiga stori na wewe mwenye nyumba na mtaani natoka nimejifunga khanga watoto shikamoo nyingi huku nasugua meno na mswaki wangu wa jero maisha hayakupi unachotaka,Maisha kama mapenzi hayana fomula.
 
Kuwa uyaone baba watu mwaka wa kumi huu na kazini unapiga stori na wewe mwenye nyumba na mtaani natoka nimejifunga khanga watoto shikamoo nyingi huku nasugua meno na mswaki wangu wa jero maisha hayakupi unachotaka,Maisha kama mapenzi hayana fomula.
Asante.
 
Kume JF nzima watu mmeoa na kuolewa? Mnatuzingua wengine kataa ndoa kumbe mna wake/waume😀😀, alafu kwenye mada zetu pendwa za kula tunda kimasihara tuko pamoja wazee mnafeli wapi😀.

Na wengine tuko jukwaa moja la pisikali, kumbe kaoa, oyaa wanandoa mnazingua mjue?,
 
Back
Top Bottom