Mwanaume usikubali kuuza nafasi yako uliyopewa na Mungu kama kichwa cha familia, hata umpende mwanamke kiasi gani nafasi yako ndio heshma yako

Mwanaume usikubali kuuza nafasi yako uliyopewa na Mungu kama kichwa cha familia, hata umpende mwanamke kiasi gani nafasi yako ndio heshma yako

Anza na Mungu hutapungukiwa. Ukianza na Mungu mengine yote utafanya na Mungu. Ukianza na Mungu utakua na imani na utafata taratibu za imani yako na za jamii yako pia

Sio kwa walokole tuu Hii ni kwa imani zote
Asante sana

Hallelujah
 
Mondi na mama yake lazma waonekane wapo sahihi sababu wana power....

Naona umeamua kumpa Abdul sapota😎😎 Kumbuka hata mambo yalipokua magumu Sandra hakumtelekeza mwanae ila Abdul alifanya hivyo na kurudi baada mtoto kuwa maarufu😎

Sijamsikia Abdul kwenda bakwata kutafuta suluhu na sababu ni kwamba hakusimama kwenye imani yake wakati anayofanya hayo yanayomgharimu sasa

Sijawahi msikia kwenda kutafuta suluhu ya huyo anayesema ni mwanae kwa familia ya Sandra, sababu ni kwamba hakufata taratibu za kifamilia hakuo, hakutoa mahari wala hakwenda kumkomboa mtoto zaidi alikua anadeal na media tuu

Sijamsikia kusema nilikua nalipa kodi ya pango kiasi hiki kwa landlord huyu kwaajili ya Sandra na mtoto

Sijamsikia Abdul kusema hizi hapa receipts nilizokua namlipia mwanangu ada ila nimemsikia akihadithia alivyouza deki akaenda kumflush Sandra mimba

Sasa wewe sapota nzuri ya kumpa ni kwenda kupima DNA kuprove anachosema kwamba ilipasuka nasib akapatikana ili arudishe heshma yake na mwanae
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
nimecheka sana hahahahaaa

Wale wanaolalamika kwamba wanawake wanapenda fweza kwanza kabisa ijulikane ni wale wasiotunza wanawake wao bila kukumbushwa.... Nina uhakika hawajui wao ni kina nani na walipewa majukumu gani kiimani na kiasili

Ila Chakorii tuache utani hakuna mwanaume au mume mwenye raha na amani kama yule anayetimiza wajibu wake bila kukumbushwa na kuombwa
Yani huu utandawazi umekuja kufanya wanaume waone mwanamke haitaji kuhudumiwa😆😆jamani...

Wanawake kazi yetu ni kuwatii wanaume.
Wanaume kazi yao ni kutupenda 😄😄sasa hapo kwenye kutupenda,ndo kuna kodi,tuma na yakutolea,nywele zimefikumuka,birthdayz,simu mbovu,na mengineyo yafananayo na hayo hapo juu
 
Mama Nasib ataendelea kuwa shujaa na malikia kwa watoto wake
Baba mlezi alikimbia, sasa yeye mama.afanye nini nikuchukua majukumu , mambo yamekuwa mazuri anaibuka haà haa, shakushangaza licha yakukimbiwa lakini yeye alifunga mkanda, mpaka kumtoa mwanaye nashangaa matusi kwake, wamuulize kwanini baada ya kuondoka hakurudi kwa kwa ajili ya mtoto, apambane tu na hali yake!
 
Ukikutana na mwanamke mpumbavu katika maisha yako, matokeo yake ni kama haya. Kumbe hata huyo mzee Abdul alijitahidi, kulea damu sio yako, eti alimpeleka mama hospitali kujifungua kumbe hata mtoto sio wake.

Matokeo ya kukutana na mtu asiye sahihi kwako.
Lakini alikuwa anajua si kwamba alifichwa ni mapenzi yake!
 
Eli79 sasa kama Abdul alikua analala na mama nasib nyumbani kwa wazazi wake alipopata uchungu angebaki nyumbani na mamamkwe halafu majirani ndio wampeleke Amana!?

Mama Nasib kasema ni kweli alimpeleka hosp lakini hajawahi mlea nasib...... inaelekea mzee nae alikua analelewa tuu
Wamuulize kwanini hakuwa na maisha yake akamchukua mkewe ? Unaishi vipi ukweni hata kama utawanunua misosi lakini patabaki ni ukweni tu.
 
Wamuulize kwanini hakuwa na maisha yake akamchukua mkewe ? Unaishi vipi ukweni hata kama utawanunua misosi lakini patabaki ni ukweni tu.
halafu utasikia kuna watu wanamtetea kwa nguvu kabisa hapa
 
M

Mzee zaidi ya miaka 8,yupo kwenye makamera.
Alafu sijui anajishughulisha na nini?

Huyu yeye sasa hivi achane na makamera asimame kama mwanaume,hana uzee wa kusema hawezi kufanya kazi ,kama ikiwezekana apotezee awalee watoto wake aliowapata uzeeni,kama kweli kaonewa malipo hapa hapa.Ila kama kweli hakuyabeba majukumu basi anacho kipitia anastahili.

Au nae alikiwa Mario kama mzee Shamte,manake kwenye mahojiano ya SnS alisema,haiwezekani watu wasiojulikana wapate kingi kuliko yeye,kama ile nafasi ya Shamte bado anaitaka.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] atakuwa anaitamani sana hiyo nafasi ya Shamte, miaka yote 8 sizani kama hata 40yrs alikuwa kafikisha sasa kutwa daa sijui hana ndugu wakumshauri!
 
Alipoondoka hakuwahi wasliana na mtoto wala mama hadi aliposikia umaarufu ndio akajongea
Achilia mbali hayo mambo mengine Nampa mwanamke mwenzangu kwa kumlea mwanae hadi kumfikisha alipo
Pongezi zake nyingi sana
 
Walimvumilia muda mrefu na kumwomba sana aache kwenda kwenye media ila yeye akatumia Hilo jina kama fimbo kumchapa mama nasib na mwanae
Sasa mama kachoka utumwa
Kayataka mwenyewe, anataka haki ambayo hakuitafuta
 
Hahaa nasikia alimuacha na kukimbia na kijana kutoka south, mimi naona wote wana makosa, huyu mama alikua anatafuta security, ni makosa tunayafanya wanawake kila leo, baba dai angekua na kazi ya kumuingizia kipato leo Daimond angekua mwanae( namaanisha mama yake asingechepuka)...story yao tunatengeneza matukio [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Mbona anasema alikuwa mpaka na magari kilimfanya nini asitafute chumba akaishi na mrembo Sandra? Hivi kuishi na mwanaume nyumbani kwenu unaionaje na huku ukiwa na ndugu zako? Kama alivyo ondoka angekaa huko huko kimya si alisusa!
 
Tangu ijumaa tarehe 15 January 2021 imekua siku mbaya sana kwa bwana Abdul Jamaa aliyekua akijulikana kama baba Nasibu au Mzee Dangote.
Hii issue ya mzee Abdul itapita lakini sisi kama jamii tuna jambo kubwa sana kujifunza haswa kwenye mahusiano na hata kwenye malezi.

Kwa wale waamini wa Mungu vitabu vitakatifu vinatoa miongozo mizuri kuhusu tunavyotakiwa kuishi, na hata wale wasioamini kwa Mungu miongozo hii ni muhimu kwani ndio sheria na taratibu za kudumisha amani na nidhamu kwenye jamii.

Mungu alimuumba mwanaume kwanza kabla ya mwanamke, na alifanya hivyo akijua umuhimu wake wa kuwa hapa duniani na uwezo wake wa kubeba majukumu. Mungu alipoona amekua mpweke alimpa mwanamke ili awe msaidizi wake. Na katika maandiko pamoja na mambo mengine maandiko yanaongelea wajibu na majukumu ya mwanaume na mwanamke.

Wanaume vaeni viatu vyenu, hata kama una mwanamke anaweza kufanya baadhi ya majukumu usibweteke sababu wanawake hufanya vitu wakiwa na mapenzi ila mapenzi yakiisha hubaki kuwa fedheha kwa mwanaume.

Tumemwona mzee Abdul alivyokwisha dhalilika na anavyoendelea kudhalilika na kuumia. Huyu mzee inawezekana kabisa kwenye ujana wake alisahau nafasi yake sababu ya mapenzi tuu aliyokua anapata, akasahau kwamba mambo yanaweza kubadilika.

Yeye anadai nasibu ni mwanae kabisa bila wasiwasi wowote lakini pia ukimsikiliza utagundua utakwamba hakuwahi kubeba majukumu yake ndio maana anakosa hata pa kusimama walau kuutetea utu wake tuu. Mambo yamemuwia magumu sababu hajawahi simama kwenye nafasi yake kama baba au mume kijamii wala kiimani

1.Hakuwahi kumuoa mama Nasib kwa kufuata taratibu zozote za anasema, za kiserikali au za kimila. Kwa maana ya taratibu huyu mwanamke hajawahi kuwa mke wake kitu ambacho kilipelekea kuzaa
~Hapakua na makubaliano

2.Mzee Abdul Jumaa kama mwanaume hakuwahi kumiliki makazi akamchukua mama Nasib na kuishi nae ndani kama familia. Anasema yeye alihamia nyumbani kwao mama nasib, nyumba aliyokua wanaishi wazazi wa mama nasib pamoja na ndugu zake wengine
~Kuishi ukweni hata kama umeoa ni fedheha kubwa sana kwa mwanaume. Sasa hapa huyu kijana wa zamani alikosea sana maana hata hakuwa ukweni, hakuwa ameoa wala kulipa mahari

3.Mzee Abdul anasema kisa cha kutengana ni kwamba mama Nasib alitoka akaenda kwa mwanaume mwingine hadi saa nane ya usiku akawa hajarudi
~Akufukuzae hakuambii toka. Hii familia walimchoka wakamuona mzigo sababu anaishi kwao, ndio maana mama nasib akawa na guts za kwenda huko anakosemekana kwenda ili jamaa aondoke

4.Baada ya kuondoka Mzee Abdul anasema hakuwahi kurudi wala kuwasliana na mama Nasib wala nasib hadi alipoanza kupa umaarufu
~Hii ni wazi kwamba mzee yalimfika hapaaa!!! Na kwakua hakuacha kitu (mke wala mtoto wa damu) haikua shida kwake kuwacancel na kuendelea na shughuli zake.... bila kujua kwamba na wao wamemcancel na kuendelea na mambo yao

Baada ya Nasib kupata umaarufu mzee Abdul alianza kurudi sababu anajua wazi nasib ameshakua maarufu na anatumia jina lake hakuna ambaye angeweza kumzuia... Mama nasib alivumilia sababu ya mwanae lakini anavyodai alikua akimwambia "wewe ulikataa majukumu....mtoto ungemtunza angekua wako..." Ila mzee Abdul aliendelea kukomaa na medias hadi yakatokea yaliyotokea.

Maskini hakujua wanawake wakibadilika wanabadilika jumla, hawajali aibu wala fedheha! Sasa mzee Abdul ataingia kwenye phase2 ya aibu kama DNA itafanyika japo yeye mwenyewe ameshagomea DNA kwa madai kwamba mtoto hagombewi!

Wanaume wanawake ni watu wazuri na wapole sana ila mnapoishi msiishie kuishi kama marafiki tuu. Waongozeni wanawake zenu kwenye imani, mila na desturi ili heshma na upendo viwe nguzo ya familia.
Binadamu sisi tuko kama tulivyo, jitahidini kuishi na sisi mkiwa wanaume maobeba majukumu yenu na mamlaka ndani ya mahusiano, familia na jamii. Mkilegea ndio tunaishia kutengeneza familia ambazo majukumu ya familia anabeba mama halafu akishayabeba yote anachukua na maamuzi nyumba inakua shubiri.


Salim Nyange RIP na mwanae Nasib Salim Nyange
View attachment 1679951
Nyage Airlines
 
Back
Top Bottom