Mwanaume usikwepe majukumu yako kwa mpenzi wako umpendaye

Mwanaume usikwepe majukumu yako kwa mpenzi wako umpendaye

kiukweli hili swala la kumpa mwanamke pesa ni kama kwangu halipingiki nawaza demu mkali kama uyu nikisipo mpa hela mimi nani ampe sasa
 
Hapana hii ni kubebeshana majukumu yasiyotuhusu kabisa, karne hii ya 50% kwa 50% kila mtu ajitunze mwenyewe, yaani mpenzi tu uhangaike hivyo kah!
Katika ulimwengu huu wa 50/50 ambao mwanamke kapewa uhuru na access zote za kutafuta hela na kumiliki mali huwa sielewi kabisa mantiki ya mwanamke huyu kutaka kuhudumiwa.
 
Bila shaka wewe unaonekaa 50/50 imekukaa akilini
Sio kweli 50/50 ni kitu ambayo iko wazi haiwezekani,hii ikifuatwa mwanamke atakuwa na mengi ya kupoteza
Kilichonikaa akilini ni kusaidiana...sio majukumu fulani ni LAZIMA yafanywe na fulani
 
Mpenzi
Mchumba

Hao hawapaswi gharamikiwa

Mke
Mama watoto

Hawa pekee ndo wanapaswa gharamikiwa
 
Mwanaume kamati hii...

Ikiwa mpenzi wako ni mzigo kwako, basi haumpendi.

Na ikiwa unampenda, lipa bili. Mtoe out kwa chakula cha jioni angalau mara moja kwa wiki.

Mnunulie losheni, manukato, vipodozi na mavazi mazuri apendeze,mtafutie usafiri mjengee nyumba na umtunze maisha yake yote.

Jifunze kwa mwamba Yakobo..
Huyu mwamba alifanya kazi kwa miaka 14 ili kumpata mrembo Raheli. Na kisha akamfanyia kazi Raheli kwa kumtunza maisha yake yote.

Acha kukwepa majukumu yako man

Umasikini tabu sana.

Mfumodume mnauendekeza wenyewe, halafu wanawake wakimilikiwa kama ng'ombe mtalalamika?

Umemfanya mwanamke awe ni mtu wa kuhudumiwa kama mtoto, kama kilema, kama mtu asiye na akili.
 
Sio kweli 50/50 ni kitu ambayo iko wazi haiwezekani,hii ikifuatwa mwanamke atakuwa na mengi ya kupoteza
Kilichonikaa akilini ni kusaidiana...sio majukumu fulani ni LAZIMA yafanywe na fulani
Haki sawa kwa uhalisia haikuwa kwenye majukumu bali kwenye Elimu na vitu vingine kwamba mtoto wa kike asiachwe nyuma.

Tatizo ni sisi tuliichukulia tofauti.

Ili jamii yetu iendelee lazima tuwekeze katika kuwapa watu kazi kulingana na uwezo bila kuangalia jinsia
 
Mungu mwenyewe alisema kuwa Mwanamke atatawaliwa na mwanaume na tamaa ya mwanaume itakuwa juu yake
 
Sio kweli 50/50 ni kitu ambayo iko wazi haiwezekani,hii ikifuatwa mwanamke atakuwa na mengi ya kupoteza
Kilichonikaa akilini ni kusaidiana...sio majukumu fulani ni LAZIMA yafanywe na fulani
Ila hii agenda mnaipush nyinyi na NGO zinawasaidia sana kupush kila siku, ila sasa kuiweka kwenye reality na kuiishi ndipo mnaposhindwa.

Mimi mwanamke akishaanza kuongea 50/50 na kuishupalia na muonea huruma,kwani najua tayari ameshapotea mazima.
 
Back
Top Bottom