Mwanaume usipande gari ambalo nauli yake haumudu from Day 1 >the end

Mwanaume usipande gari ambalo nauli yake haumudu from Day 1 >the end

BIOTOXINS

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2026
Posts
1,091
Reaction score
2,283
Haya makosa wanaume walio wengi wanayafanya pasipokujua mlipuko wake upo,na lazima ulipuke
1. Epuka "Fake Life" (Maisha ya Sifa)
Wanaume wengi wanapoanza mahusiano, ili kumvutia mwanamke, hujifanya wana uwezo mkubwa wa kifedha kuliko uhalisia wao. Wanatoka nao kwenye hoteli za gharama kubwa na kuwapa zawadi nono. Mwanamke anapoingia mzima mzima akiamini hilo ndilo gari lake, mwanaume anaanza kuchoka na kushindwa kuendeleza hiyo "nauli." Matokeo yake ni migogoro, dharau, na hata ukatili pale mwanaume anapoona haheshimiwi tena.
2. Chagua Mtu Anayeendana na Kipato Chako
Kila mwanamke ana viwango na gharama zake za maisha (maintenance fee). Kama wewe ni mtu wa maisha ya kawaida (kama kusafiri kwa daladala au kula mamantilie), usilazimishe kuwa na mwanamke ambaye standard yake ni Uber na migahawa ya hadhi ya juu, isipokuwa kama yeye mwenyewe yuko tayari kushuka na kuishi maisha yako. Ukilazimia, utafilisika au utaishia kuishi kwa msongo wa mawazo.
3. Amani ya Akili (Peace of Mind)
Mwanaume anayeishi kwa uhalisia wake tangu siku ya kwanza huwa na amani sana. Mwanamke anayekubali kuanza na wewe akijua kabisa uwezo wako, hawezi kukupa presha ya kifedha isiyo ya lazima. Mahusiano hayo yanajengwa kwenye misingi imara ya upendo na urafiki badala ya misingi ya kibiashara na maslahi.
Kimsingi,

3.Umemkuta mwanamke anasuka ,anaweka kope ,wanja nk
Unamwambia sasa mke wangu tubane MATUMIZI .ohooo my friend atakubali lakin ndani ya nafsi yake hajakubari

Narudia panda gari unaloweza kumudu nauri,Kila mwanamke na daraja lake

*Usipande tren ya sgr kama nauli Yako ni ya treni ya dar to kigoma
*Usipande ndege kama nauri Yako ni ya bas mwisho wa safari ni mbaya sana
 
Ushauri murua, mwenye macho asome na azingatie

Madini tupu, kongole kwa mtoa mada
 
Back
Top Bottom