matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 9,514
- 23,523
Mazungumzo ya wachungaji, mashehe, wanasiasa ni kana kwamba mwanaume kukoswa pesa ni jambo la kujitakia na uzembe.
Mtu wa namna hii hupuuzwa na kushambuliwa kama ni mvivu hata kama ni kipindi cha mpito anapitia.
Hii tabia inawaweka wanaume wenye changamoto za kiuchumi katika hali ngumu sana.
Ni wakati jamii izungumze kwa kitoa suluhisho sio lawama. Mfano mwalimu wa serikali mwanaume anaishi DSM analipwa kama 500K. Anafamilia, anamichango, anabills bado hajapata mradi anaanza kushambuliwa kwa kosa la uvivu na kutojituma. Wakati huo kuna mtu anafamilia kubwa na watoto wanamtegemea na wazazi wake lakini kazi kafukuzwa, biashara imefeli huyu wakati anajitafuta hakuna kundi lolote katika jamii linamuunga mkono.
Anashambuliwa na watu wa ndani, nyumbani kwake, mkewe, wazazi, wakwe, kanisani, wanasiasa, kila kona kama spiral wa kona.
Jamii iache ulimbukeni wa mafanikio, pamoja na kuhamasisha kazi na kujituma isiwasahau wanaume waliokwama sio kwa hiyari yao ila na wao watakuja tu Mungu akiwafungulia njia katika kujitafuta kwao.
Ni hayo tu.