Judithkaunda
Member
- Aug 21, 2022
- 90
- 231
Habari wana JF,
Ni asili ya mwanaume kuanzisha mahusiano na mwanamke ndio mwenye maamuzi ya kukubali au kukataa, hata kama mwanamke ataanza kumpenda mwanaume ni vema kusubili mwanaume aanze kwasababu yeye ndiyo dereva anatakiwa kuwa na uhakika wa safari yenu na ramani ya huko mnakoelekea.
Mwanamke anapoamua kuingia kwenye ndoa anaingia na mtazamo huu kichwani kwake.
Tunajua nyinyi wanaume mnajua kila kitu kuhusu maisha, mnajua tunachotakiwa kufanya, mnajua tunakotakiwa kufika kama familia.
Kwasababu hatukuwahi kuona mnafundwa wala kupelekwa kwa somo kabla ya ndoa. Wakati najifunza kuishi na mtu tofauti na familia yangu kw aukaribu nategemea pale ninapokosea unifundishe na kunielekeza kwasababu tunaamini mwanaume anamajibu ya maswali yote.
Sasa shida inakuja pale mwanaume anapoingia kwenye majukumu hayo wakati hajui kitu, ni mbaya sana mwanamke akigundua wewe hujui chochote.
Mwanaume hakikisha una maono na unasimama kwenye nafasi yako kama dereva mwenye ramani ya kule mnakotakiwa kufika, usiyumbishwe na kelele za konda ni kawaida yetu kupiga kelele.
Lakini kama mwanamke akigundua hata wewe hujui mnakotakiwa kwenda ataanza kukuelekeza kwasababu wanawake hatukubali kuingizwa chaka, na hapo ndipo wanawake tunakosea kwasababu tunahitaji hekima zaidi kukuelekeza hadi mtuelewe.
Ni kweli mapenzi hayana mwenyewe unaweza kumpenda yoyote umtakae, lakini kati ya mahusiano yenye wakati mgumu zaidi ni yale ambayo mwanamke kamzidi umri mwanaume, kwasababu ni asili ya mwanaume kuwa kiongozi haijalishi mwanamke anawezo kiasi gani.
Kama mwanamke atakuzidi sana umri safari yenu itakuwa ngumu sana kwasababu yeye atakuwa tayari anapajua zaidi huko mnakokwenda na lazima umsikilize mwenyeji, na hapo utatumia nguvu nyingi kuonyesha uanaume wako.
Mwanaume simama kwenye nafasi yako, wewe ni mwamba.