Mwandishi Ansbert Ngurumo apewa hifadhi kwa usalama wake nchini Finland

Mwandishi Ansbert Ngurumo apewa hifadhi kwa usalama wake nchini Finland

Ngurumo, acha propaganda za kudanganya watu kwamba umepewa ukimbizi nchini Ufini, hii siyo kweli, ulichofanya kama ni kweli ni kwamba ombi lako la ukimbizi limechukuliwa na linafanyiwa kazi na baada ya kujiridhisha kwamba ni kweli unastahili kupata Ukimbizi nchini Ufini kulingana na vigezo vyao ndiyo utapewa kibali cha kuwa Mkimbizi!

Ulichokifanya ni kuomba kuwa mkimbizi jambo ambalo kila raia wa Dunia hii anaweza kulifanya, lakini kukubaliwa ukimbizi ni jambo lingine kabisa, acha kudanganya watu, umetuma maombi lakini haujakubaliwa kupewa ukimbizi na maombi yako yatakataliwa lakini usisahau kutupa mrejesho hapa maombi yako yakikataliwa, kwani hauna sababu za kupewa Ukimbizi nchini ufini hivyo majibu yako nina uhakika kwa 90% yatakuwa negative, lkn kuomba hifadhi kila mtu anaweza kufanya hata members wote wa JF, Mayala, Mbowe, Zito, Mangi Kimambi &Co. wanaweza kuomba, lakini kama watakubaliwa ni swala lingine kabisa, ...

mmechukia kwasababu mmeshindwa kumtesa na kumuua.
 
Tatizo lenu mmekabidhi akili kwenye kopo tupu. Kuna tofauti ya kupewa ukimbizi na kupewa ulinzi ili usidhulike.

Kama zinawatosha ebu fikirieni haya

1. Mnakusudia kutengeneza wakimbizi?
2.Je ni kweli ametishiwa maisha?
3. Je ni kweli yuko Finland?
4. Udhaifu wenu ni wa kiwango gani hadi amewaponyoka?

Maana ya haya yote wewe na genge lako na uchwara wenu ni mambumbumbu kweli kweli. Kila kitu mnafeli hadi mtu unafikiri hii laana ya awamu ya tano tumekosea nini hadi tuadhibiwe hivi? Mlichofaulu ni kuonyesha sura TBC na kushinda kwenye kutoa maelezo.
 
Definition ya ukimbizi inaeleweka vizuri au...tunaandika tu ukimbizi.
Still Tanzania is the best place to live ever seen
Mwambie baba yako asimame jukwaani na kumkosoa Magu uone baada ya wiki kama hukuweka turubai na kulala matanga nyumbani kwako
 
Mwambie baba yako asimame jukwaani na kumkosoa Magu uone baada ya wiki kama hukuweka turubai na kulala matanga nyumbani kwako
mgoloko, KWA SABABU NYINYI KWA HILA NA UFINITIVU MTAFUTA NA KUMUUA ILI ALIYETUKANWA AONEKANE NDIYE KAUA
 
Ni habari mbaya kwa nchi yetu inaendelea kuwa na hadhi mbaya ndani /nje ya mipaka yake. Maisha ya waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati yamekuwa ya mashaka.

Mwanahabari Ansbert Ngurumo aliyewahi kuwa mhariri wa Magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, amekimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi huko, kwa muda alikuwa akisema anatishiwa kuuawa.

Habari zaidi soma=> Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo

UPDATE:

Mwandishi wa Habari mwandamizi nchini, Ansbert Ngurumo amepata hadhi ya kupewa ulinzi nchini Finland, baada ya kudai amekimbia aliowaita "wauaji" wake.

Ngurumo ambaye amewahi kuwa mhariri wa magazeti kadhaa nchini; Mtanzania, Tanzania Daima na MwanaHalisi, ameiambia JamiiForums kuwa amekiepuka kifo kilichopangwa na wale aliowaita "wasiojulikana."

Akizungumza na JamiiForums, Ngurumo alisema ni kweli amekimbia Tanzania ili kuulinda uhai wake baada ya kuanza kuwindwa na watu wasiojulikana.

"Tangu mwaka jana nimekuwa nikipokea vitisho vingi na vyenye kuogofya kufuatia makala zangu kwenye gazeti la MwanaHalisi. Nimenusurika kuuawa mara kadhaa, lakini nashukuru Mungu hadi leo niko hai," anasema Ngurumo.

Anasema ili kunusuru uhai wake, alilazimika kujificha Mwanza tangu mwaka jana na baadaye kupata kwenda Kenya, kabla ya kwenda Sweden na sasa Finland, ambako amepewa hifadhi.

Ngurumo anasema hadhi aliyopewa Finland, siyo ya ukimbizini, bali ni "hifadhi ya kimataifa," kuunusuru uhai wa mtu ambaye yuko katika hatari ya kuuawa nchini mwake.

Vyombo vya Habari vya Finland na mitandao ya kijamii, imeandika habari ya Ngurumo kukimbia Tanzania kwa hofu ya kuuawa.

"Nimezungumzia mkasa wangu wa kunusurika kudakwa na watu wasiojulikana, ambao wamekuwa wakipanga kuniua na wamejaribu mara kadhaa bila mafanikio, sasa nikaona niwakimbie, kwani kufa kijinga ni dhambi kubwa," anaongeza Ngurumo.

JamiiForums inatambua kuwa Ngurumo alianza kuhofia maisha yake baada ya kudai kupokea vitisho kwa alichodai ni kufuatia kuandika makala kwenye gazeti la MwanaHalisi ikiwa na kichwa cha habari; “Tumuombee Rais Magufuli au Tundu Lissu?”
Hiki kiingereza ni Ansbert kweli?
 
Songs by Ansbert Mugamba Ngurumo

Pamoja na uandishi wa Habari Ngurumo pia ni mtunzi na mwanamuziki wa nyimbo katoliki
Kwaya karibu zote siku ya mkesha wa Pasaka lazima ziimbe wimbo wake wa Mwanga wa Kristu, pia ibada nyingi za upadrisho wimbo wake wa mimi ni nani hata umenileta nikutumikie lazima uimbwe,
 
Ni habari mbaya kwa nchi yetu inaendelea kuwa na hadhi mbaya ndani /nje ya mipaka yake. Maisha ya waandishi wa habari, wanasiasa na wanaharakati yamekuwa ya mashaka.

Mwanahabari Ansbert Ngurumo aliyewahi kuwa mhariri wa Magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi, amekimbilia nchini Finland na kupewa hifadhi huko, kwa muda alikuwa akisema anatishiwa kuuawa.

Habari zaidi soma=> Ansbert Ngurumo: Muda wowote naweza kufa maana natishiwa kifo

UPDATE:

Mwandishi wa Habari mwandamizi nchini, Ansbert Ngurumo amepata hadhi ya kupewa ulinzi nchini Finland, baada ya kudai amekimbia aliowaita "wauaji" wake.

Ngurumo ambaye amewahi kuwa mhariri wa magazeti kadhaa nchini; Mtanzania, Tanzania Daima na MwanaHalisi, ameiambia JamiiForums kuwa amekiepuka kifo kilichopangwa na wale aliowaita "wasiojulikana."

Akizungumza na JamiiForums, Ngurumo alisema ni kweli amekimbia Tanzania ili kuulinda uhai wake baada ya kuanza kuwindwa na watu wasiojulikana.

"Tangu mwaka jana nimekuwa nikipokea vitisho vingi na vyenye kuogofya kufuatia makala zangu kwenye gazeti la MwanaHalisi. Nimenusurika kuuawa mara kadhaa, lakini nashukuru Mungu hadi leo niko hai," anasema Ngurumo.

Anasema ili kunusuru uhai wake, alilazimika kujificha Mwanza tangu mwaka jana na baadaye kupata kwenda Kenya, kabla ya kwenda Sweden na sasa Finland, ambako amepewa hifadhi.

Ngurumo anasema hadhi aliyopewa Finland, siyo ya ukimbizini, bali ni "hifadhi ya kimataifa," kuunusuru uhai wa mtu ambaye yuko katika hatari ya kuuawa nchini mwake.

Vyombo vya Habari vya Finland na mitandao ya kijamii, imeandika habari ya Ngurumo kukimbia Tanzania kwa hofu ya kuuawa.

"Nimezungumzia mkasa wangu wa kunusurika kudakwa na watu wasiojulikana, ambao wamekuwa wakipanga kuniua na wamejaribu mara kadhaa bila mafanikio, sasa nikaona niwakimbie, kwani kufa kijinga ni dhambi kubwa," anaongeza Ngurumo.

JamiiForums inatambua kuwa Ngurumo alianza kuhofia maisha yake baada ya kudai kupokea vitisho kwa alichodai ni kufuatia kuandika makala kwenye gazeti la MwanaHalisi ikiwa na kichwa cha habari; “Tumuombee Rais Magufuli au Tundu Lissu?”
Abaki hukohuko,akichoka kama alivyochoka Kambona aje tumzike
 
Miaka ya tisini kuna mshkaji alirudishwa kutoka Sweden.Ni miongoni mwa watu waliozamia kuondoka Tanzania kwa gia ya ukimbizi Zanzibar.

Alivyorudi akawa kaja maskani. Kuna mtu akawa anamsifia Nyerere. Jamaa akamponda sana Nyerere.

Akasema Nyerere ni sababu yeye karudishwa Tanzania.

Mshkaji anasema alipokuwa Sweden alikuwa anapeta kama mkimbizi, siku moja Nyerere akatembelea Sweden katika kazi zake za kimataifa baada ya urais. Watu wakamuuliza, Mwalimu Nyerere Tanzania inaelekea wapi siku hizi, mnatoahata wakimbizi wa kisiasa wanakuja kuomba hifadhi huku? Kulikoni?

Nyerere akasema wako wapi wakimbizi hao? Natakakuongea nao.

Akaambiwa tulia, tutakupeleka.

Akapelekwa mpaka kwenye mkutano na hao wakimbizi.

Nyerere akaanza kuwaluliza mmoja mmoja, wewe umetoka wapi. Kila mmoja anataja alipotoka.Ingawa walijikokikama Wazanzibari, wengi walikuwa watoto wa Dar.

Ilipofika zamuya mshkaji akaulizwa, akasema anatoka Faya. Nyerere akamhamakia "Faya hapa Mwembetogwa hapa? Kuna vurugu gani ya kukufanya uwe mkimbizi?". Nyerere alitumia jina la zamani la Faya "Mwembetogwa", kuonesha kwamba anapajua hapo kipindi kirefu tangu anaishi Magomeni.

Basi akawaambia wale wa Swidi, hapa hamna mkimbizi wa kisiasa,hawa vijana wote wanatafuta maisha wametoka Dar es salaam ambapo hakuna matatizo.

Siku chache baada ya hapo wakapandishwa ndege wakatupwa Bongo.

Jamaa tangu sikuhiyo hataki kumsikia Nyerere.

Nasikiyika kwa nchi yetu ilipo leo, watu wanaweza kujenga case credible ya kutafuta na kupata ukimbizi.
Hivi mkuu, kama mtu akipatiwa nafasi hiyo gharama za maisha ya Nchi anakopewa hifadhi hugharamiwa na Nchi husika?

Au hujigharamia mwenyeweee?
 
Watanzania wamefikia sasa hatua hata ya kukimbia nchi yao wenyewe.

Watanzania hawa wasio na hatia inawezekana kosa lao kubwa ni kupenda kwao haki na kuonesha kuidai hiyo haki bila kubaki kimya kumewaponza.

Ndiyo, kudai haki ni kosa mbele ya wasopenda haki, kudai haki ni kosa kwa watawala wenye fikra finyu zilizokosa utu, kwao chuki na ubinafsi ndiyo msingi wao mkuu na mara nyingi wanafurahi kuona raia wanateseka kwa shida na taabu wanazosababisha wao.
Watawala hawa[siyo viongozi hawana sifa ya kuitwa viongozi] wakiona unadai haki yako waliyoipoka wanakueka katika 'blacklist' ya the next target.

Ndiyo mana wenzetu hawa mwandishi Ngurumo na wengine walijaribu kuishi kwa kujificha huko Tanzania bila mafanikio wakaona salama yao ni kutafuta hifadhi ughaibuni.

Hii ya kukimbia nchi na kuomba hifadhi[asylum seeker] tulizoea kuiskia tu na kuona kwa majirani zetu wa Uganda na Rwanda huko siyo Tanzania sababu haijawahi kutokea hivi karibuni.

Kweli ni aibu kubwa sana kwa nchi ambapo watawala wanajinasibu kuna amani, amani gani mnazungumzia watu wanakimbia nchi?
Hakika hii ni laana kwa wote wanaosababisha haya yatokee.

Wengine tulijaribu kutahadharisha kabla sababu tulishaona.

Mie hapo awali tarehe 25 september 2017 siku ya jumatatu mida ya asubuhi hivi niliandika hapahapa mada nikipa title ya "Watanzania kuanza kukimbilia uhamishoni." nia yangu ya heri tu ilikuwa kutahadharisha na kufikisha ujumbe kwa watawala ili wajirekebishe kama wanahekima na busara na wanamuogopa Mungu kama wanavyojinadi kila kukicha tuwaombee.

Niliskitika sana mada hiyo ilikumbana na misukosuko mikali yenye nia ovu hapa Jamiiforums hatimaye ikafutiliwa mbali.

Kwa kuwa sikuvunja sheria za hii forum na tena sikuvunja sheria hata moja ya nchi ya Tanzania sikufahamu sababu ya kuifuta mada hiyo muhimu kwa ustawi wa Jamiiforums, members wote wa forum hii ndani na nje ya nchi na watanzania wote kwa ujumla hasa wapenda haki.

Ile mada nikairudisha tena na tena nikiomba wakuu- authority ya jamiiforum wailinde mada yangu au kama nimevunja sheria waniambie watende haki hawakufanya hivyo zaidi tu ya kufuta ile mada.

Leo yanatokea yale niloeleza kwenye mada ilofutwa ambapo kama ingeachwa online nani ajuaye ingesaidia.
Member kama Alwatan nakumbuka na wengine walipinga sana mada kufutwa sababu walibahatika kuisoma na haikuwa na shida hata ya kuzuiwa.

Nimalize kwa kuleza wakati huu ambapo media nyingi ziko kimya kwa uoga, salama yetu ni kujaribu kuwa wamoja huku kwenye mitandao na tupende haki.

Kudumu kwa forums kama hii ni umakini na nia ya wamiliki wa forum katika kusimamia sheria za forum zisivunje sheria za nchi na kujali haki pasi na hivyo haiezi kufika mbali hata watawala wanaeza kuifunga tu hakutakuwa tena na moral authority yeyote ya kuwapinga hao kama wenyewe tu hatutendeani haki sisi kwa sisi.

Leo ukiona hayakupati wewe hujui kesho yatakufika nani atasimama upande wako sababu hukusimama kwangu au ulisimama na wadharimu wanuka damu za watu ukijua uko salama unajidanganya, amka wewe.
 
I dared to criticise President Magufuli and nearly paid the ultimate price.
tanzania-ansbert-ngurumo.jpg

Ansbert Ngurumo (left) reads one of the newspapers he previously edited. Credit: John Dande.

When I chose to go into journalism over 20 years ago, I never anticipated the friends I would come to make. I never foresaw that two decades down the line, my whole fate would rely on allies far from home who I had never met.

I also never realised the enemies I would make. Little did I know that powerful opponents of journalistic truth would end up chasing me from my homeland of Tanzania. Yet that is what happened to me after writing articles that dared to criticise President John Magufuli.

I first knew I was on the president’s radar in early-2016 when a friend of mine was sent to advise me against criticising the then new leader. At the time, I did not take the message too seriously. I had received similar warnings for over ten years under the Magufuli’s predecessors Benjamin Mkapa and Jakaya Kikwete.

But I realised I was in real danger on 2 October 2017 when some good Samaritans alerted me of a plot to kill me. I was fortunate that, in my fear and uncertainty, I could immediately call on friends for help.

They quickly transferred me from Mwanza to Dar es Salaam where I sought the aid of a local human rights group. As my pursuers tracked me, this organisation kept relocating me, putting me up in four different hotels over the next two weeks.

But that was not enough to keep me out of harm’s way. At the fourth hotel, the manager notified me one night that “some government people” had been asking about me. He warned me that two of them, who claimed to be police officers, had booked rooms.

Terrified and smelling death, I fled that very moment. I called a friend who arrived within 15 minutes. I got into his car and we sped off with no destination in mind. As we drove, I phoned another contact within an opposition party who thankfully found me a secret residency where I could seek sanctuary. There, I seemed to be safe, and that is where I was two weeks later when an international press organisation came to help me leave the country.

That meant that by 21 November, when Azory Gwanda, a reporter with Mwananchi newspaper, was abducted in chilling circumstances, I was already safely relocated in Nairobi. Gwanda, who had also published critical reports of the government, was probably seized by the same individuals that had targeted me. His whereabouts are still unknown and the government remains silent.

Thinking of Gwanda’s fate makes me even more grateful to the friends in Tanzania and from as far as Kenya, Finland, Denmark, Sweden and the US who saved my life.

Magufuli tightens the noose
Since then, I have been able to flee even further afield, while the situation in Tanzania has only deteriorated.

President Magufuli, who came to power in 2015, is ruling by decree and only follows the constitution when it serves his impulses. Tanzania’s democratic gains from 25 years of multiparty politics are fast diminishing.

In just the last few months, two opposition leaders have been killed, while two more have been sentenced to jail for “insulting” the president. Other critics have been intimidated or attacked, while a university student was accidentally shot dead by police when they opened fire at an opposition demonstration.

In a short time, Magufuli has managed to tighten the noose around the neck of civil society, the opposition, artists, and the media. He has used regressive legislation such as The Cybercrime Act, Statistics Act, Media Services Act and more to suffocate freedom of expression and silence dissent.

His government has shut down at least five critical newspapers since he came to office. Meanwhile, journalists have been arrested on questionable charges, intimidated or – in Gwanda’s case and very almost mine – faced much worse.

Even posting criticism on social media has become a risky endeavour. Several Tanzanian citizens have been charged with cybercrimes for criticising Magufuli online, and at least two have been convicted. Bob Wangwe, a human rights defender, was sentenced to 18 months imprisonment or a fine of five million shillings ($2,200). Issac Abakuki was handed down three years in prison or a fine of seven million shillings ($3,000).

In Tanzania today, independent journalism is fast withering, while dissenting opinions are openly discouraged and ruthlessly punished.

Tanzania pushes back
Fortunately, there are some brave groups in Tanzania pushing back against these worrying trends.

The Legal and Human Rights Centre (LHRC) and Media Council of Tanzania (MCT), for example, intend to demand a court interpretation of the term “sedition” as part of a challenge to the assault on freedoms of expression. Meanwhile, another group of activists is seeking legal redress against what they see as the unconstitutional ban on political gatherings.

Furthermore, in a rare show of collective alarm last month, a wide host of religious, student and civil society groups issued statements. In these strongly-worded releases, they expressed their concerns at rising levels of political violence and called on the government to prevent them.

In many of these efforts, domestic groups have sought support from international partners. They are becoming more increasingly unsettled too. According to sources in the European Union, Tanzania’s positive reputation changed drastically in September 2017 when senior opposition lawmaker Tundu Lissu narrowly survived a brazen assassination attempt. In February, the EU also released a statement voicing concerns over recent threats “to democratic values and the rights of Tanzanians”.

Domestic and international partners must now join hands. Together, the Tanzania people and their allies must make it clear that they are not willing to give up their freedoms. They must pressure the government to change repressive laws and abide by the constitution.

In these troubling times for my now distant homeland of Tanzania, sustained and joint action is the only way to stop more journalists succumbing to my fate or, much worse, that of Azory Gwanda.

Source: I had to flee my home Tanzania for doing journalism. I was lucky. - African Arguments
 
Back
Top Bottom