Uchaguzi 2020 Mwandishi John Marwa wa Dar24 akamatwa kwa kumkashifu Naibu Waziri Mwita Waitara

Uchaguzi 2020 Mwandishi John Marwa wa Dar24 akamatwa kwa kumkashifu Naibu Waziri Mwita Waitara

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Mwandishi John Marwa akamatwa na kunyimwa dhamana ya polisi kwa kumchafua naibu waziri Mwita Waitara

- Ni katika malumbano ya kisiasa katika kundi la whatsapp la jambo Tarime

- *Mpelelezi wake adai hawezi kumpa dhamana hadi amkamate mshitakiwa mwenzake ajulikanae kwa jina la David Gichogo
1591797417192.png

John Marwa ambaye ni mwandishi wa habari ameshikiliwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kilichopo Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni uliopo katika Jiji la Dar es Salaam kwa tuhuma za kumchafua Mbunge wa Jimbo la Ukonga na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Mwita Mwikwabe Waitara katika malumbano ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hususani katika Jimbo la Tarime Vijijini.

Malumbano hayo yaliyofanyika katika kundi la WhatsApp lijulikanalo kama Jambo Tarime lilipelekea Naibu Waziri Mwita Waitara kuwafungulia mashitaka Mtuhumiwa John Marwa na David Gichogo kwa makosa ya kumchafua kimtandao.

Juhudi za kumuwekea dhamana zimeshindikana baada ya mpelelezi wake kudai hawezi kumpa John Marwa dhamana hadi hapo atakapofanikiwa kumkamata David Gichogo ambaye bado hajapatikana, jambo ambalo sio sahihi kisheria.

Kando ya uandishi wa HABARI, John Marwa pia ni mwanachama wa ACT-Wazalendo hivyo huenda mabishano yalitokana na minyukano ya kisiasa kwa sababu wanatoka katika vyama tofauti vya kisasa.

Juhudi zinaendelea kufanyika kupitia kwa wakili wa John Marwa na kwa viongozi wa Jeshi la Polisi ili kuhakikisha haki ya dhamana inapatikana kwa John Marwa maana makosa anayotuhumiwa nayo yana dhaminika.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusu jambo hilo kadri linavyoendelea ila kwa sasa juhudi za kumuwekea dhamana bado zinaendelea kupitia Wakili wake.
 
Hivi kama mtu hataki kuchafuliwa kuandikwa au kuongelewa popote kuna sheria inayomlinda au kuna sheria inayotaka jamii na vyombo vya habari kumsema mtu?
 
Back
Top Bottom