Ukitaja majina ya Waandishi 10 mahiri wa vitabu nchini basi jina la Edwin Semzaba halikosekani.
Huyu alikuwa Mwanamasumbwi, Muigizaji Mwandishi na Mhadhili wa Chuo kikuu cha UDSM.
Moja ya kazi zake zilizompatia umaarufu ndani na nje ya Tanzania ni kitabu cha "Ngoswe penzi kitovu cha Uzembe"
Kikiwa ni kitabu kilichodumu kwa muda wa miaka 20 kikitumika kama kitabu cha kiada kwa shule za Sekondari.."Kitabu cha Ngoswe nilikiandika nikiwa kidato cha pili wakati huo nikiwa na miaka 16 tu tena ilikuwa sababu ya kukimbia somo la Hesabu hivyo wakati najificha nilitumia muda huo kuandika na hii ilikuwa mwaka 1967 wakati wa sensa ya kwanza kabisa ya watu na makazi kufanyika nchini. Enzi hizo mwanafunzi wa Livingstone College na sasa Kigoma sekondari"..Anasema Edwin Semzaba.
Vitabu vingine alivyowshi kuviandika ni pamoja na;
Tendehogo 1982
Sofia wa Gongo la mboto 1985
Mkokoteni 1988
Tausi wa Alfajiri 1996
Funke buge buge 1999
Tamaa ya boimanda 2002
Marimba ya Majaliwa 2008
Rest in piece Edwin Semzaba Daima tutakukumbuka hasa kwa kazi zako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.