TANZIA Mwandishi nguli wa Fasihi nchini, Edwin Semzaba afariki dunia

TANZIA Mwandishi nguli wa Fasihi nchini, Edwin Semzaba afariki dunia

Pumzika kwa amani mzee wetu. Umetangulia nasi tutafuata kila mtu kwa wakati alopangiwa na Muumba.
 
1453062122863.jpg

Mwandishi nguli wa riwaya na tamthilia duniani, Edwin Semzaba almaarufu kama Ngoswe (Jina la tamthilia aliyoiandika alipokuwa kidato cha pili) ameaga dunia leo.

Mbali ya kuwa mwandishi, amefundisha katika Idara ya Sanaa chuo kikuu cha Dar es Salaam (Department of Fine and Performing Arts kipindi hicho).

Ndugu Semzaba ameandika riwaya na tamthilia nyingi kama Ngoswe, mkokoteni, Joseph & Josephine (hakijatoka bado) Marimba, Gongo la mboto just to mention a few.

What a loss.
Edwin Semzaba is a legend.
May his soul rest in eternal peace. Amen.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.

Mwanafunzi wako kipenzi: Unko T
 
Pumzika kwa amani Semzaba..Kazi yako itaendelea kuishi vizazi na vizazi
 
Yule mwandishi nguli wa Fasihi Tanzania, Edwin Semzaba afariki dunia (RIP).

Kwa wale wana Fasihi na wana UDSM & Tanzania kwa ujumla tumepatwa na msiba mkubwa sana leo.

Edwin Semzaba ni mwandishi wa kitabu maarufu cha Ngoswe - Penzi kitovu cha uzembe.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la bwana lihimidiwe!!
Bwana ametoa, Bwana ametwaa; Upumzike kwa Amani Babu Edwin Semzaba.
 
nakosa cha kusema hasa nikikumbuka ucheshi wake...rafiki,mtunzi,mwalimu na gwiji la uandishi....taswira hazinishi!poleni FPA,poleni TATAKI
 
1997 nilibahatika kufundishwa na yeye kitabu chake NGOSWE raha ilioje daah
 
Kwa wale Wana fasihi NA WANA UDSM TUMEPATWA NA MSIBA MKUBWA SANA LEO

EDWIN SEMZABA mwandishi wa kitabu maarufu cha Ngoswe penzi kitovu cha uzembe. Amefariki dunia leo.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la bwana lihimidiwe
Cc Kipilipili Creative Writing 256-257
Ntakukumbuka sana Mwalim wangu,ulinijenga kuwa hivi nilivyo.
Kazi za Semzaba nilizowahi kupata kuzisoma
1.Sofia wa Gongo la Mboto
2.Marimba ya Majaliwa-Hii riwayahutaiweka chini ukiishika,ukiwa unaisoma unajikuta unaizunguka Tanzania bara na visiwan ukiwa umeshika kitabu
3.Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe-Tamthiliya Iliyompa umaarufu sana,na inasomwa mpaka leo,na alipata kusema anaandaa Ngoswe part II,
Wadau wa Fasihi wamepata msiba usio na maelezo
BABU NGOSWE,,,
 
nakosa cha kusema hasa nikikumbuka ucheshi wake...rafiki,mtunzi,mwalimu na gwiji la uandishi....taswira hazinishi!poleni FPA,poleni TATAKI
Acha tu babu Ngoswe na ile 'WASIFU WA MPENZI WANGU' wallah sitasahau jinsi nilivyomsifia kipusa wangu mtoto wa Mwananyamala nilokutana nae Tandale,ana rangi ya kichuguu,MIE SISEMI KAKA
 
Back
Top Bottom