Ngoja wewe ndo nikuelezee labda hujui.
Utawala wa kirumi ndio uliwaondoa Wayahudi kutoka Yudea ambayo ndio Yerusalem mwaka 135 CE na kuubadili jina kuuita Palestina. Zingatia mwaka hapo ni muhimu.
Baada ya hapo Warumi walisambaa maeneo mbalimbali ambayo yalikuwa chini ya utawala wa Kirumi ambayo ni Ulaya ya leo.
Umetaja vita ya msalaba ya karne ya 11, hiyo vita wayahudi waliuawa sana na wapigania Kristo kwa madai kuwa wao ndio chanzo cha kifo cha yesu.
Karne ya 14 pia wakauawa sana kwamba wao ndo chanzo cha black deaths.
Na muda wote huo walikuwa Ulaya.
Sasa sujui unaposema vita ya msalaba una maana gani maama wameuawa na crusaders.
Sasa turudi kwenye swali moja. Natives wa america ni red Indiana, kama wazungu wa kwanza kufika america wamefika mwaka 1565, na leo wanaimiliki Amerika wahindi weusi hawadai ardhi yao, iweje watu waliondoka hapo mwaka 135 CE (Yani zamani zaidi) warudi baada ya mamia ya miaka kudai ardhi?
Kila saa ninakuuliza awali dogo, na narudia tena.
Hivi inawezekana Wangoni leo hii warudi Afrika Kusini waende kwenye enewo walilofukuzwa na Shaka Zulu, waseme hili eneo lilikuwa la kwetu, tumerudu kulichukua, na dunia iwaunge mkono kuchukua hilo eneo? Inawezekana kweli?
Kama haiwezekani hilo kwa wengine, ni kwanini iwe tu kwa Jews?