Mwandosya tuliambiwa asiye na Wizara maalum, Mkuchika kazi maalum. Kazi zipi hizo?

Mwandosya tuliambiwa asiye na Wizara maalum, Mkuchika kazi maalum. Kazi zipi hizo?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Ninakumbuka Jk alipounda baraza lake la kipindi cha pili cha uongozi wake, alimteua pro. Mark Mwandosya akatuambia kuwa amemteua kama waziri asiyekuwa na wizara maalum.

Sasa hivi tena ameteuliwa waziri Mkuchika ambaye tunaambiwa kuwa ni waziri kazi maalumu.

Kwa uelewa wangu mambo yote ya uongozi wa nchi hugawanywa chini ya wizara tofautitofauti.

Hapa ndio najiuliza huyu waziri jukumu lake analitekeleza kwa muktadha upi? Au ni namna tu ya kutengenezeana ulaji
 
Ninakumbuka Jk alipounda baraza lake la kipindi cha pili cha uongozi wake, alimteua pro. Mark Mwandosya akatuambia kuwa amemteua kama waziri asiyekuwa na wizara maalum.
Sasa hivi tena ameteuliwa waziri Mkuchika ambaye tunaambiwa kuwa ni waziri kazi maalumu.
Kwa uelewa wangu mambo yote ya uongozi wa nchi hugawanywa chini ya wizara tofautitofauti.
Hapa ndio najiuliza huyu waziri jukumu lake analitekeleza kwa muktadha upi? Au ni namna tu ya kutengenezeana ulaji!
Kila sehemu kuna umaalum, huo umaalum ukitokea ndipo mkuchika utamuona akifanya kazi, Kwahiyo tulia haraka ya nini?
 
Ujanjaujanja Umerudi Tena
Mambo Ni Fire
Tonge La Mwisho Ndiyo Lakukombea Mboga!!!
😆😅😄😃😂😁😀😀😀😄😄😅😅😃😂😂😎
 
Ninakumbuka Jk alipounda baraza lake la kipindi cha pili cha uongozi wake, alimteua pro. Mark Mwandosya akatuambia kuwa amemteua kama waziri asiyekuwa na wizara maalum.
Sasa hivi tena ameteuliwa waziri Mkuchika ambaye tunaambiwa kuwa ni waziri kazi maalumu.
Kwa uelewa wangu mambo yote ya uongozi wa nchi hugawanywa chini ya wizara tofautitofauti.
Hapa ndio najiuliza huyu waziri jukumu lake analitekeleza kwa muktadha upi? Au ni namna tu ya kutengenezeana ulaji!
Pale Ikulu kila siku kunakuwa na waziri wa zamu. Sasa ili kuondoa zamu hizi Rais anaweza kumteua mtu ye yote kufanya kazi za pale Ikulu badala ya kuwa na waziri wa zamu.

Mawaziri hawa huitwa mawaziri wasio na wizara maalum.
 
Ni kupeana ilaji tu kizee kama kile kikae nyumbani kilee wajukuu
 
Ninakumbuka Jk alipounda baraza lake la kipindi cha pili cha uongozi wake, alimteua pro. Mark Mwandosya akatuambia kuwa amemteua kama waziri asiyekuwa na wizara maalum.
Sasa hivi tena ameteuliwa waziri Mkuchika ambaye tunaambiwa kuwa ni waziri kazi maalumu.
Kwa uelewa wangu mambo yote ya uongozi wa nchi hugawanywa chini ya wizara tofautitofauti.
Hapa ndio najiuliza huyu waziri jukumu lake analitekeleza kwa muktadha upi? Au ni namna tu ya kutengenezeana ulaji!
Ukiwa Waziri usiye na Wizara maalum, kimsingi wewe ni msaidizi wa Raisi, kwa hiyo unaweza kupewa assignment inayohusu wizara yeyote ili ukasaidiane na waziri anaehusika. Na pia utakuwa unamwakilisha Raisi katika majukumu mbalimbali pamoja na ziara za ndani na nje, kufungua miradi nk. Kukiwa na ugeni kutoka nje wewe utahudhuria mikutano hiyo na Raisi karibu yote, wakati mawaziri ni wale tu wanaohusika na jambo litakalozunguziwa ndio wanahudhuria

Kwa hiyo ni uteuzi muhimu sana kwa Raisi na anapewa mtu ambaye ana akili ya kutambua na kuelewa mambo kwa haraka kuhusu siasa za ndani na mahusiano na nchi za nje. Unakuwa pia mshauri wa karibu sana wa Raisi katika mambo yanayohusu kila Wizara. Hata raisi akitaka kumtimua waziri mtu wa kwanza kuongea nae atakuwa wewe, kisha Waziri Mkuu ndio ataambiwa. Na una nguvu ya kumshauri Raisi kuwa waziri fulani katika wizara fulani hafai. Kumbuka kwa mfano, Prof. Mwandosya akiwa Waziri asiye na wizara maalum ndie hata alienda Rwanda kutatua mtifuano kati ya Kikwete na Kagame. Alifanya kazi nyingi sana kwa niaba ya Kikwete. Lakini mara nyingi hufanyi hizo kazi kwa uonekano. Unatakiwa kumfanya Raisi ang'are bila wewe kung'ara. Unakuwa busy sana, hivyo lazima uwe mchapakazi wa kweli.

Uwaziri usio na Wizara maalum kimsingi ni kama maandalizi ya kukufanya uwe raisi. Ni sawa na kuwa Raisi Msaidizi na Waziri Mkuu msaidizi asiyetambulika kikatiba, lakini somehow unamzidi hata Waziri Mkuu. Waziri asiye na wizara maalum anawajibika zaidi kwa raisi kuliko kwa Waziri Mkuu. Waziri Mkuu anaweza kuwa na majadiliano na Raisi juu ya jambo fulani, na Raisi akamwambia Waziri Mkuu utamwakilisha Raisi katika hayo majadiliano. Watu vihiyo walikuwa wanabeza uteuzi wa Prof. Mwandosya kwenye hii nafasi, niliwashangaa sana.

Kumbuka pia, ili kumdanganya Mwandosya kwamba atakuwa raisi baada yake, JK alimpa nafasi hii, kumbe ilikuwa ni chenga ya mwili. JK alitambua wazi alihitaji akili za mtu kama Mwandosya kuendesha nchi wakati anaitwa dhaifu nk. Kama uligundua, mwishoni JK alionekana kuwa na busara sana za uongozi - nyuma ya hilo ilikuwa ni akili za Prof. Mwandosya.

Hii ndio nafasi nasubiri mama Samia aniteue!
 
Kapteni George Mkuchika ameteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais ambaye tumetangaziwa kuwa majukumu yake ni maalumu.

Hakuna tatizo lakini ningependa/tungependa watanzania hili likawekwa wazi ni shughuli gani hizo "maalum" atakazokuwa anazifanya huyo MH. Waziri wa kazi maalumu?

Tuna Haki ya kujua/kufahamu kwasababu tunamlipa posho/mshahara na marupurupu mengine kupitia kodi zetu sisi wananchi wa Tanzania.

Isije ikawa ni kupeana nafasi tu za kutafuna fedha zetu kwa minajili ya kusaidiana nyie watawala.

Nahitaji kufahamu majukumu ya Waziri Ofisi ya Rais kazi maalumu .
 
Back
Top Bottom