Ukiwa Waziri usiye na Wizara maalum, kimsingi wewe ni msaidizi wa Raisi, kwa hiyo unaweza kupewa assignment inayohusu wizara yeyote ili ukasaidiane na waziri anaehusika. Na pia utakuwa unamwakilisha Raisi katika majukumu mbalimbali pamoja na ziara za ndani na nje, kufungua miradi nk. Kukiwa na ugeni kutoka nje wewe utahudhuria mikutano hiyo na Raisi karibu yote, wakati mawaziri ni wale tu wanaohusika na jambo litakalozunguziwa ndio wanahudhuria
Kwa hiyo ni uteuzi muhimu sana kwa Raisi na anapewa mtu ambaye ana akili ya kutambua na kuelewa mambo kwa haraka kuhusu siasa za ndani na mahusiano na nchi za nje. Unakuwa pia mshauri wa karibu sana wa Raisi katika mambo yanayohusu kila Wizara. Hata raisi akitaka kumtimua waziri mtu wa kwanza kuongea nae atakuwa wewe, kisha Waziri Mkuu ndio ataambiwa. Na una nguvu ya kumshauri Raisi kuwa waziri fulani katika wizara fulani hafai. Kumbuka kwa mfano, Prof. Mwandosya akiwa Waziri asiye na wizara maalum ndie hata alienda Rwanda kutatua mtifuano kati ya Kikwete na Kagame. Alifanya kazi nyingi sana kwa niaba ya Kikwete. Lakini mara nyingi hufanyi hizo kazi kwa uonekano. Unatakiwa kumfanya Raisi ang'are bila wewe kung'ara. Unakuwa busy sana, hivyo lazima uwe mchapakazi wa kweli.
Uwaziri usio na Wizara maalum kimsingi ni kama maandalizi ya kukufanya uwe raisi. Ni sawa na kuwa Raisi Msaidizi na Waziri Mkuu msaidizi asiyetambulika kikatiba, lakini somehow unamzidi hata Waziri Mkuu. Waziri asiye na wizara maalum anawajibika zaidi kwa raisi kuliko kwa Waziri Mkuu. Waziri Mkuu anaweza kuwa na majadiliano na Raisi juu ya jambo fulani, na Raisi akamwambia Waziri Mkuu utamwakilisha Raisi katika hayo majadiliano. Watu vihiyo walikuwa wanabeza uteuzi wa Prof. Mwandosya kwenye hii nafasi, niliwashangaa sana.
Kumbuka pia, ili kumdanganya Mwandosya kwamba atakuwa raisi baada yake, JK alimpa nafasi hii, kumbe ilikuwa ni chenga ya mwili. JK alitambua wazi alihitaji akili za mtu kama Mwandosya kuendesha nchi wakati anaitwa dhaifu nk. Kama uligundua, mwishoni JK alionekana kuwa na busara sana za uongozi - nyuma ya hilo ilikuwa ni akili za Prof. Mwandosya.
Hii ndio nafasi nasubiri mama Samia aniteue!