Mwanza: Akutwa amekufa pembeni kukiwa na ujumbe ‘mke wa mtu ni sumu’

Mwanza: Akutwa amekufa pembeni kukiwa na ujumbe ‘mke wa mtu ni sumu’

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji ya mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40-42 yaliyotokea katika mtaa wa Kanyerere kata ya Mkuyuni mkoani humo.

"Kando ya mwili wa marehemu kulikutwa ujumbe uliosomeka kuwa 'mke wa mtu ni sumu' watuhumiwa wanahojiwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani," amesema Muliro jana Jumatano Machi 31, 2021 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Wakati huohuo, amesema wanamshikilia Mengi Muheta ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Kishiri pamoja na wenzake 18 kwa tuhuma za wizi wa vitabu 529 vya shule za msingi.

Watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako ulioendeshwa kati ya mwezi Februari na Machi, 2021 na kwamba vitabu hivyo ni vya shule ya msingi Bujingwa, Igoma na Manguluma zote za wilayani Kwimba mkoani Mwanza.

Muliro amesema vitabu hivyo viliibwa kwa nyakati tofauti baada ya watuhumiwa kuvunja ofisi za shule hizo.

"Uhalifu huo umefanywa na walimu, walinzi na baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wanataka kuvinunua jijini Mwanza ambapo ili kuidhinisha uhalifu huo walikuwa wanafuta alama maalumu inayowekwa kuashiria vinamilikiwa na serikali inayosomeka "hakiuzwi" ili waweze kuviuza kwa urahisi."

"Baada ya kuwakamata tunaendelea na uchunguzi kuwabaini wahusika wote, upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani,” amesema.

Pia, wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusafirisha gunia sita zilizokuwa na dawa za kulevya aina ya bangi katika kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela.
 
Wameamua kugawana majengo ya serikali kisa mtu ambae ataendelea na maisha yake wakati wao wakitumbukia
Huwa ninawambia watu hiki kitu wananiona mjinga, ukioa mke alafu akachepuka achana nae wala hata ukimkuta kitandani kwako na jamaa wewe toka nje alafu rudi baadae mwambie aondoke, kuliko kumuua mtu alafu unaishia jela
 
Huwa ninawambia watu hiki kitu wananiona mjinga, ukioa mke alafu akachepuka achana nae wala hata ukimkuta kitandani kwako na jamaa wewe toka nje alafu rudi baadae mwambie aondoke, kuliko kumuua mtu alafu unaishia jela
jamaa hajawa convicted bado😁
 
Aliyeingia kwa mke wa jirani yake maana yake ni kwamba ameenda kujinywesha sumu mwenyewe.


Hao walimu walioiba vitabu wakaamua kuviuza nao huenda uchumi umekuwa mbaya kwao wakaamua kujilipua. Tamaa mbaya


Waliokamatwa na bhangi wakawasalimu wenzao huko segerea. Bhangi inaharibu vijana wasio na ajira.
 
Kwenye maisha yako usiguse mke wa mtu, hata usipogundulika lakini vita yake kiroho itakugharimu tu one day labda ufanye toba ya kweli. Kiapo cha mke wa ndoa iwe kanisani, msikitini au popote ni hatari hatari hatari kuingilia ukiwa unafahamu
 
Bado ni fikirishi ... Kama kauliwa na wahuni tu wakaamua kutia bosheni kwa kuandika kikaratasi na kukitupa !!?? Mme gani huyo aandike hivyo baada ya mauaji !!!?? Si anakuwa amejilengesha !!??
Amejilengesha kivipi mkuu?

Wewe umemkuta mke wako anapigwa mashine na lijaaamaa lingine kumuua yule jamaa na kutumtupa huku umeacha message sio issue
 
Back
Top Bottom