MWANZA: Aliyefariki wiki chache nyuma akutwa akiwa mzima

MWANZA: Aliyefariki wiki chache nyuma akutwa akiwa mzima

Wazungu kwa uelewa ninyi chakushangaza kuamini yesu alikufa na akafufuka munaamini
Na huyo mwana wa Yesu ama
Hapo kama ni uchawi mnajuana maana waswahili ni mambo ya maovu tu ndio tunakazania
Wizi, uchawi, uchafu

Wazungu hawana ujinga huu na kila kitu lazima kichunguzwe mpaka kijulikane kitaaluma na sayansi pia

Ila ukweli lazima upatikane na hawawezi kufikia maamuzi na kusema tu huu ni ushirikina au ooh kafufuka kama yesu ila mtaa mwingine na sio kaburini
 
Wakazi wa Kijiji cha Salong’we kilichopo wilayani Magu mkoani Mwanza wamekumbwa na taharuki baada ya mtoto aitwaye Mabilika Wilson aliyefariki na kuzikwa tarehe 17 mwezi huu kupatikana akiwa hai katika Kijiji cha Mwangika wilayani Kwimba mkoani humo.

Wilson Bulabo ni baba mzazi wa mtoto huyo amesema ni kweli mtoto wake huyo aliumwa kwa siku mbili na kufariki hatimaye wakamzika lakini alipoenda kumuangalia huyo mtoto aliyeonekana Kijiji cha Mwangika alimgundua kuwa ndiye mtoto wake aliyezikwa wiki chache zilizopita.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amefika katika Kijiji hicho na kushuhudia kaburi likifukuliwa kwa ajili ya taratibu za uchunguzi wa tukio hilo ambapo amewataka wakazi wa Kijiji hicho na vijiji vya Jirani, kuwa watulivu kipindi ambacho uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

#EastAfricaTV
View attachment 2604593
Sukhuma witches!
 
Kamati ya ulinzi na usalama ya eneo husika ikifanya kazi yake sawasawa yatakuwa kama yule Mama wa Maiti ya mtoto kugeuka kuwa Jiwe
Hata yule wa jiwe huenda ni kweli lakini kazibwa mdomo, watu wana mambo ya siri sana kuzidi hata dunia yenyewe
 
Hivi ukishazika unaweza kwenda kufukua bila kibali? Hapo umesoma ukaelewa?
Kibali Cha kufukua maiti kinatoka Mahakamani na si police, tena huko Mahakamani ni hadi hàkimu Mchunguza maiti ajiridhishe na shauri hilo ndiyo atatoa hicho kibali! Sasa jiulize je huyo Mtoto aliyeonekana akiwa hai ambae Baba Mtu kasema ni mwanawe,je DNA imesha thibitisha hilo!? Isije kuwa ni wenge tu la kufiwa na Mtoto sema akili haitaki kukubali!!
 
Back
Top Bottom