Mwanza City: The Photo Gallery

Naunga mkono baadhi ya hoja .ila Kwa uzoefu wangu pia maeneo ambayo umeyarefer ni Peri urban Yani nje kidogo ya mji ...ndio utapata hizo disturbance . eneo pekee ambalo Lina majaruba na liko mjini ni kati nyegezi kuja mkuyuni pembeni mwa reli pale ..na Yale ni maeneo ya viwanda..na hifadhi za reli ...eneo lingine maybe nyamhongolo ambapo ni eneo la viwanda na uwekezaji maaalumu
 
Stendi ya nyamhongolo.. haiwezi kujaa kiurahisi hivyo .na kama inajaa waondoe tata zote ziishie kisesa..yabaki magari makubwa ...
Stendi ya kisesa isiwe ya hiace za vijijini tu Bali pia hizo tata ziondolew nyamhongolo.zipelekwe huko
Changamoto kubwa kwa Mwanza niliyoiona suala la usafiri siyo stressful Kama Dar.

Mwanza bado abiria wanaringa kupanda daladala. Ukiwa na hiace lako limechoka utapiga yowe masaa 6 abiria hawapandi.

Abiria wanataka daladala jipya au lenye TV wanasubiria Hilo Hilo.

Hivyo, wengi wanahisi wakiweka coaster kubwa hasa milango 2 Kama za Dar hawapata idadi ya abiria kujazana gari.

Hata kwasasa coaster nyingi kubwa ni zile zinazoenda sehemu Kama Buswelu au Buhongwa ambako Kuna abiria wengi.
 
Hii concept yako imekaa kwenye ruti za mjini.....ila mim Nazungumzia ruti za vijijini huko ..
Kwa wazo lako ni kweli mwanza usafiri sio stresful kama dar ..Kwa sababu dar Ina watu wengi zaidi ya Mara nne ya mwanza ...
Kuhusu Costa ,,, coaster mwanza zimeongezeka sana ndani miaka ya karibuni ..
Ruti ya nyashishi kwenda kisesa (nadra kuona hiace)
Ruti ya nyamadoke kwenda nyashishi (sijaona hiace)
Ruti ya ilalila kuja mjini (hiace chache)
Ruti ya town kwenda nyaguruguru(hiace chache)
Hizi ruti Kwa asilimia kubwa zimeunganisha maeneo mengi ya mwanza ..
Daladala ndogo zipo sana sana barabara ya airport
 
Labda niulize kidogo, ukitoka National, ukashuka chini Kama unaenda Mahina, Nyanguruguru, mpaka huko mbele naambiwa ukienda unafika Buzuruga kwa short cut huo ni siyo katikati ya mji???

Siku ya mwisho nataka kuondoka, nilipanda daladala Kijereshi nikaenda mpaka Kishiri ( hapa barabara ni ya vumbi na mabonde ), nilipofika Kishiri nikagundua ni sehemu ambayo wananchi wameichangamsha sana lakini haina mkono wa serikali kabisa.

Nilipofika hapo Kishiri center, tukapelekwa Kuna sehemu panaitwa Bukaga ni mbele ya Kishiri center barabara ni vumbi Ila watu wamejenga kweli. Hiyo barabara inaenda mpaka inakutana na Rami ya Kisesa Usagara eneo la Sumve. Kumbuka hii Kishiri yote ni Nyamagana.

Kuna siku ndio nilichoka, nilipelekwa Luchelele Malimbe huko karibu na ziwa, kutoka kituo Cha daladala nauli ya Bajaj elfu 4!!

Hapo ndio nikagundua kwanini watu wanajaa Kisesa kuliko baadhi ya maeneo ya Nyamagana na Ilemela.

Ingawa rami ya sabasaba imesaidia kuifungua Buswelu, na maeneo yake ya pembeni.
 
Yeah ....hayo maeneo yote uliyataja sio katikati ya mji ni pembeni.....ni maeneo ambayo ni Peri urban na ndio hayo yenye changamoto kubwa kihuduma
 
Yeah ....hayo maeneo yote uliyataja sio katikati ya mji ni pembeni.....ni maeneo ambayo ni Peri urban na ndio hayo yenye changamoto kubwa kihuduma
Kwahiyo kwa Mwanza tukizungumza Urban tunazungumzia wapi?
 
Stendi Ina capacity ya mabas 120 ,,,kinachowavuruga ni hizo tata za kwenda simiyu ,mugumu,bunda ,kisorya,nyambiti,musoma na kiabakari ...wazipeleke kwenye stendi ya kisesa...ni njia nyepesi isiyo na gharama
Hizi tata ndio zinachangia stendi kuwa ndogo, au wangeweka stendi ndogo nje.
 
Au kublock kabisa... Maana mi sioni haja ya mtu kutukana matusi ya ajabu ajabu...
 
Ni kubwa kama utahusisha n parking ya malory mkuu.
 
Anzia mkolani Hadi town then town Hadi ilemela ,town Hadi nyakato ...
Nyegezi
Butimba
Mkuyuni
Igogo
Town
Kirumba
Isamilo
Pasiansi
Kitangiri
Nyamoro
Nyakato
Mabatini
Mbugani
Pamba
Hizi ndio kata za mjini
Lakini hii ni Mwanza ya mwaka 2010 huko. Sasa hivi ni miaka 10 baadaye lazima fikra ziendane na ukubwa wa mji.
 
Nje ya stand pale ndio daladala zinashusha. Kwahiyo ukitaka hizo bus ndogo zipakie tena hapo nje, inakuwa changanyikeni.
Pale nje waparekebishe kuna eneo kubwa sana, watenge sehemu ya daladala na sehemu ya kupark tata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…