Ifike mahali rasilimali zisambazwe nchi yote sio kila kitu kinawekwa sehemu moja, Mwanza miradi yote ya barabara ipo kwenye feasibility study miaka nenda rudi hakuna utekelezaji, nahisi baada ya mkoa wa Dar ni Mwanza inafuata kwa wingi wa watu hata geographically hazina tofauti sana 3.6mp vs 5mp apa gap ni kama 200k, kama Mwanza ina idadi kubwa ya watu wanashindwa nini kuboresha huduma za kijamii. Barabara ya Kenyatta ikipanuliwa njia nne mpaka Mwanangwa with BRT wamepata pesa ya kujenga daraja dar bila bajeti kupitishwa ila iyo barabara inasubiri bajeti. Barabara ya Airport Igombe Nyanguge inafanyiwa feasibility study miongo kadhaa sasa huku ni kudumaza maendeleo ya jiji la Mwanza na kuifanya miji mingine kuwa superior kimiundombinu. Sasa wabunge wa Kanda ya ziwa wasiwaache Wabunge wa Ilemela na Nyamagana wapambane peke yao kwani Mwanza ni kioo cha ukanda wetu kwani nikiwa mkoa wowote nikasema natokea Kanda ya Ziwa Mkoa watakao anza kuguess ni Mwanza, Wabunge wapambane Barabara ya Mwanza city centre to Nyanguge 4ways with BRT,barabara ya KenyattaMwanangwa 4ways with BRT, Buhongwa_Igoma 4ways with BRT, barabara ya Airport -Nyanguge 2ways with special barabara kwaajiri ya Mashindano ya baiskeli kwa sababu ni mchezo pendwa kwa Wana Lakezone, Barabara ya Kigongo-Usagara iwe njia nne na flyover iwepo Usagara kwa maana ya junction iliyopo Usagara yaani Usagara-City centre, Usagara-Mwanangwa,Usagara-Kigongo, Usagara-Kisesa