Uliyoyataja yote mzee Busan . serikali haiwezi kuyafanya Kwa muda unaouhitaji ..mfano unataka flyover Usagara ambayo si chini ya bilioni 100 ..at the same time mwanza ni jiji lenye uhaba mkubwa wa maji .....
Nirudie kusema hili mwanza ni mji ambao una pewa fedha nyingi kuliko majiji mengine ukiacha dar Kwa sababu ya miradi yake ya kimkakati....daraja tu la busisi pesa Yake ingejenga hyo fly over ,ikajenga dual carriage hata 3 za km 20 na mambo mengine kede kede ...
Mimi siungi mkono hoja ya kwamba mwanza ni jiji linaloonewa
Kaka kubali tu, Mwanza imetengwa kwa muda mrefu sana imekuja kukumbukwa kipindi cha Magufuli.
Sasa mji mkubwa kama wa mwanza mahitaji yake ni makubwa vilevile.
Sidhani kama mwanza inaizidi Dodoma kwenye kupata pesa nyingi za miradi.
Na hasa tukisema jiji kwa maana ya Nyamagana na Ilemela hamna kitu ndugu yangu tusijifariji.
Daraja la kigongo busisi haliko kwenye jiji, liko Misungwi na Sengerema.
Meli ile ni mradi wa kanda ya ziwa sio mwanza tu.
Mradi pekee utakaogusa na kuleta mandhari jijini ni sgr.
Miradi iliobaki ni ya kawaida tu inafanyika nchi nzima.
Chukua miradi ya jiji la Dodoma linganisha na jiji la mwanza, hata nusu sidhani kama tunawafikia.
Dar kila siku inapata pesa za miradi halafu sisi tukae kimya?
Kisa kuna jpm Bridge ambayo hata haiko kwenye jiji la Mwanza.
Au kaka unataka tusubiri daraja na sgr viishe ndio tuombe miradi mingine? Mbona kwingine miradi inabebanishwa tena mikubwa?