Mwanza City: The Photo Gallery

Misungwi na Magu hazitakubali mkuu
Mkuu Halmashauri ya Magu na Misungwi zote ni za serikali kuu wala si mtu binafsi hivyo kama serikali kuu ikiona kuna umuhimu (umuhimu huo tayari upo) wa kumega maeneo ya hizo halmashauri za wilaya na kuipa Mwanza jiji hilo jambo litafanyika tu bila kikwazo chochote. Serikali kuu ndio yenye maamuzi ya mwisho juu ya mipaka ya nchi, mikoa wilaya, kata na hata vijiji wengine huku chini ni watekelezaji tu. Hivyo ni suala la muda tu.
 
Kwa Sengerema ni ngumu, Hata hizo Magu na Misungwi ni ngumu pia sema tu kwa Magu na Misungwi zitamegwa sehemu kuuunda wilaya mpya na sio halmashauri za hiyo miji zitaongezwa kuunda jiji. Hayo maeneo yatayomegwa yanatokana na ukaribu wao na jiji kihuduma na si vinginevyo. Tayari Kisesa na Usagara japo kuwa zipo Misungwi na Magu lakini wananchi wa maeneo yao ni rahisi kupata huduma jijini kuliko kuliko Magu au Misungwi mjini.
 
Mimi mmoja wapo,naishi zangu Usagara ambayo ni Misungwi lakini huduma zangu zote napata Nyamagana na wakati mwingine Ilemela na jiji lenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…