JINSI NILIVYONUSURIKA KIFO BAADA YA MIKDDE KUNIPONZA
Kama kawaida juzi siku ya jumapili niliingia kwenye uzi wangu pendwa wa Mwanza city photo gallery kupeana mawili matatu kuhusiana na miradi mbalimbali zinazoendelea jiji Mwanza huku tukihabarishana juu ya mambo kadha wa kadha, sasa kuna mdau wangu mmoja anajulikana kama mikdde akaomba picha ya jengo la mahakama kuu ya kutolea haki kanda ya ziwa lililojengwa Buswelu jiji Mwanza, nami bila hajizi niliwiwa kulipost humu tena ingawa nilishawahi kulitupia humu ndani.
*
Story inaanza hivi siku ya jana nilikuwa na mihadi na mganga mkuu wa Ilemela, kwaajiri ya kupewa mawili matatu kuhusiana na mambo mbalimbli ya afya, kama kawaida niliamka asubuhi nikijua task yangu leo asubuhi nionane na DMO then nirudi job kupeleka mrejesho.
Nilifika ofisini kwa DMO, kwa bahati mbaya sikumkuta, bali nilikutana na mdada mmoja mzuri balaa aliyejitambulisha kama secretary wake, kiukweli huyu mdada alinitoa udenda[emoji39][emoji39][emoji39][emoji39] lakini nikapiga moyo konde nikisema kitombile acha hili kombe linipite [emoji23][emoji23][emoji23], nikataka kuchukua namba kwa mahitaji yangu ya baadae lakini nikasita, basi yule dada akaniambia kama naweza kumsubiri sawa usipoweza unaweza kwenda nami nitamtaharifu ujio wako ili mpange tena mihadi ya kuonana, tuliagana na yule bidada nikaondoka zangu.
Nilipokuwa naondoka nikakumbuka mdau wangu wa humu Mikdde aliniomba picha ya jengo la mahakama ya kutolea haki[emoji848][emoji848][emoji848], nikaajisemea "muda ndio huu sasa" nilijisogeza mdogo mdogo adi kwenye jengo hilo kwani halipo mbali na ofisi za DMO pamoja na NIDA.
Wakati nakaribia eneo hilo la jengo nikaona watu wengi sana na 95% walikuwa wanawake waliopendeza sana kwenye mavazi mbalimbli, na vidada vya size yangu vilikuwepo kama ilivyoada kitombile mimi huwa mdhaifu sana kwa wadada warembo huwa nakuwa kichaa kwa muda, wakati ni kiwaza nifanye nini kufanikisha hazima yangu ya kupata picha ya hili jengo.........
ITAENDELEA..