Mwanza: Daraja la Magufuli limekamilika. Je, Makamanda wa CHADEMA watalitumia?

Watanzania tutafute maarifa.

Unafaham Tsh Trillion 10 ya Leo ni USD ngapi?

Na Trillion 1 ya 2010 ilikuwa Sawa na USD ngapi ?
 
Mnatuonea sana vijana 2000 mtoto akinyea mkono usiukate mwelekeze Ata kuelewa kutulaumu siyo solution hakuna aliyezaliwa anajua hapa Duniani wote tunajifunza umri wangu ni miaka 24 tu naomba kuwasilisha
Bila shaka umezaliwa kuanzia 2000,siyo kosa lako na historia ya nchii huijui.
 
Watanzania tutafute maarifa.

Unafaham Tsh Trillion 10 ya Leo ni USD ngapi?

Na Trillion 1 ya 2010 ilikuwa Sawa na USD ngapi ?

Unajua hesabu? Serikali ya Tanzania kuanzia mwaka 1961 hadi 2021 ilikuwa imekopa Trilioni 60 ,Tafuta wastani kwa mwaka.....Serikali ya Bi Kimzikazi ndani ya miaka mitatu imekoa trilioni 30 tafuta wastani kwa mwaka.

Haujaambiwa exchange rate maana tukitaka kukumbushia zamani basi hata nyerere alikuwa siyo mwizi wa mali za umma ,alikuwa hana matumizi yasiyo na kichwa wala miguu hadi anafariki alikuwa na nyumba moja tu msasani tena zile kama za magomeni upande vyumba kati korido.

Nyerere hadi anastaafu alikuwa hana gari ya maana hadi wizara ya Mambo ya nje wakampa Nissan Muranno,alikuwa hana nyumba kwao huko Butiama ikabidi wamjengee na tena akataka aikatae maana ni kubwa kwani yeye tembo?
 
Mnatuonea sana vijana 2000 mtoto akinyea mkono usiukate mwelekeze Ata kuelewa kutulaumu siyo solution hakuna aliyezaliwa anajua hapa Duniani wote tunajifunza umri wangu ni miaka 24 tu naomba kuwasilisha
Uko sahihi 100%,samahani kama nitakuwa nimekukwaza ndugu yangu,unajua lugha za kejeli za vijana wenzio zinasababisha tuwape ukweli kwa kutumia historia.Vijana wengi wanaona marais wote wanne waliotangulia kabla ya Awamu ya Tano hakuna walichofanya ila baada ya Awamu ya Tano ndiyo nchi imejengwa.
 
Kwani hela zilizojenga chadema hawakulipa kodi ili kuwezesha upatikaji wake?
 
Tunapenda mtueleweshe sema amani sana mkuu tuko pamoja
 
Umekurupuka! Niliemquote alikuwaanazungumzia samaki na hilo daraja ...nilichomwambia samaki kusafirishwa hakuhusiani na hilo daraja. Jaribu kuwa muelewa
 
Sasa Chadema wanahusika vipi hapo mkuuu.
Je unazani Chadema hawalipi Kodi mkuu.
Achaa mentality za kimaskini na za kichuki .

Chadema ninwanachi.kama walivyo CCM pia tofauti ni itikadii tuuu .
So leave such kind of hypothetically spirits and poverty spirits
 
Weka ushahidi hapa wa video/picha ukisema CHADEMA wanapinga ujenzi wa daraja hilo.

Kodi za wananchi zinapotumika haziangalii chama wala itikadi.

Kwani mkandarasi wa hilo daraja ni mwanachama wa CCM au CHADEMA?

Jibu utalipata hapa,sasa kama mkandarasi hata sio raia na hana itikadi yoyote kwanini walipa kodi wazuiwe kiitikadi?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…