Mwanza: Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, kutumikia mwezi mmoja tu

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imemhukumu Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kumkuta na hatia katika makosa mawili kati ya matatu kwenye kesi ya jinai namba 10/2022.

Akisoma hukumu hiyo leo Januari 25, 2023, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Monica Ndyekobora amesema Zumaridi na wenzake wanne wamekutwa na hatia katika makosa mawili ambayo ni pamoja na kumzuia Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana, Christina Mwisongo (46) kutekeleza wajibu wake na kuzuia maofisa wa polisi kutekeleza jukumu lao.

Pamoja na kosa hilo, Hakimu Ndyekobora amewakuta hawana hatia katika kosa la shambulio la kudhuru mwili.
Katika kesi hiyo, washitakiwa wengine wanne wameachiliwa huru.

Hata hivyo, Zumaridi atatumikia mwezi mmoja katika gereza la Butimba jijini Mwanza kutokana na kukaa miezi 11 mahabusu wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa, huku wenzake wanne wakitumikia kufungo cha nje.
 
Hata hivyo, Zumaridi atatumikia mwezi mmoja katika gereza la Butimba jijini Mwanza kutokana na kukaa miezi 11 mahabusu wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa
Haka kakipande kangekuwa kanatumika kwa wote wenye kesi kwana watu wangekuwa wanaidai Jamuhuri fidia ya miaka ambayo wametumikia kabla ya hukumu
 
Hawa watu wanaocheza na imani wangepewa lesseni baada ya kumaliza mafunzo kwenye vyuo vinavyotambulika hizi resource zisingetumika kwa sarakasi za namna hii.

Wazir wa Mambo ya ndani tafadhali mshauri Rais ipasavyo
 
Serikali ikate rufaa, adhabu inaanza siku ya kutamkwa, rumande sio sehemu ya adhabu
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imemhukumu Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi na wafuasi wake wanne kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kuwakuta na hatia katika makosa mawili kati ya matatu kwenye kesi ya jinai namba 10/2022 huku wafuasi wengine wanne wakiachiwa huru

Mahakama imesema Mfalme Zumaridi atatumikia mwezi mmoja katika gereza kuu la Butimba jijini Mwanza kutokana na kukaa miezi 11 mahabusu wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa huku wenzake wanne wakitumikia kufungo cha mwaka mmoja nje ya gereza

---

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza imemhukumu Diana Bundala maarufu 'Mfalme Zumaridi' kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kumkuta na hatia katika makosa mawili kati ya matatu kwenye kesi ya jinai namba 10/2022.

Akisoma hukumu hiyo leo Januari 25, 2023, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Monica Ndyekobora amesema Zumaridi na wenzake wanne wamekutwa na hatia katika makosa mawili ambayo ni pamoja na kumzuia Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana, Christina Mwisongo (46) kutekeleza wajibu wake na kuzuia maofisa wa polisi kutekeleza jukumu lao.

Pamoja na kosa hilo, Hakimu Ndyekobora amewakuta hawana hatia katika kosa la shambulio la kudhuru mwili.
Katika kesi hiyo, washitakiwa wengine wanne wameachiliwa huru.

Hata hivyo, Zumaridi atatumikia mwezi mmoja katika gereza la Butimba jijini Mwanza kutokana na kukaa miezi 11 mahabusu wakati kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa, huku wenzake wanne wakitumikia kufungo cha nje.
 
Serikali ikate rufaa, adhabu inaanza siku ya kutamkwa, rumande sio sehemu ya adhabu
Mi naona kuwa adhabu huanza pale mtuhumiwa anapotiwa hatiani na sio siku ya kukamatwa.
Japo mi sio mwanasheria
 
Back
Top Bottom