Karani wa uandikishaji wa mtaa wa Kabambo huko Mwanza amebanwa baada ya kugundulika ameongeza majina hewa takribani 200 kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Teknolojia imezidi kufichua mbinu za zamani za kuhujumu uchaguzi kwa kuongeza wapiga kura hewa kutoka watu 688 hadi 860
Kuna mama juzi nilimpigia simu kumuuliza akajibu, ajiandikishe kwenye kura zitakazo kuja kuibiwa ili iweje , halafu alikua sisiem damu kipindi za mwendazake😁😁😁
TAMISEMI wizara katika Ofisi ya Rais(OR)-Tawala za mikoa serikali za mitaa inaleta jeuri ya chama dola kongwe CCM kwa kutuletea matatizo kupanga uchafuzi wa mchakato huu wa kuelekea uchaguzi wa TAMISEMI 2024 November.
Kujaza majina na kura za maruhani kutumika na CCM kupiga kura, kisha kujitangazia ushindi wa kishindo kupitia mamluki katika kuta za majengo wakijidai ni matokeo ya uchaguzi huru uliosusiwa na raia.
Huu utaratibu wa kujiandikisha nadhani umepitwa na wakati ni kupoteza muda tu. Karne ya 21, miaka 60 ya uhuru tunatumia makatasi. Tutoke analojia twende kidigitali zaidi.
Hapo mwandikishaji amepewa lengo/idadi ya watu anaotakiwa kuandikisha ndiyo maana akiona hali ngumu anaongezea majina yake.
Kuna wajinga wa kiccm na uchawa wao huja humu na vihoja uchwara kwamba Samia anapendwa na ccm inakubalika sana. Ujinga wao na wafuasi wao eanaosapoti ujinga huwo, bila ya figisu ccm haina uwezo hata wakushinda 20%.
SISIEMU bila wizi hawatoboi ,huwa nashindwa kuelewa ,wao si wanasema wanakubalika na wana wanachama wengi sana ,sasa kwanini bado wanaiba kura? Si wansema kama wamefanya maendeleo ya kufa mtu ,sasa mbona wanaogopa?