LGE2024 Mwanza: Karani abanwa baada ya kuongeza majina hewa 200 kwenye daftari la Wapiga Kura

LGE2024 Mwanza: Karani abanwa baada ya kuongeza majina hewa 200 kwenye daftari la Wapiga Kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Karani wa uandikishaji wa mtaa wa Kabambo huko Mwanza amebanwa baada ya kugundulika ameongeza majina hewa takribani 200 kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Teknolojia imezidi kufichua mbinu za zamani za kuhujumu uchaguzi kwa kuongeza wapiga kura hewa kutoka watu 688 hadi 860
Pia, Soma:

==>
Karatu: Kijana Jasiri aibua Kashfa, Msimamizi wa kituo aondoka na daftari la wapiga kura ajaza majina kivyake!
==> Shinyanga: Mwanafunzi wa miaka 16 akutwa na wakala wa CHADEMA akiwa anajiandikisha kwenye Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa. Apigwa maswali mazito!
==> Special Thread: Hali ya Vituo vya Kujiandikisha kupiga Kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa Picha na Video
 
TAMISEMI wizara katika Ofisi ya Rais(OR)-Tawala za mikoa serikali za mitaa inaleta jeuri ya chama dola kongwe CCM kwa kutuletea matatizo kupanga uchafuzi wa mchakato huu wa kuelekea uchaguzi wa TAMISEMI 2024 November.

Kujaza majina na kura za maruhani kutumika na CCM kupiga kura, kisha kujitangazia ushindi wa kishindo kupitia mamluki katika kuta za majengo wakijidai ni matokeo ya uchaguzi huru uliosusiwa na raia.
 
CCM badilini mgombea mtapenya,

CHADEMA susia uchaguzi, harakati za kudai Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote viendelee.

Nilisema tangu awali,

Hapatafanyika uchaguzi wowote wa HAKI bila kwanza kupatikana Tume huru ya Uchaguzi na Katiba mpya kabla ya Uchaguzi wowote.

Tusubiri.
 
Huu utaratibu wa kujiandikisha nadhani umepitwa na wakati ni kupoteza muda tu. Karne ya 21, miaka 60 ya uhuru tunatumia makatasi. Tutoke analojia twende kidigitali zaidi.
Hapo mwandikishaji amepewa lengo/idadi ya watu anaotakiwa kuandikisha ndiyo maana akiona hali ngumu anaongezea majina yake.
 
Hivi wewe ukiwa Rufiji ukasikia kuwa kura imeibwa huko Mwanza na kupitisha kiongozi wa mtaa ambaye hajachagukiwa na wananchi wewe unapata faida gani?
 
Kuna wajinga wa kiccm na uchawa wao huja humu na vihoja uchwara kwamba Samia anapendwa na ccm inakubalika sana. Ujinga wao na wafuasi wao eanaosapoti ujinga huwo, bila ya figisu ccm haina uwezo hata wakushinda 20%.
 
Back
Top Bottom