Nimeshangaa sanaLakini nanyi waandishi saazingine huwa ninapata mashaka na kiwango chenu cha taaluma!
Kaliua ya mkoani Tabora ndiko madhila yalikotokea kakini kichwa cha habari kinatamka Mwanza, why?
"Gambe" labda umekunywa wewe.Hii habari hata haieleweki, mara kaliua mara mwanza, brother umekunywa pombe "gambe"
"Gambe" labda umekunywa wewe.
1. Habari inasikitisha sana.
2. Huwa mnalipwa kiasi gani kurukia treni kwa mbele?
View attachment 1823671
Narukia treni?
Wewe ndio umekurupuka, umepata taarifa ya kitu kaa chini uandike vizuri sio kukimbilia huku kupost, uonekane we ndio wa kwanza kupata taarifa?.
Unaendelea kukurupuka jombi. Originally kichwa kilikuwa hivi:
"Mtoto aungua Moto hadi kufa katika operesheni ya Dola."
Baada ya maelezo ya juu link hii kama ilivyo hapa niliambatanisha:
Mtoto ateketea kwa moto askari wakiendesha operesheni kuondoa wavamizi
Mtoto Nyanzore Ng'wandu (4) amefariki dunia kwa kuteketea kwa moto wakati wa operesheni ya kuwaondoa wananchi waliovamia eneo tengefu ndani ya Hifadhi ya jamii Isawimo inayoundwa na vijiji 11 vya...www.mwananchi.co.tz
Moderator wamekuja wakakarabati kwa makosa kichwa. Pia wakatoa link na kuya paste maelezo ambayo yana pia huo ukakasi wa Mwanza.
Kistaarabu - habari inasikitisha na hilo nimelisema. Makosa ya Moderator yanihusu miye vipi?
Bado tu huoni kukurupuka kwako?
Huyo mkuu wa wilaya achunguzwe
Haya poa braza K
Hivi serikali inachomea wananchi wake nyumba so sadπ‘π‘
Mtu mwenye akili timamu anaweza akafanya haya waliofanya hao mashetani?, mimi ningekuwa Rais, ningewalisha kitanzi hao mbwa wote endapo watathibitika pasi na shaka kufanya uzembe uliosababisha kifo cha mateso makali kiasi hicho kwa malaika mdogo kiasi hicho, lazima tuwe na utu at some point!!Habari hii ni kutoka Kaliua, Tabora ambako wale jamaa wasiokuwa na chembe ya utu walikuwa wametia timu kwenda kufanya yao.
Unachoma vipi nyumba ambayo wanaweza kuwemo ndani watoto wadogo, wazee au wasiojiweza?
Piga picha kumwona mtoto wa miaka 4 yuko je.
Eeh mola wetu umrehemu malaika wako huyu aliyetangulizwa kifedhuli kwako. Ukawakirimu majahili hawa ujira sawa sawa na matendo yao:
(Picha za tukio hili haziwekeki hapa katika hali yoyote).
=====
Mwanza. Mtoto Nyanzore Ng'wandu (4) amefariki dunia kwa kuteketea kwa moto wakati wa operesheni ya kuwaondoa wananchi waliovamia eneo tengefu ndani ya Hifadhi ya jamii Isawimo inayoundwa na vijiji 11 vya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana Ijumaa Juni 18, 2021 mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Abel Busalama amethibitisha kifo cha mtoto huyo kilichotokea wakati wa operesheni iliyofanyika Juni 16, 2021.
Mtoto aliyetekea kwa moto ni mjukuu wa mzee Ng'ombeikungire Ng'wandu, mkazi wa kijiji cha Kombe wilayani Kaliua.
"Serikali imesikitishwa na kifo cha mtoto huyo na vyombo vya dola vimeanza uchunguzi wa kuhusu tukio hilo. Mimi binafsi nimefika eneo hilo nikiongozana na kamati ya usalama ya wilaya."
"Kuna maswali na hoja nyingi kuhusu kifo cha mtoto yule, kwanza wana familia wanasema aliteketea baada ya kuanguka mlangoni katika jitihada za kujiokoa. Lakini eneo mwili upokutwa ni karibia hatua mbili kutoka mlangoni," amesema.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, kuna hisia kuwa kifo cha mtoto huyo ni tukio la kutengenezwa kwa nia ya kukwamisha operesheni ya kuwaondoa waliovamia eneo la hifadhi na kuendesha shughuli za kibinadamu ikiwemo makazi, kilimo, uvuvi na ufugaji.
"Siwezi kusema kwa uhakika ni nani ametengeneza tukio hilo lakini mazingira yanatia shaka na ndio maana vyombo vinafanya uchunguzi wa kina," amesema mkuu huyo wa wilaya
Akizungumzia tukio hilo, diwani wa Usinge, Titus Kavura amelaani kitendo cha askari Mamlaka ya Wanyamapori na Jeshi la Polisi walioshiriki operesheni hiyo kutumia nguvu na mabavu badala ya busara kiasi cha kuteketeza nyumba bila kutoa fursa kwa wananchi kujiokoa na kuokoa mali.
"Walichokuwa wanafanya askari wale ni kufika na kutia moto nyumba bila kujali ndani kuna watu wala mgonjwa, hii ndio maana wazazi walitimua mbio kujiokoa na kumsahau mtoto aliyekuwa amelala ndani," amesema diwani Kavura.
Mwanachi
Eti mtoto kakutwa hatua mbili toka mlangoni, ndio hoja ya utetezi hiyo, kama mtu kazidiwa na mto hapo na akadondoka alitakaje sasa? Awajibishwe mbwa huyo!!!!!!Kuna watu wana roho mbaya sana aisee.
Walllahi hakyaMungu, ikifika kesho huyo DC hajawajibishwa, naenda kuwasomea albadiri kuanzia huyo DC hadi aliyemuweka huyo DC hapo, potelea mbaliMnamchanganya Mama, anaweza akamtumbua DC wa Mwanza kumbe sio wa Mwanza!
Anyongwe mbwa huyo, ikithibitika kahusika na uzembe uliosababisha kifo cha mateso makali namna hiyo, tena kwa malaika wa miaka minne??!!πππππSio tu kuchunguzwa... Afukuzwe kazi kwa kosa la uharibifu wa mali na kusababisha kifo Cha mtoto...
Utetezi wake una ukakasi mkubwa huyo hafai kuwa kiongoz...
Ila itakua funzo kwa maDC wengine na huyo ajae baada ya kutumbuliwa huyu, kwamba maisha ya binadamu yana thamani kuliko kitu kingine chochote kile!!!Ishatokea hakuna litalobadilika
Hakika mkuuKwa nini hawakuwapa muda wa kuokoa Mali zilizokuwa ndani...
KwA nini wachome moto... Huu ni uharibifu wa mali kinyume na sheria.
Mkuu wa wilaya hafai kuwa kiongozi... Utetezi wake ni wa kutilia mashaka...