Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

Mwanza: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mbowe na wenzake wanyakuliwa na Polisi usiku wa manane, haijulikani wako kituo gani

View attachment 1861764

View attachment 1861765
View attachment 1861766

Usiku majira ya saa tisa, Polisi walivamia Hoteli aliyokuwa amefikia Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na wageni wengine pamoja na wenyeji wao.

Waliochukuliwa:
1. Freeman Mbowe
2. John Pambalu
3. John Heche
4. Rose Mayemba
5. Masenya(Mwenyekiti BAVICHA Ilemela)
6. Steven Odipo
7. Dr. Rwaitama
8. Seti (Dereva kanda ya Victoria)
9. Apollo (Afisa Habari Taifa)
10. Frank Novatus (CHASO)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benja (BAVICHA Kinondoni)

Mpaka sasa haijajulikana wamechukuliwa kwa kosa gani.

=====

My Take.
Uonevu, uvunjifu wa haki za kiraia, kutoheshimu katiba ya nchi unaendelea kwa kasi katika serikali ya Samia Suluhu Hassan.
Anyway, Aluta continua, uonevu huu utaisha oneday, dawa tutaipata tu.

Nimkumbusha Samia kuwa alikuwepo mtu katika nchi hii anaitwa Magufuli, tulimuita Chuma, Jiwe—Leo yuko wapi?

====

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)

Taarifa Kwa UMMA

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe..Freeman Mbowe alivamiwa na Jeshi la Polisi hotelini alipokuwa ( Kingdom Hotel) majira ya saa nane na nusu usiku na kumkamata pamoja na viongozi wengine waliokuwa naye.

Viongozi wengine walipelekwa Kituo cha Kati cha Polisi Mwanza,Ila Mwenyekiti Mbowe haijulikani alipelekwa wapi na mpaka Muda huu hakuna taarifa zozote za mahali alipo.
Waliokamatwa ni wafuatao;

1. Mhe .Freeman Mbow
2. Mhe.John Pambalu
3. Mhe. John Heche
4.Mhe. Rose mayemba
5. Masenya( Mwenyekiti Bavicha ilemela)
6. Steven Odipo
7.Dr. Azavel Lwaitama
8. Seti ( Dereva Kanda ya Victoria)
9. Apolinary Appolo (Afisa habari Taifa)
10. Frank Novatus (Chaso Mwanza)
11. Mwakiaba (Mwenyekiti Nyamagana)
12. Benjamin Kambarage ( M.kiti Bavicha kinondoni)

Tunalitaka Jeshi la Polisi kujitokeza na kusema alipo Mwenyekiti wa Taifa na sababu za kumkamata zilikuwa nini.

Tunalaani ukandamizaji huu wa Haki za Watanzania Kwa nguvu zote , na hizi NI dalili za wazi kuwa Udikteta uliokuwepo enzi za utawala wa Rais Magufuli bado unaendelea .

Tutatoa taarifa kadiri ya Muda na jinsi tutakavyozipokea .
Huyu dikteta wa kike ni mbaya kuliko shetani
 
Mtu kanichukulia milioni 370 yangu.
Mtu "kawapoteza" jamaa zangu wawili.
Mtu kaharibu biashara yangu ya korosho na kunisababishia hasara ya mamia ya mamilioni.
Mtu kaharibu mfumo wa biashara nchini na kusababisha nisifikie malengo yangu.
Huyo mtu akifa nisishangilie!!???
Mungu yu Mwema, kila wakati Mungu Yu Mwema.
Kamwe hatutaacha kumlilia na Yeye Yahweh hatuachi bila kutufuta machozi.
Wewe inaonyesha ukiingia majaribuni na kupoteza Mali kwa kusudi la Mungu kama Ilivyokua kwa Ayubu, utamtukana mungu kama afande sele
 
Vipi kwani?

Si mnapumua baada ya dhalimu wenu kufariki?
safari ya wana wa Israel haikuwa rahisi, wapo waliokuwamo kwenye safari hiyo walikuwa wakimlaumu Musa na wapo walioamini Musa atawavusha. so wapumbavu kama ninyi mnaojitokeza kusema hamna shida na katiba mpya ni wapumbavu tu kama wale wa enzi za Musa. Miaka 60 huo uchumi mnnaojenga usiokuwa ni upi? afu mafala hayazinduki tu, ndio maana sisi tz umasikini kuisha ni ndoto
 
Chadema wajioange vizur ujinga waache waachane na swala la katiba wadili sasa na mahitaji ya wananhi wasimame nayo majukwaani
 
Watu wanapotendewa mbaya wewe unanufaika na Nini!....kama miTOZO tunalipa wote au wenzetu mna exemption
Sijaona sehemu yoyote Samia katendea mtu baya.

CDM walichotaka battle sasa ukitaka battle mwenyewe ukapigwa utakuwa umeonewa ?
 
sweka ndani wote na mjinga atakayesogea eneo la tukio vunja magoti kabisa...

badala muhamasishane kutafuta hela mnahamasishana ujinga tu kila siku halafu baada ya hapo mnaomba michango...
Kuzungumzia katiba ni ujinga ?! . Elimu inayotumika Tz ni janga.
 
Chadema wajioange vizur ujinga waache waachane na swala la katiba wadili sasa na mahitaji ya wananhi wasimame nayo majukwaani
Yani umeshindwa hata kujali yalitokea kwa mwendazake kwenye KATIBA hii.
 
Mama atamaliza vibaya zaidi akiendelea hv.
Maisha magumu, tozo kila eneo, uhuru na democrasia hakuna ,maendeleo hakuna..
mpaka sasa mama hajaleta jipya zaidi ya kutudanganya kwa kuachia watu wawili watatu lakini maumivu aliyoleta ni makubwa zaidi...
Maumivu aliyoleta mama hayajapata kutokea hapa Tz.
 
Chadema inapenda shari ndio siasa zake,usipofanya hivi watakupapasa hata makario,inatakiwa mjirekebishe,
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Back
Top Bottom