Hyo agenda ya katiba ingekuwa na support ya wananchi wangeandamana, Sasa wananchi tu tumevurugwa na makodi mengi mara tozo mara ajira then utuambie katiba unafikiria tutakuelewa. In short CDM waje na agenda zinazogusa wananchi ka tozo, afya na ajira uone ka watakosa support hyo katiba ni janja Yao ya kutaka madaraka
Mkuu hayo matatizo yanayogusa wananchi: tozo, afya, ajira, n.k. haitatokea yashughulikiwe kikamilifu kwa vile si katiba iliyopo wala bunge lililopo vinaweza kuibana serikali kutimiza wajibu wake kwa wananchi. Katiba iliyopo inamuweka Rais juu ya kila mhimili, taasisi na sheria. Kazi za kisiasa zimejazwa (overloaded) serikalini na maslahi mazito. Gharama ya kuendesha serikali (overheads) ni kubwa haiwiani na hali ya uchumi. Utashi na maslahi ya viongozi ndio kipaumbele. Hazina ya taifa inaweza kuchotwa na kutumika kwa kadiri Rais anavyojisikia na kuruhusu. Hata akiamua kujenga mji wake mpya hakuna wa kuhoji.
Watanzania hawawezi kuandamana hata wakinyanyaswa namna gani. Msg toka State iko clear: andamana uwe kilema au uache wategemezi/watoto wako yatima. Aidha, kila mtu anawaza jinsi atakavyotoboa kivyake. Hakuna mshikamano wala maslahi ya pamoja. Ukipata masahibu utajijua mwenyewe.
Kwa katiba hii hii, wakati wowote, mtu wa hatari anaweza si tu kushika madaraka kama ilivyotokea kwa SSH, bali hata kusuka mpango wa kukaa madarakani for good kama mwelekeo wa JPM ulivyokuwa. Kwa kifupi, kwa katiba hii, Watanzania wote hata makada, wanachama na mashabiki wa CCM, wanaishi kwa kutegemea fadhila na huruma ya Rais.
Ni Rais wa awamu ya kwanza pekee, JKN, ndio hakuwa na tamaa; alihakikisha maslahi ya wananchi yanawekwa mbele. Alikuwa dikteta kweli; alibana uhuru wa kisiasa, mawazo mbadala na habari lakini kwenye maendeleo ya watu na vita dhidi ya ufisadi, alikuwa genuine. A benevolent dictator. Alisacrifice. Kosa lake kuu (legacy) alituachia hii katiba ya hatari sana.
Sasa kama tunaamini katika kuishi kama Taifa kwa imani kwa serikali hii na kuliona suala la katiba ni kwa “maslahi ya CHADEMA” tu, so well and good. Hatutaki kujiuliza kwa nini CCM na Serikali ya SSH wameamua kulikimbia suala hilo kwa kisingizio cha kutaka “kurekebisha mambo” ambayo majuzi tu JPM alidai “ananyosha nchi”?
Katika hali ya kawaida kabisa, baada ya kashkash za JPM zilizofanya wengi wadai kwamba “nchi sasa inapumua; mama anaupiga mwingi“, ilikuwa dhahiri sana kwamba pamoja na hatua za dharura kurekebisha mambo, Mh. SSH angeamua kwa dhati kuwa analipa suala la katiba mpya priority.
Naamini wengi tunakubali kuwa majuzi tu tumetoka kuepuka hatari kubwa sana iliyotukabili kama taifa kwa kutegemea kuishi kwa huruma ya Rais anayekuwa madarakani. Hivyo ni budi sasa kuchukua hatua za dhati kuepuka kurudia hatari ile. Kama alivyofanya kwa Covid-19, Rais angeunda kamati ya kuandaa utaratibu na ratiba ya kushughulikia suala hilo badala ya kuwaachia “hotheads” wa CHADEMA.
Ni juu yetu kuuona na kukubali au kuupuuza ukweli huu. Wenye hekima wanasema:
Those who cannot learn from history are doomed to repeat it. Na,
Choices have consequences.