Mwanza: Polisi wauzingira Ukumbi litakapofanyika Kongamano la Katiba Mpya

Mwanza: Polisi wauzingira Ukumbi litakapofanyika Kongamano la Katiba Mpya

Kumbe ndio maana brother aliwahi kuniambia nikiwa mdogo kuwa kazi za kiaskari ni za watu wasio na akili sawasawa.
Ni za watu wasioweza kuamua, kazi yao kubwa ni kusubiri amri tu.
lakini hakukwambia kama kuna kazi unaweza kujiamulia cha kufanya.

kama aliitaja hata moja tu alikudanganya, haipo.
 
nyoosha hao wapuuzi wasio na kazi za kufanya tena akisogea mtu vunja kiuno tutamuombea kwa Mungu ampumzishe mahari pema peponi amina

Mbona hamkumuombea Jiwe apone acheni kujipendekeza kwa watawala..
 
Dunia na vyote vijazavyo ni mali ya BWANA, ccm mkilijua hili mtaacha kulazimisha kutawala watu ambao hamjawaumba.

Otherwise mkiamua kuendelea kutumia mabavu kutawala kila kitu, mwenye mali atawanyamazisha

Ondokeni hapo kitangiri mtuache tufanye shughuli zetu.
 
Kweli rais alisema Mimi na magufuli ni kitu kimoja je tulimwelewa au la?
Labba Nina swali kwenu Wana jf.kama anatoa amri kwa haya yanayoendelea kuzuia shughuli za kisiasa Sasa anaongoza nchi kwa katiba gani aliyoapia kuilinda?mbona tayari hapa anavunja haki za watu.
Si mnasema katiba ya sasa tuliyonayo ni ya hovyo kuliko hata ile ya shetani: sasa mbona mkibinywa kidogo tu hamchelewi kulia kwamba anayewabinya anakiuka katiba aliyoapa kuilinda? Halafu kama aliapa kuilinda, hamuoni kwamba ni ujuha kumwambia kwamba aitupilie mbali katiba hiyo (mnaiita ya Msekwa) na kuweka nyingine mnayoiita mpya aka ya Waroba aka ya Lissu/Mbowe? Utakitupaje kitu ulichoapa kukilinda na kukitekeleza? Kwa nini msisubiri hadi mtakapochukua dola ndiyo mtuletee hiyo katiba yenu mpya? Yaani kwa akili yenu mnaamini kwamba ccm wata 'install' hiyo katiba yenu mpya mnayoidai kwa kuwapigia makelele na kuwavyalia manguo mekundu na kutishia kuingia mitaani kufanya vurugu? Hilo haliwezekani, sana sana mtaishia kupasuliwa ngeo. Please come back to your senses.
 
View attachment 1861973

Askari Polisi waliojihami kwa silaha za moto na mabomu ya kutoa machozi wamezingira na kufunga njia za kuingia na kutoka Hoteli ya Tourist eneo la Kitangiri jijini Mwanza ambako Kongamano la Katiba Mpya lililoandaliwa na CHADEMA lilitarajiwa kufanyika leo.

Kuna zaidi ya askari polisi 200.
View attachment 1861973View attachment 1861981View attachment 1861982View attachment 1861983View attachment 1861984
Wangepeleka moja Kariakoo!
 
Katiba ya nchi haidaiwi kwa makongamano ya chama fulani kimoja kwa masilahi yake huku wakiwa wamevaa yunifomu nyekundu. Kuvaa nguo nyekundu wanashiria wako tayari kumwaga damu za watanzania ili kutimiza lengo lao hilo. Waanze kwanza wao kumwaga damu zao. Polisi wanawasubiri hapo Turist Hotel kuwasaidia kumwaga hizo damu zao. Tunatumaini watajitokeza.
LEO NDIO NIMEFAHAMU UKIVAA NGUO NYEKUNDU UNA NIA YA KUMWAGA DAMU..AISEE,valentine sivai tena red,NITAWASHAURI LIVERPOOL WAVAE NYEUSI
 
Hahahaha yaani ukiwa akili ya kipolisi pole yako....kama robot vile
Nimependa sana utulivu wa watu wa Mwanza, wapo busy na mambo yao wanaendelea na shughuli zao na ratiba zao za Sikukuu, kujitafutia Riziki na wengine wapo wanakunywa Bia! Watu wa Mwanza wamechagua Amani, utulivu na usalama wa Taifa lao Mama Tanzania!
 
Ni lini Makongamano yamekuwa dhambi? Busara zitumike na sio maguvu.
Rais alishatoa msimamo kuhusu hiyo propaganda ya katiba mpya. Kinachoendelea na kukiuka maagizo Hali ya Rais na wakaidi lazima washughulikiwe
 
Back
Top Bottom