Hivi mtoto wa mtu asipoenda kirumba watamfanyaje ?, mimi nafikiri hawa wanafunzi wafike mahala wajitambue, unaacha kwenda unakaa nyumbani unapumzika ni muda mzuri wa kuangalia tamthilia, kule mkoani kagera mwaka 2015 kuna wanafunzi fulani shule moja ya sekondari walikataa kufanya kazi ya kutengeneza kura hewa kama ambavyo walikuwa wameagizwa na mkurugenzi wa eneo hilo, na wakaenda mbali zaidi kwa kuzitupa zile karatasi za kupigia kura walizokuwa wamepewa na wakawaambia waandishi wa habari, hao ndio aina ya wanafunzi wanaotakiwa kwa zama hizi.