JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Watumishi hao waliandamana jioni ya Aprili 8, 2022 ambapo malipo hayo ni Sh 100,000 kwa siku tano ambapo kila siku malipo yalikuwa ni Sh 20,000 kwa mtu mmoja.
Akizungumzia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel alisema atawasiliana na viongozi wa mradi huo na viongozi wa kata kisha atatoa taarifa kwa walimu hao kuhusu malipo yao.
“Wanatufokea, wanatutukana, sisi ni watumishi wa umma, sasa hivi wanaanza kutuzungusha kuwa tutalipwa kwa kaya kitu ambacho ni tofauti na makubaliano yetu,” alisema mmoja wa waandamanaji hao.
Chanzo: Nipashe