Mkunazi Njiwa
JF-Expert Member
- Apr 22, 2023
- 8,538
- 7,559
[emoji1787][emoji1787]Hao majini hutumia mawimbi kuwapotosha watu wabishi kama wewe kuendelea na ujinga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji1787][emoji1787]Hao majini hutumia mawimbi kuwapotosha watu wabishi kama wewe kuendelea na ujinga
Msomi wa chuo mwaka wa 3 na kuogelea ziwani kuna uhusiano gani mkuu?Yaani msomi wa Chuo tena wa mwaka wa 3 anaenda kuogelea ziwani?????
Hizi Elimu za kukariri sijui zinatusaidia nin
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Wewe binafsi si unaamini kuna kiumbe cha kufikirika kinaitwa jini? It’s so sad jinsi udini ulivyofunika ufahamu wako . Isingekuwa udini una akili nzuri sana tu
...Ina maana mmoja alitaka kumuokpa mwenzie aliyekuwa anazama?? Ilikuwaje Mapacha Wawili wanaojua kuogelea Wakafa Wote Kwa Pamoja??Sasa nini kiliwaua akati wanajua kuogelea???
Mkuu umeshawahi kuvua?!!!Kwahiyo yake mawimbi tunayoyaona ni majini? Kweli sijaona mwisho wa ujinga km nilivyodhani. Nchi hii kuna watu ni wajinga mpaka mnashangaza na kuacha rekodi.
Havoc[emoji22]Dah imagine wewe ndio mshua uneletewa taarifa za majembe yako mapacha wawili hawapo tena ulimwengu huu.
Aiseee nimeumia sana hapa na ninavyopenda mapacha sasa.
Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
Huyo "mbubu" anaendelea kujifunza ya duniani....Imani potofu kivipi wakati hao chunusi/majini nao ni viumbe?
Kwani haujui kuwa Mungu aliumba vinavyoonekana na visivyoonekana?
Wenzake tunayatumia katika kupata pesa na maisha yanaendelea....aendelee kuatamia ufukara tu....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Ungeelewa Maana ya neno jinni kwa Kiswahili usingapata tabu kukijuwa.
TerribleUkweli ndio huu hapa kwa sisi wataalam wa maji.
Kuna mwaka alikufa jamaa wa TPDC hakuna aliye amini yule jamaa alikuwa hadi anashiriki nashindano ya kuogelea
[emoji106]Japo pengine watu watakimbilia ushirikina lakini pengine hiki ndicho kilichotokea.
Kwa vile wote ni waogeleaji wazuri pengine walikuwa wameshaogelea kwa muda mrefu. Inawezekana mmoja alipata tatizo la misuli kukaza na akaanza kuzama. Mwenzake alipoona pacha wake anazama akaenda kumwokoa bila kuchukua tahadhari. Kwa sababu ya panic huyu aliyekuwa anazama akamrukia mwokoaji kwa namna ambayo hakuweza kuogelea tena na wote wakaishia kuzama.
Ni hatari sana kumwokoa mtu anayezama maana anakuwa tayari katika panic mode na anaweza akakung'ang'ania hata mikono ambayo ndiyo unaihitaji sana katika kuogelea. Mtu anayezama inabidi umshike kwa mbali tena kwa mkono mmoja tu halafu umvute huku wewe ukiogelea. Ukijichanganya tu ukamsogelea kuna hatari ya wote kufa. Hapo lazima kuna mmoja amekufa akijaribu kuokoa maisha ya mwenzake.
Na hili tatizo la misuli kukaza aisee linashangaza sana maana hata mimi lilishawahi nitokea. Mimi ni mwogeleaji mzuri tu mpaka wa maji yanayotembea. Nimechukua pia darasa la kuogelea kabisa ili kujifunza jinsi ya kubakia juu ya maji bila kutumia nguvu nyingi.
Sasa siku moja nilikuwa naogelea katika bwawa kubwa la hoteli moja iitwayo Omni Resorts kule Orlando, Florida. Nilikuwa nimeogelea kwa zaidi ya masaa mawili na kilichokuwa kimenibakiza pale ni kwamba kulikuwa na mishangazi ya uhakika kibao myeusi na mizungu ipo kwenye bikini tu inajibinua. Basi nikajikuta nimefurahia kutazama ile misambwanda ya kufa mtu huku nasukumizia na chicken wings za hapa na pale. Na mingine tukawa tumezoeana zoeana mpaka tunapiga na vistori vya hapa na pale.
Basi bana baada ya kukaa kwenye kijua kwa muda kwenye hivi viti vya kulaza hivi nikajitosa kule kwenye kina kirefu (futi 12). Eeee bana eeeh!
Najaribu kuogelea hivi hakuna kinachojongea. Misuli imekaza mikono na miguu haisogei. Kengele ya tahadhari ikalia kuwa haki ya nani kuna hatari ya ngosha kufia kwenye pool leo. Na mijimama yote hii dah! Aibu iliyoje!
Nikajaribu tena lakini nikakuta hakuna kinachojongea na hapo tayari nshapiga vikombe kadhaa vikubwa tu. Bahati nzuri sana karibu yangu kidogo kulikuwa na familia ya kizungu inaogelea na mtoto mmoja tineja aliniona akamwambia babake "I think he is drowning". Yule baba alimwita mhudumu mmoja aliyekuwa karibu hapo wana haya mafimbo marefu mwisho yana kama kikofia nchani huwa wanayatumia kuondolea uchafu unaoelea kwenye pool akaninyoshea nikadaka lile lifimbo macho yamenitoka hatari nahema balaa. Wakanivuta nikatoka nje.
Kwa vile nilikuwa nimeogelea pale kwa muda mrefu yule mfanyakazi akawa ananiuliza "What happened?" Nikamwambia I just can't move my hands and legs...Oooh muscle issues. It happens sometimes. Mpaka leo huwa nawaza ningekuwa peke yangu siku ile sijui ingekuwaje [emoji15]
Tangu hapo nikisikia mwogeleaji mzuri amezama wala huwa sishangai. Na baadaye niliambiwa kuwa tatizo hilo linaweza kusababishwa na upungufu wa madini ya Magnesium mwilini na au sehemu fulani ya misuli kukosa hewa ya Oksijeni kwa ghafla. Inapaswa kuwa hydrated pia maana ukiwa dehydrated misuli inaweza kukugomea wakati wo wote. Ulaji wa chungwa moja au mawili pamoja na ndizi pia unasaidia kuzuia tatizo hilo. Wacheza soka na michezo mingine pia wanalijua tatizo hili na sijui huwa wanatumia mbinu gani kulizuia.
[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Vijana wadogo tu masikini maisha yao yamekatizwa. Wapumzike salama [emoji1545]
We jamaa umelewa kangara ama ?!!! [emoji1787][emoji1787]Wazazi wangekua wanawatenganisha hawa watoto. Mmoja akasome UDSM mwingine Mwanza.
Bora hasara nusu.
Mtume tena ?!!!!hao majini wa maji mtume amewahi kuwazungumzia popote bibi?
Umelewa smart gin ?!!! [emoji1787][emoji1787]Yaani msomi wa Chuo tena wa mwaka wa 3 anaenda kuogelea ziwani?????
Hizi Elimu za kukariri sijui zinatusaidia nini
Exquisite [emoji7]Kuna samaki anaitwa mkunga kwa kiingereza electric eel.
Huyu samaki ana uwezo wa kukupiga shoti.
Inaaminiwa wengi wanaopotea baharini na kwenye maziwa yawezekana walipigwa shoti na mkunga wakapatwa na stroke au cardiac arrest na kuzama.
Nimeona nondo zako kali hapo juu na boti yako ya uvuvi. Naogopa hata kujibishana nawe namhala.[emoji106]
Ngosha wa Orlando Florida huyoooo.....
Yashilagga guukuuu [emoji1787]
Hii comment imenizungumzia kabisa. Huwa sitaki kabisa mazoea na man WATERR.i.p hakika ni pigo kubwa.
Nikienda kutuliza akili beach uwa naishia maji ya ugoko tu sitaki mazoea na maji