Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Barabara inapojengwa msanifu huweka kitu kinaitwa Road shoulders

Kazi ya shoulders ni kufanya watembea Kwa miguu kupita pamoja na makundi ya wenye uhitaji maalumu

Sasa hivi shoulders zinatumika vibaya na viongozi wanaangalia tuu humo utakuta ndio sehemu ya Jogging, machinga kupanga vitu chini, pamoja na parking za magari Kwa baadhi ya sehemu mfano msimbazi road nk
Najiuliza swali je dereva akikosea hapo wa kulaumiwa ni serikali, au dereva?
Tuchukue hatua kabla ya kuanza kulalamika

R I P wote mliopoteza maisha Mungu awapokee salama muendako
 
Mfano ile barabara ya Morogoro kutoka komoa hadi Masika mzigo una sehemu ya magari watembea kwa mguu na waendesha baiskeli ila bado kuna mbwa zinapita na bodaboda huu upande wa watembea kwa miguu trafiki wakamate uso dog mara moja please
 
...Inaelekea Njemba alikuwa Kasi Sana! Mpaka vyuma vya gari vimepinda hivyo Kwa kugonga TU Watu ??[emoji26]
RIP Marehemu na Poleni Sana Wafiwa..
 
Juzi kati nipo maeneo ya redstone-moshi (saa 12 asubuh) zile basi za mikoani zilichonifanya pamoja na lile roli dah kweli Mungu bado ananipenda. na kiherehere cha kukmbia ile rod kiliisha sku ile ile
 
hivi hawa walikuwa wanakimbia katikati ya bara bara au?? sema barabara za bongo zimebana mnooo yanii watembea kwa miguu hakuna nafasii kabisaa so jamaa itakuwa alikuwa mwendo wa ngirii alafu hawa jamaa wanatabia ya mmoja anatangulia mbele na kibendera chekundu sasa haitoshi aiseee... jogging za makundi bongo ni risk mnoo
 
ninatoa pole za dhati kwa wanamazoez wenzetu,Mungu afanyike faraja kwa familia [emoji120]

Ajali zingne hazina kinga,tuwe waangalifu tunapokua barabaran,maderava wengi sio watu makini,zile kaz znachosha na kuvuruga akili
 
Tuna maeneo mengi ya kukimbia na kufanyia mazeoezi mbali na barabara mkuu.
Basi na tuendelee kukimbia katikati ya barabara sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…