KERO Mwanza Yageuzwa Jangwa: Wiki ya Tatu Bila Maji, Viongozi Wanaendelea na Siasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

tausi2020

Member
Joined
Jul 5, 2025
Posts
67
Reaction score
94
Ukweli Mchungu

Viongozi wa mkoa wa Mwanza wanaendelea kukwepa ukweli na kugeuza hali ya maji kuwa siasa.

Tayari ni takriban wiki ya tatu sasa jiji la Mwanza linakumbwa na ukosefu mkubwa wa maji. Hivi karibuni mkuu wa mkoa alitangaza wazi kwamba marekebisho yamekamilika—lakini hali halisi kwa wananchi ni tofauti kabisa.

Maeneo mengi kama Nyegezi stendi, Kumalija, Majengo, na Mkolani (eneo la Elly Hotel) bado yanakabiliwa na shida kubwa. Maji yakitoka, yanakuja kwa kasi ndogo mno na huishia maeneo ya mwanzo pekee, huku wananchi wengi wakikosa kabisa huduma hii ya msingi.

Kibaya zaidi, hata kabla ya mgao huu, maeneo mengi ya Mwanza yalikuwa yakipata maji mara mbili tu kwa wiki—siku ya Jumatatu na Ijumaa. Hiyo ni katikati ya jiji! Je, hali ikoje maeneo ya pembezoni?


Kila mara tatizo likijitokeza kisingizio ni mitambo au umeme. Hii imekuwa kama kasumba ya kila mwezi. Swali la msingi: kwanini hakuna suluhisho la kudumu? Mwanza imetelekezwa kwa shida hii ya maji au viongozi hawana dhamira ya kweli kutatua tatizo?


Ama kweli, wananchi wanaumia kimya kimya huku kauli za kisiasa zikichukua nafasi ya vitendo.
 

Attachments

  • IMG_2165.jpeg
    287.4 KB · Views: 28
Nawapasulia ukweli wa MWAUWASA:
Kuna ka mradi kao Ka kuuza maji, unapiga simu wankuletea na boozer zao zenye namba DFP, kutegemea na umeongeaje ila gari moja ni sh.300,000/ wateja ni wafugaji, wenye mahotel NK. Ukilipa hakuna control number wala risiti! Mtumishi gani aruhusu mabomba yote maji au afanye biashara ya kuuza maji!

Kuna tetesi ule Mradi wa maji Mama alizindua majuzi mabomba yaliyotandazwa chini yanafukuliwa na kuuzwa na watumishi wa idara ya maji....mnunuzi ana kiwanda cha mabomba anayayeusha na kutengeneza mengine (low quality) ya serikali yaliwekwa enzi za Magufuli yalikuwa ya ubora WA Hali ya juu!

Dawa za kutibu maji mfano Chlorine, NK ni dili Sana nchi jirani, watumishi wanayachepusha KULINGANA NA UREFU WA KAMBA ZAO...hili ninao uthibitisho, ila mwanajeria wangu kasema hawezi kutetea maiti!

Hii nchi kwa uongozi huu kufika 2030 itakuwa duni zaidi ya wakati tumemaliza vita vya Kagera!
Mitano tena!
 
Hii nchi ili raia wengi kuzinduka inabidi tufike hiyo 2030
 
Wizi, kujiongezea matatatizo na kulalamika ndio akili ya mtu mweusi, inasikitisha sana
 
Na KURA/KULA MTAWAPA!
WADANGANYIKA SHIDA...
 
hii inaweza kua na ukwel ndani yake maana kwel hayo magar tunayaona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…