Jamani, na mimi nipo hapa Mwanza, japo kutokana na majukumj, nahisi sitahudhuria mpaka mwisho wa mkutano maana ni lazima nisafiri. Hata hivyo, dakika 15 zijazo nitaelekea viwanja vya Furahisha kuona maandalizi yanavyokwenda.
Huu ni zaidi ya mkutano. Ni mwanzo mpya, ni ujumbe tosha kuwa tulipotoka, sasa tuna dhamira ya kwenda kwenye ustaarabu wa kuheshimu katiba, kulinda uhuru wa maoni na haki za watu. Hamasa haitokani tu na ujumbe utakaotolewa na viongozi wa CHADEMA bali ni kuwaambia watawala kuwa sisi wananchi tunawataka watawala waheshimu katiba na sheria.