MWAUWASA: Eneo la Mahina lilikuwa na changamoto ya maji lakini hatua zimeshaanza kuchukuliwa

MWAUWASA: Eneo la Mahina lilikuwa na changamoto ya maji lakini hatua zimeshaanza kuchukuliwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imetoa mrejesho kuhusu hoja ya Mdau aliyeandika ~ Watu wa Mahina - Mwanza, Waziri akija maji yanatoka, akiondoka nayo yanaondoka.

MWAUWASA:

Tunapenda kufafanua kuhusu changamoto iliyowasilishwa ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa eneo la Mahina, ni kweli eneo hilo lilikuwa na changamoto ya kuzidiwa kwa miundombinu ya maji iliyowepo awali kutokana na ongezeko la idadi ya wakazi, hata hivyo hadi sasa hatua zimekwisha chukuliwa na Mamlaka imetekeleza mradi mdogo wa dharura wa kuboresha mfumo wa usambazaji maji katika eneo hilo.

Mradi umeleta matokeo na huduma imeimarika kwenye baadhi ya maeneo kuliko kamilika maboresho na maeneo mengine yanaendelea kufikiwa kwakuwa kazi inaendelea na mafundi wapo "site" .

NB: Changamoto nyingine tuliyokuwa tukiipata ni wananchi kuingilia mfumo wa usambazaji maji kwa kufungua na kufunga valves bila utaratibu uliopangwa, hilo nalo tumelifanyia kazi na huduma imeendelea kuimarika.
 
Back
Top Bottom