Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA):
Tunapenda kueleza kuwa hali ya huduma ya maji katika eneo la Kanda ya Nyegezi imerejea kwenye hali ya kawaida, isipokuwa kwa kipindi cha siku kadhaa kati ya tarehe 13 hadi 20 Oktoba 2026.
Kulikuwa na changamoto ya uzalishaji maji kutokana na hitilafu ya bomba kuu la kusafirisha maji kutoka chanzo cha Butimba kwenye Tenki la Nyegezi ambalo ndilo huhudumia maeneo hayo ya Ukanda wa Nyegezi kama taarifa zetu rasmi za tarehe hizo zilivyoeleza.