MWAUWASA: Maeneo ya Milimani Mwanza hukumbwa na upungufu wa maji kutokana na msukumo mdogo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Mtaa wa Kaseze, Kata ya Mkolani, Wilaya ya Nyamagana aliandika ~ Mwanza: Mtaa wa Kaseze, Nyamagana hatuna maji, badhi ya Wananchi wanajisaidia vichakani, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imepa majibu Mwananchi huyo.
=========================​

Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkolani

Eneo la Mkolani linapata huduma ya maji kwa kiwango cha kuridhisha, isipokuwa kunapojitokeza changamoto kama kukatika kwa umeme kwenye chanzo cha maji/Vituo vya kusukuma maji au matengenezo ya Miundombinu.

Maeneo ya milimani hukumbwa na upungufu wa maji kutokana na msukumo mdogo, MWAUWASA imeweka utaratibu wa mgao wa maji kwa maeneo hayo, kuhakikisha wanapata huduma angalau mara tatu kwa wiki. Wananchi pia wanahimizwa kuhifadhi maji kwa matumizi wakati wa upungufu.

Kwa upande wa Usafi wa Mazingira, MWAUWASA kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa, inaendelea kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora ili kuzuia utiririshaji wa majitaka ovyo.

Kuhusu miundombinu ya majitaka, MWAUWASA inaendelea kutekeleza miradi ya ukusanyaji wa majitaka hatua kwa hatua kwenye maeneo ya milimani, ingawa Mkolani haina mtandao rasmi wa Uondoaji majitaka, huduma ya magari ya kunyonya inapatikana kwa gharama nafuu.

Kitengo cha Mawasiliano MWAUWASA
 
Mwauwasa washakua wanasiasa hao mkolani hapo maji mgao pro max na hawana sababu yoyote ya maji kua na mgao hv inaingia akili maji kutoka mwanza yanatumika kahama tabora nahayataktiki ila mwanza humu humu kuna mgao na istoshe rais samia amefungua mradi mkubwa mkuyuni wa maji akasema tatizo la maji bye bye leo upuuz gan huo wanasemaje.Swala la maji n crosscutting issue sio mkolan tu n sehem kubwa mwanza maji n shida mjini ndo maji ya uhakika lazm waziri wa maji awawajibishe Mwauwasa its too much maana viongozi mkoa huu wanajisahau sna
 
Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Mtaa wa Kaseze, Kata ya Mkolani, Wilaya ya Nyamagana aliandika ~ Mwanza: Mtaa wa Kaseze, Nyamagana hatuna maji, badhi ya Wananchi wanajisaidia vichakani, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imepa majibu Mwananchi huyo.
=========================​

Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkolani

Eneo la Mkolani linapata huduma ya maji kwa kiwango cha kuridhisha, isipokuwa kunapojitokeza changamoto kama kukatika kwa umeme kwenye chanzo cha maji/Vituo vya kusukuma maji au matengenezo ya Miundombinu.

Maeneo ya milimani hukumbwa na upungufu wa maji kutokana na msukumo mdogo, MWAUWASA imeweka utaratibu wa mgao wa maji kwa maeneo hayo, kuhakikisha wanapata huduma angalau mara tatu kwa wiki. Wananchi pia wanahimizwa kuhifadhi maji kwa matumizi wakati wa upungufu.

Kwa upande wa Usafi wa Mazingira, MWAUWASA kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa, inaendelea kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora ili kuzuia utiririshaji wa majitaka ovyo.

Kuhusu miundombinu ya majitaka, MWAUWASA inaendelea kutekeleza miradi ya ukusanyaji wa majitaka hatua kwa hatua kwenye maeneo ya milimani, ingawa Mkolani haina mtandao rasmi wa Uondoaji majitaka, huduma ya magari ya kunyonya inapatikana kwa gharama nafuu.

Kitengo cha Mawasiliano MWAUWASA
Ninyi MWAUWASA mmekuwa na kiburi sugu – hamfanyi kazi ipasavyo! Kila siku visingizio: mara “umeme hauko stable”, mara “Mwanza iko milimani”.

Kama mliona mlima ni tatizo, si mhame Mwanza? Waje wanaoweza kuwahudumia hata walio milimani!

Leo ni mwezi wa pili sasa – maeneo mengi hayana maji kabisa, halafu bado mnakuja na “fix” zisizo na maana. Acheni kabisa tabia hii ya kuonea watu!

Mfano halisi ni Nyegezi
– mitaa mingi hapa mjini maji hakuna kabisa. Halafu bado mnatuona kama watu wajinga?

Sasa TANESCO wenyewe wamesema kutakuwa na matengenezo mwezi wa nane – je, kwa hali hiyo, watu wa Mwanza maji wataanza kupata baada ya miezi mitatu?
Hii maana yake nini? Kwamba mateso ya wananchi yataendelea hadi lini?

Niwakumbushe kitu kimoja muhimu:
Sasa hivi nchi hii ina wasomi wengi. Msitudharau na kutufanya wajinga wote.
 
Mdau wa JamiiForums.com aliyejitambulisha kuwa Mkazi wa Mtaa wa Kaseze, Kata ya Mkolani, Wilaya ya Nyamagana aliandika ~ Mwanza: Mtaa wa Kaseze, Nyamagana hatuna maji, badhi ya Wananchi wanajisaidia vichakani, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imepa majibu Mwananchi huyo.
=========================​

Huduma ya Maji na Usafi wa Mazingira Mkolani

Eneo la Mkolani linapata huduma ya maji kwa kiwango cha kuridhisha, isipokuwa kunapojitokeza changamoto kama kukatika kwa umeme kwenye chanzo cha maji/Vituo vya kusukuma maji au matengenezo ya Miundombinu.

Maeneo ya milimani hukumbwa na upungufu wa maji kutokana na msukumo mdogo, MWAUWASA imeweka utaratibu wa mgao wa maji kwa maeneo hayo, kuhakikisha wanapata huduma angalau mara tatu kwa wiki. Wananchi pia wanahimizwa kuhifadhi maji kwa matumizi wakati wa upungufu.

Kwa upande wa Usafi wa Mazingira, MWAUWASA kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa, inaendelea kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora ili kuzuia utiririshaji wa majitaka ovyo.

Kuhusu miundombinu ya majitaka, MWAUWASA inaendelea kutekeleza miradi ya ukusanyaji wa majitaka hatua kwa hatua kwenye maeneo ya milimani, ingawa Mkolani haina mtandao rasmi wa Uondoaji majitaka, huduma ya magari ya kunyonya inapatikana kwa gharama nafuu.

Kitengo cha Mawasiliano MWAUWASA
Hujyu hata aibu aibu hana mwauwasa umesomea nini? Unasema eti milimani? Msukumo mdogo? Ziwa liko wapi?

Alafu hii tabia ya kusingizia tanesco muache tanesco wanajitahidi sana msitake kufa nao.

Uoni aibu kusema walau mara tatu? Iundwe timu izunguke maeneo ya nyegeze na mitaa yake na mkolani hadi buhongwa mostly maji mnatoa mara 02 kwa wiki na yenyewe ikitokea shida yoyote imepita.

Kua na aibu unalipwa na hao wananchi wanao kaa milimani na sehemu nyingine.

Umesoma mambo ya maji kama unaona ni shida kuhudumia acheni kazi waje wengine wahudumie
Majibu yako ni kejeli na dharau kwa wakazi wa mwanza.

Aibu iwe juu yako
 
Back
Top Bottom