MWAUWASA: Tumeandaa Mradi wa Tsh. Bilioni 8.4 kufikisha Huduma ya Maji maeneo ya Kishiri na jirani ambayo hayana huduma hiyo

 MWAUWASA: Tumeandaa Mradi wa Tsh. Bilioni 8.4 kufikisha Huduma ya Maji maeneo ya Kishiri na jirani ambayo hayana huduma hiyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kuelezea kuhusu changamoto ya huduma ya maji iliyopo katika Kata ya Kishiri, ufafanuzi wa Mamlaka ya Maji Mwanza umetolewa.

Kujua alichokisema Mdau huyo unaweza kubofya hapa ~ Changamoto ya maji Kanindo Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana

==== ====
Neli Msuya, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) anasema:

"Ili kuweza kufikia eneo la Kishiri ambalo halijafikiwa na huduma ya maji, MWAUWASA imeandaa mradi kabambe wa thamani ya shilingi bilioni 8.4 ili kuweza kujenga mfumo wa maji.

"Maeneo yatakayonufaika ni pamoja na Kishiri, Mahina, Ipuli, Nyangulugulu, Kagua, Busekwa na maeneo yote ya jirani.

"Mradi huu utagharamiwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka mfuko wa Taifa wa Maji na Bank ya TIB, na fedha zinategemewa kutoka Oktoba 2024."

"Kupitia mradi huu zaidi ya maunganisho 5000 yatafanyika ili kufikia wananchi wa maeneo husika."

d1d611de-d8a7-44b8-be75-de72d1fe633f.jpg

Hali ilivyo maeneo ya Kishiri
 
MWAUWASA TUNAOMBA MTUREJESHEE MAJI KISHIRI A" MABOMBA MMEFUKIA MAJI HAKUNA. MCHINA AMESHA MALIZA KUSHINDILIA BARABARA.


AU WAZIRI WA MAJI NDO ATA TUREJESHEA HUDUMA?
 
Back
Top Bottom