MWAUWASA: Tunafahamu changamoto ya Maji katika baadhi ya maeneo Nyegezi, tunaifanyia kazi

MWAUWASA: Tunafahamu changamoto ya Maji katika baadhi ya maeneo Nyegezi, tunaifanyia kazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Kufuatia andiko la Mwanachama wa JamiiForums.com kuhusu huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ya Nyegezi Jijini Mwanza kudaiwa kuwa ni duni, kisha kuitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) ijitafakari kwa kuwa inawakwamisha Wananchi wengi wa maeneo hayo, Mamlaka hiyo imeelezea kinachoendelea.

Kusoma kilichoandikwa na Mwanachama bofya hapa ~ Idara ya maji Nyegezi Mwanza (Mwauwasa) jitafakarini suala la ukosefu wa maji

Akifafanua kuhusu hali ya huduma Nyegezi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa MWAUWASA, Vivien Temu anasema:

Siku za nyuma kulikuwa na changamoto ya maji upande wa Nyegezi kwa kuwa tulikuwa tunategemea chanzo kimoja cha Capri Pointi, kwa sasa tuna chanzo kingine cha Butimba ambacho kinapeleka huduma pia maeneo hayo ya Nyegezi.

Kuna maeneo ambayo yana changamoto ya usambazaji, miundombinu iliyopo kwa sasa ni chakavu na haikidhi mahitaji ya watu, maeneo hay oni Nyakagwe, Kigoto na Luchelele.

Tayari kuna mradi mkubwa ambao umeshapangwa kufanyika, Mkandarasi ameanza kazi ya kuchimba akianzia Luchelele, akitoka hapo ataelekea Kigoto kisha kumalizia Nyakagwe.

Tumeshazungumza na Mkandarasi agawanye watu wake maeneo tofauti ili kazi iende kwa kasi.

Kwa hiyo kwa ufupi ni kuwa maeneo yenye changamoto ni hayo ambayo tuna taarifa zao na tayari MWAUWASA imeshachukua hatua kukabiliana na changamoto hizo.

Pia itambulike wazi kuwa sio kwamba hawapati huduma ya maji moja kwa moja, wanapata mwa mgawo wakati utaratibu mwingine ukiendelea.

Pia soma ~
MWAUWASA: Tunafahamu changamoto ya Maji katika baadhi ya maeneo Nyegezi, tunaifanyia kazi
 
Back
Top Bottom