Mwelekeo wa Ndoa yangu umefikia pabaya sana

Mwelekeo wa Ndoa yangu umefikia pabaya sana

incredible terminator

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2016
Posts
2,498
Reaction score
4,162
HABARI wakuu, kwanza kabla ya yote niwatakieni mfungo mwema.

Umri wangu ni Miaka 33, Nipo katika ndoa pia nina Watoto Wawili na huyu mwanamke, naona nisiandike Mengi kuhusu maisha yangu na huyu Mwanamke ila kimsingi tu ni MTU ambae ninapitia changamoto nyingi sana katika mahusiano haya, yaani kiufupi tu hata sielewi mwelekeo wa ndoa hii, Tulikutana nae tukachukuana nae Tukaamua kuishi pamoja hadi sasa tuna watoto wawili, lakini sijamtolea mahali, lakini sio kwamba sina uwezo wa kutoa mahali ila kinachonichelewesha ni aina ya maisha ambayo tunaishi nae.

Yaani siku za furaha ni za kuhesebakika kuliko siku za kununiana, ana vijisababu visivyokuwa na mashiko anajinunisha, Mara utastuka usiku unamkuta MTU amekaa kitandani analia bila sababu, Mara atoke akae jikoni usiku, Mara ajidai amepandisha presha nianze kumpepea usiku yaani ni mateso bila ya kifo.

Kimaisha siko vibaya ninamtimizia kila hitaji pia ninakaa kwangu sijapanga na Mimi ni mtu wa kutoka asububi narudi jioni kutokana na aina ya harakati zangu zinazoniweka mjini, sasa kulitokea kasumba Kikitokea kimgogoro kidogo ananinyima unyumba, hadi inafkia mda unazuka ugomvi ndo napewa huwa nawaza namna ya kuachana nae, ila nawaonea huruma sana wanangu, pia hata yy namuonea huruma, maana nishamzalisha watoto Wawili wote alafu nimuache huwa kimsingi naishi nae kwa sababu ya huruma, pia kwa sababu ya kuwaonea huruma wanangu nilitamani wanangu walelewe na wazazi wao ila mwelekeo wa Maisha haya sijajua hatima.

Tangu mwezi wa Pili kuna shida ilitokea nikawa nanyimwa unyumba hadi ikafikia hatua nikakosa namna ikabidi nianzishe uhusiano na mtu mwingine ila kibaya nilianzisha kama njia ya kumaliza haja zangu nikirudi nyumbani najilalia zangu maana sikutaka ugomvi wa kutaka mbususu kwa wife ila kibaya naona nimezama mazima yani huyu mtoto anajua kucare, anajali kiufupi ninapata kila kitu ambacho nilikuwa nakosa awali, lakini kibaya zaidi na bahati mbaya kwa sasa huyu Mtoto ana ujauzito wangu, hapa nipo njia panda.

Kusema kweli ingekuwa uwezo wngu ningemuoa huyu mtoto maana kimsingi mke ninaekaa nae ameshindwa kutambua thaman yangu, lakini kila likija swala la wanangu huwa naishiwa nguvu maana siwezi kuruhusu wanangu kukaa mbali na Mimi pia sina imani kama mwanamke huyu ataishi na wanangu vizuri mda ambao Mimi sipo, kusema kweli najikuta naishi katika majuto niliingiaje 18 za huyu mwanamke! Na ni namna gani nitaepuka hili.

Pia kuhusu suala ya yeye Pengine ana mahusiano mengine siwezi jua na huwa sina asili ya kifuatilia maisha yake maana nipo bize sana na pia huwa sitaki kabisa kufanya kumfuatilia maana matokeo ya kumfuatilia MTU siku zote hayawi mazuri.

Kibaya zaidi ni kuwa jamii tunayoishi nayo inatuona tuko vzuri maana mchana tunaigiziana ila ikifika usiku hakuna MTU anamsogelea mwenzie.

USHAURI WENU MUHIMU
 
Yote tisa kumi tatizo ni wewe, unamzalishaje mtoto wa watu watoto wawili wote hujamtolea mahari. Hakika kilio chake ni majuto ayapatayo. Anatamani nae aonekane mwanamke, ni sahihi unavyombeza. Wanawake na sisi bhana.
 
Mkuu pole Sana Sina Ushauri Ila nadhan kosa ulilifanya kwa kuanzisha mahusiano nje ukidhan unasolve tatizo

Je, ushawasharikisha wazaz au washenga? Au mtu wa kiroho sheikh padri au mchungaji?

Ukijibu haya ntatoa Ushauri
 
Sasa situation uliyojiweka ndio utakoma. Utajuta nakwambia.

Unaona huruma kumuacha mama mtoto wako wa kwanza sababu ana watoto wako 2 na unapenda wanao walelewe na wazazi wote wakiwa pamoja sasa na huyo mpya unaeenda kumzalisha huyo mtoto wako utafanyaje? Utaishi nae?

Oa wote wawili watajiheshimu.

Wanasemaga ukitaka kumuua mbwa unampa jina baya, na ndo unachofanya mkubwa. Wewe lengo lako ni kumuoa huyo mchepuko wako haya ya kusema sijui wife kafanya hiki mara hiki ni kumtafutia chochoro ya kumuacha tu. Hivi we kwa akili yako mkuu unaamini kabisa hayo mahaba anayokuonesha mchepuko wako sasa hivi ndo ataendelea hivyo hivyo hadi milele ukimuoa? Pole sana.

Hata hivyo, yawezekana my wife wako ana stress za kumzalisha watoto na kuishi nae miaka kadhaa bila ndoa

All in all, cheza karata zako vizuri. Umeshafanya kosa kubwa kumpa mchepuko mimba! Hili lijue tu
 
Yote tisa kumi tatizo ni wewe....unamzalishaje mtoto wa watu watoto wawili wote hujamtolea mahari....hakika kilio chake ni majuto ayapatayo ... Anatamani nae aonekane mwanamke...ni sahihi unavyombeza.wanawake na sisi bhana
Nilishasem uwezo wa kupeleka mahali ninao mda wowote ila changamoto aina ya maisha tunayoyaishi ndio hayaridhishi kabisa nakumbuka alishawahi kunipiga na kukimbia na nilivyotaka kumkimbiza kuna wazo likanijia nitaonekana mjinga mbele ya jamii kwa hiyo huwa namwacha, tu ila ni tukio haliwez kufutika kila nikiwaza kumrasimisha kuwa mke wng
 
Pole sana, hayo ndo madhara ya kuchukuana na kuanzia kuishi Moja kwa Moja.

Pole kwa hao watoto maana wao ndo huathirika zaidi na migogoro ya wazazi.

Huyo baby mama wako anaenda attention, inahitaji nguvu ya ziada kumfanya aache hizo tabia za hivyo, ukiwa wale wa kupotezea Bila kumchana ukweli utateseka sana.
 
Umeamua kuchepuka malizia tu haja zako huko huko usilete nyumbani iwe mtoto au ujauzito pili huyo sio mkeo huyo ni hawala tu maana hauna uhalali wowote uwe wa kidini,kiserikali au kimila
Ni sawa ila namna ya kumrasimisha huwa nashindwa nataman nitoe mahari nami nihesabike kama nimeoa ila huyu mwanamke ananipa wakat mgum sana maana kumtolea yy mahari naona kama naingia jehanam kwa macho yangu na kumtimua ili nioe kiharari bado nashindwa
 
Yote tisa kumi tatizo ni wewe....unamzalishaje mtoto wa watu watoto wawili wote hujamtolea mahari....hakika kilio chake ni majuto ayapatayo ... Anatamani nae aonekane mwanamke...ni sahihi unavyombeza.wanawake na sisi bhana
Na mimi nimewaza kama wewe. Wanawake tunajihamishiaga kwa wanaume tukiwa na matarajio ya ndoa. Tunakuja kushtuka tumeshazaa watoto kadhaa na hakuna chochote kinachoendelea, tunaishia kupata kichaa cha ndoa.

Wasiwasi wa kutokujua mustakabali wa mahusiano yetu; unaanza kuleta hasira na visirani. Hapo anawaza what if kesho mwanaume anaishia kuoa mwanamke mwingine; na perhaps anatamani kuondoka ila akiwaza tayari ana watoto juu anaishia kulia. She needs security period. Unakaa na mtoto wa watu, unazaa naye hadi watoto wawili na bado hata tu kufika kwao kujitambulisha hakuna; kwa nini dada wa watu asiwe na visirani? I can't imagine ajue kuna mwenzie huko nje and she is expecting.
 
Back
Top Bottom