Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa Kingono

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imemsimamisha kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu, Karim Khan. Hatua hii inakuja baada ya uchunguzi wa miezi 18 uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.

Khan anatuhumiwa kumnyanyasa kijinsia mara kwa mara mfanyakazi wa kike wa ICC kwa muda mrefu. Inadaiwa alifanya naye ngono bila ridhaa yake ofisini kwake, nyumbani kwake, na hata walipokuwa kwenye safari za kiofisi.

Wachunguzi kutoka Ofisi ya Huduma za Usimamizi wa Ndani ya Umoja wa Mataifa (OIOS) walisema kuna viashiria vya ukweli kuhusu tuhuma hizo. Hata hivyo, majaji watatu waliopitia ripoti hiyo walihitimisha kuwa ushahidi uliopo hautoshi kuthibitisha kosa hilo "bila kuacha shaka yoyote".

Khan amekuwa akikanusha vikali tuhuma hizo, na mawakili wake wamesema uamuzi wa kumsimamisha kazi si wa kisheria, haukufuata taratibu na hauna ushahidi. Mpaka sasa, hakuna mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa dhidi yake.

Tuhuma hizi ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na mtu wa tatu mnamo Mei 2024, lakini kesi ilifungwa baada ya mhanga kukataa kushiriki. Baada ya kukosolewa kuwa uchunguzi wa kwanza uliharibiwa, suala hilo lilirudishwa tena Oktoba 2024 na kusababisha uchunguzi mkubwa wa Umoja wa Mataifa uliomsimamisha kazi. Kwa sasa atasubiri kura ya mwisho kutoka kwa nchi 125 wanachama wa mahakama hiyo.

Khan, ambaye amekuwa mwendesha mashtaka mkuu tangu mwaka 2021, alitoa hati za kukamatwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Marekani iliongeza shinikizo dhidi ya mahakama hiyo, hasa kutokana na hati ya kukamatwa kwa Netanyahu, na kuweka vikwazo kwa wafanyakazi pamoja na majaji wa mahakama hiyo.

1780992998024.png

​
Source: BBC, DW, Al Jazeera
 
Huyu kabananishwa kisa tu alitoa hati ya mashtaka dhidi ya Netanyahu!! Hii dunia hakuna demokrasia ya kweli, ukigusa wenye nguvu unaundiwa zengwe ila cha ajabu wao ndio wanajifanya kupigania demokrasia au kupambana na ugaidi dunia nzima!!

Unafiki wa ajabu sana
 
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imemsimamisha kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu, Karim Khan. Hatua hii inakuja baada ya uchunguzi wa miezi 18 uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.

Khan anatuhumiwa kumnyanyasa kijinsia mara kwa mara mfanyakazi wa kike wa ICC kwa muda mrefu. Inadaiwa alifanya naye ngono bila ridhaa yake ofisini kwake, nyumbani kwake, na hata walipokuwa kwenye safari za kiofisi.

Wachunguzi kutoka Ofisi ya Huduma za Usimamizi wa Ndani ya Umoja wa Mataifa (OIOS) walisema kuna viashiria vya ukweli kuhusu tuhuma hizo. Hata hivyo, majaji watatu waliopitia ripoti hiyo walihitimisha kuwa ushahidi uliopo hautoshi kuthibitisha kosa hilo "bila kuacha shaka yoyote".

Khan amekuwa akikanusha vikali tuhuma hizo, na mawakili wake wamesema uamuzi wa kumsimamisha kazi si wa kisheria, haukufuata taratibu na hauna ushahidi. Mpaka sasa, hakuna mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa dhidi yake.

Tuhuma hizi ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na mtu wa tatu mnamo Mei 2024, lakini kesi ilifungwa baada ya mhanga kukataa kushiriki. Baada ya kukosolewa kuwa uchunguzi wa kwanza uliharibiwa, suala hilo lilirudishwa tena Oktoba 2024 na kusababisha uchunguzi mkubwa wa Umoja wa Mataifa uliomsimamisha kazi.

Source: BBC, DW, Al Jazeera
SITAKI UPUZI HII NCHI LAZIMA NIDHAMU IWEPO LA SIVYO TUTAENDELEA KUDIDIMIA KAMA TAIFA. DISCIPLINE NA KAZI LAZIMA IWEPO NINAANZA HUMU HUMU JAMII FORUM. SITAKI NA SIPENDI UPUZI.

FREE TUNDU LISSU NOW

GACHAGUA LAZIMA AWE RAIS WA KENYA.

adriz de mbusii
 
Sisi tunachotaka hao ICC waje hapa wafanye uchunguzi dhidi ya mauaji ya Oktoba 29 mwaka jana kwa sababu ICC sio mwendesha mashtaka mkuu tu.

Ni ukweli usiopingika kwamba hakuna uchunguzi wowote wa maana uliofanyika hadi leo, haiwezekani watuhumiwa wa uhalifu eti tena ndio wajichunguze wenyewe. Hilo halipo.
 
Karim Khan, mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) huko The Hague, amesimamishwa kazi akisubiri kura ya mwisho kutoka kwa nchi 125 wanachama wa mahakama hiyo, kufuatia uchunguzi wa miezi 18 kuhusu utovu wa nidhamu wa kingono unaomhusisha msaidizi wa zamani.

Chuo kinachoongoza ICC kilisema kesi hiyo itapelekwa kwenye kikao maalum ambacho hatimaye kinaweza kuamua kama Khan ataondolewa madarakani. Khan, ambaye amekana madai yote na kuelezea kesi hiyo kuwa isiyo ya haki na isiyoungwa mkono na ushahidi, tayari alikuwa amejiuzulu kutoka kwa majukumu yake mnamo Mei 2025 wakati uchunguzi ulipokuwa ukiendelea.

Kusimamishwa huko kunaonyesha mara ya kwanza katika historia ya ICC kwa mwendesha mashtaka mkuu aliye madarakani kusimamishwa rasmi.
 
Attachments

  • IMG_5492.jpeg
    IMG_5492.jpeg
    119.3 KB · Views: 23
Huyu kabananishwa kisa tu alitoa hati ya mashtaka dhidi ya Netanyahu!! Hii dunia hakuna demokrasia ya kweli, ukigusa wenye nguvu unaundiwa zengwe ila cha ajabu wao ndio wanajifanya kupigania demokrasia au kupambana na ugaidi dunia nzima!!

Unafiki wa ajabu sana
Dunia hii ni ya kinafiki sana, sio UNo wala YTO, wote ni hao hao
 
Nawashangaa mnaoihusisha marekani na tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili Khan.

Yapo mazingira ambayo mtu ungeweza connect useme kweli marekani kahusika, marekani wangeweza hata kusema hawana imani nae, hiyo ingetosha kumuweka Khan kwenye wakati mgumu.

Lakini tuhuma zinazohusisha mwanamke hilo ni balaa lake alikojitafutia mwenyewe.
 
Yaani miaka yote hana kashfa mpaka siku tu aliyoamua kumkamata Netanyahu? Hata huyo judge anayesikiliza kesi ya ufisadi ya Netanyahu usishangae akapewa kesi ya ubakaji.
 
Marekani iliongeza shinikizo dhidi ya mahakama hiyo, hasa kutokana na hati ya kukamatwa kwa Netanyahu, na kuweka vikwazo kwa wafanyakazi pamoja na majaji wa mahakama hiyo.
Hapa ndipo main body ilipo, hayo mengineyo ni sarakasi tu. Wao walitaka hiyo mahakama ya ICC iwe inashughulikia viongozi wa Afrika na latin America. Walivyoona Netanyahu kaguswa wakaweka Nongwa.
 
Yaani miaka yote hana kashfa mpaka siku tu aliyoamua kumkamata Netanyahu? Hata huyo judge anayesikiliza kesi ya ufisadi ya Netanyahu usishangae akapewa kesi ya ubakaji.
Hapa issue ya msingi ni mtuhumiwa amefanya kosa au hajafanya, suala la wakati sioni kama lina maana.

Mtu yeyote anaweza fanya any stupid thing at any time regardless ya nafasi yake popote.

Kuanza kwake kusikiliza kesi ya Neta hakukumzuia kufanya stupid thing, wacha wenye maamuzi wakae chini waamue.
 
Hajafanya kosa ni tuhuma tu za mwanamke mmoja kuwa "alimshika" bila idhini yake. Sasa kweli kumshika mtu mkono tu ndio kesi ya kumfukuzisha mtu? Unaona kabisa ni kisiasa. Mtu kama Khan kwa hela zake tu anaweza agiza mrembo yoyote kwa bei yoyote kulala naye wala hahitaji "kumshika shika" mfanyakazi wa taasisi yake.
 
Mahakama yenyewe imekueleza haina ushahidi usio na mashaka. Umeona kuna hukumu hapo?

Majaji watatu walioendesha kesi hawakuona ushahidi, wewe umeupata wapi?
 
Marekani haihusiki chochote na ICC huyo bwana kapatikana na makosa kivyake tu na hata hivyo yeye sio malaika kwamba hawezi kukosea.

Sisi tunawasubiri waje watufanyie uchunguzi wa mauaji ya halaiki ya Oktoba 29 mwaka jana.
 
Hajafanya kosa ni tuhuma tu za mwanamke mmoja kuwa "alimshika" bila idhini yake. Sasa kweli kumshika mtu mkono tu ndio kesi ya kumfukuzisha mtu? Unaona kabisa ni kisiasa. Mtu kama Khan kwa hela zake tu anaweza agiza mrembo yoyote kwa bei yoyote kulala naye wala hahitaji "kumshika shika" mfanyakazi wa taasisi yake.
Nimeshakwambia, iwe uwezo wa mtu kiuchumi, au nafasi ya mtu kijamii
Hajafanya kosa ni tuhuma tu za mwanamke mmoja kuwa "alimshika" bila idhini yake. Sasa kweli kumshika mtu mkono tu ndio kesi ya kumfukuzisha mtu? Unaona kabisa ni kisiasa. Mtu kama Khan kwa hela zake tu anaweza agiza mrembo yoyote kwa bei yoyote kulala naye wala hahitaji "kumshika shika" mfanyakazi wa taasisi yake.

hakumzuii kufanya kosa, na mwenye mamlaka ya kuamua kama amekosea ni hizo kura za hao members states 125, sio wewe wala mimi.

Navyojua, kwa sheria za wenzetu kumshika mwanamke bila idhini yake ni kosa, ila kwa hapa bongo ndio tumezoea kushikana hovyo
 
Back
Top Bottom