Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa Kingono

Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa Kingono

Hapana ni Marekani na Israel wasipokutaka utaondoka tu. AIPAC inatoa mabilion ya fedha kufadhili wanasiasa wa USA so lazima watie joto mpaka wasiyemtaka aondolewe.

Ila angekua amekamata viongozi wa Hamas na Iran ungeona ambavyo angetetewa. Kwa kuamini tu angalia waliohusishwa na Epstein files je wangapi wamekamatwa hadi sahivi? Dunia imejaa unafiki tu.
Hizi ni hisia zako tu umeandika hapa. Nilishakwambia mwanzo, Khan sio malaika wacha wafuate taratibu zao kujua mbivu na mbichi.
 
Hizi ni hisia zako tu umeandika hapa. Nilishakwambia mwanzo, Khan sio malaika wacha wafuate taratibu zao kujua mbivu na mbichi.
Sio hisia mkuu mimi huwa naandika facts. Hii hapa official page ya AIPAC ikipush Congress ya marekani kupitisha muswada wa kumnyoosha Khan. Muswada unaitwa; Illegitimate Court Counteraction Act of 2023 na kazi yake ni kuwawekea vikwazo Khan na wenzake wote wanaohusika kuwafungulia mashtaka wayahudi na wamarekani.

Kwahiyo ni Israel na wafanyabiashara wa kiyahudi sio tu walishawishi Congress kuandaa muswada huu bali waliwaelekeza namna ya kumng'oa Khan na wote walioshirikiana kumfungulia mashtaka Netanyahu.

Hii ni statement kutoka hiyo link kama hamtofungua. Hivyo sio hisia zangu bali ni facts kuwa Israel ndio imemng'oa kupitia AIPAC lobby group.
Screenshot_20260613_100943_Chrome.jpg

Cc Proved
 
View attachment 3606827

Cc Proved
By the way nimesoma sheria, ujue sio kila utapotumia kifungu cha sheria kujibu hoja ndio ujione uko sahihi, you wrong.

Huo muswada wapi wanasema watamtumia mwanamke ili wapate sababu ya kumuwekea KHAN vikwazo?

▪Naona huo muswada unazungumzia Israel wakati kesi iliyopo mezani ni mwanamke, unajichanganya.

Leta ushahidi unaojitosheleza, sio "kujiongeza" kama unavyofanya, ndio maana nakwambia unaandika hisia zako tu.

Huwezi kumtetea mtu simply kwa "kujiongeza" .Narudia tena one last time, KHAN sio malaika, wacha taratibu zao zifuatwe ijulikane.
 
Huo muswada wapi wanasema watamtumia mwanamke ili wapate sababu ya kumuwekea KHAN vikwazo?
Umesema vikwazo kwa yoyote anayefungulia mashtaka Israel au USA. Na kweli aliwekewa vikwazo kupitia sheria hii na process ya kumtoa ilianza hata kabla ya sex allegations.

Kwahiyo abake au asibake ilikua lazima atolewe kwa mujibu wa muswada huu. Ndio maana licha majaji kukosa ushahidi mzito kama nilivyokuwekea ruling jana bado wameendelea na impeachment.

Kasome hiyo sheria na utekelezaji wake ndio utanielewa.
 
By the way nimesoma sheria, ujue sio kila utapotumia kifungu cha sheria kujibu hoja ndio ujione uko sahihi, you wrong
Kusoma sheria sio issue, hata mimi nilisoma course ya international business law ngazi ya M.A so sio layman wa sheria pia.
Naona huo muswada unazungumzia Israel wakati kesi iliyopo mezani ni mwanamke, unajichanganya.
Sio kweli, umezungumzia kumuondoa prosecutor na wenzake wa ICC pale wanapomtuhumu mmarekani au muisraeli/myahudi. Kwahiyo hoja yangu bado inasimama kuwa ALITAKIWA KUONDOLEWA kwa kupitia sheria hii irrespective ya kesi ya ubakaji.
Leta ushahidi unaojitosheleza, sio "kujiongeza" kama unavyofanya, ndio maana nakwambia unaandika hisia zako tu.
Sawa nakuwekea timeline hapo chini
 
Umesema vikwazo kwa yoyote anayefungulia mashtaka Israel au USA. Na kweli aliwekewa vikwazo kupitia sheria hii na process ya kumtoa ilianza hata kabla ya sex allegations.

Kwahiyo abake au asibake ilikua lazima atolewe kwa mujibu wa muswada huu. Ndio maana licha majaji kukosa ushahidi mzito kama nilivyokuwekea ruling jana bado wameendelea na impeachment.

Kasome hiyo sheria na utekelezaji wake ndio utanielewa.
Naona huishiwi maneno ya kuandika, usinipe kazi ya kusoma vitu visivyoendana na hiki kinachojadiliwa kwa huu uzi.

Nijibu hapa:

- Wapi USA wamesema watamuwekea mtego wa mwanamke?

- Khan ni malaika asiyekosea?
 
Kusoma sheria sio issue, hata mimi nilisoma course ya international business law ngazi ya M.A so sio layman wa sheria pia.

Sio kweli, umezungumzia kumuondoa prosecutor na wenzake wa ICC pale wanapomtuhumu mmarekani au muisraeli/myahudi. Kwahiyo hoja yangu bado inasimama kuwa ALITAKIWA KUONDOLEWA kwa kupitia sheria hii irrespective ya kesi ya ubakaji.
Sawa nakuwekea timeline hapo chini
Acha kuweka utazidi kujitoa nje ya mada. Jibu hayo maswali mawili hapo tufunge mjadala.
 
TIMELINE
Mei 2024: Karim Khan aliomba ICC kutoa hati za kukamatwa dhidi ya viongozi wa Hamas na viongozi wa Israel.
Mei–Oktoba 2024: Malalamiko ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya Khan yaliwasilishwa ndani ya ICC.
Novemba 2024: Uchunguzi rasmi wa OIOS (umoja wa mataifa) ulianza kuhusu tuhuma hizo.
Februari 2025: Serikali ya Marekani iliweka vikwazo dhidi ya Karim Khan kutokana na hatua za ICC kuhusu viongozi wa Israel.
Mei 2025: Khan alijiondoa kwa muda madarakani akisubiri matokeo ya uchunguzi.
Desemba 2025: Uchunguzi wa OIOS ulikamilika na kuwasilisha matokeo yake.
Juni 2026: Khan alisimamishwa kazi huku mchakato wa uamuzi wa mwisho ukiendelea.

kwa timeline hii unaona kabisa alitungiwa sheria na kuwekewa vikwazo ikiwemo ICC kunyimwa fedha ya bajeti na kuzuiwa kuingia US kabla hata uchunguzi haujaisha wala majaji hawajatoa hukumu.

Maana yake alishawekewa vikwazo kabla hata majaji hawajatoa hukumu. Hivyo bila hata kesi ya ubakaji alishapigwa vikwazo hivyo asingeweza endelea kuwa prosecutor wa ICC. Sasa wapi nimeingiza hisia wakati hizi zote ni facts.
 
Bado hujajibu maswali yangu, sioni kitu hapo.
 
- Wapi USA wamesema watamuwekea mtego wa mwanamke?
Usilazimishe, alishawekewa vikwazo kabla ya uchunguzi hata kuisha. Kwahiyo alishakua blacklisted na kutakiwa kuondolewa whether or not kesi ya ubakaji angeshinda.

Ambacho huelewi ni nini? Sanctions zimetolewa kwa Khan kabla ya kesi ya ubakaji.
 
Bado hujajibu maswali yangu, sioni kitu hapo.
Nimekujibu mbona kuwa sheria ilitungwa na ikamchukulia hatua Khan kwa sababu tu ya kufungulia mashtaka Netanyahu (Muisraeli) na ndio ilivyokua Trump alisign kuwa sheria na kumpiga vikwazo Khan na ICC staff kabla hata ya uchunguzi wa kesi ya "kumshika shika" mfanyakazi wake kuisha.

Kwahiyo hoja yangu ni kweli kuwa alichukuluwa hatua sababu tu ya kutoa arrest warrant kwa Netanyahu. Hili umeshindwa kukataa sababu nimekuwekea ushahidi wa kisheria na vikwazo vilivyotokea kabla ya uchunguzi kuisha.
 
Usilazimishe, alishawekewa vikwazo kabla ya uchunguzi hata kuisha. Kwahiyo alishakua blacklisted na kutakiwa kuondolewa whether or not kesi ya ubakaji angeshinda.

Ambacho huelewi ni nini? Sanctions zimetolewa kwa Khan kabla ya kesi ya ubakaji.
Unashindwa kujibu maswali unaleta ubishi tu, na muendelezo wa hisia zako.

Kwani sanctions zinamzuia Khan kutenda kosa lingine? Hapa hatujadili vikwazo alivyowekewa Khan na US, tunajadili tuhuma dhidi ya Khan.

Uunajichanganya tu huelewi chochote hapa.

Am off.
 
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imemsimamisha kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu, Karim Khan. Hatua hii inakuja baada ya uchunguzi wa miezi 18 uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.

Khan anatuhumiwa kumnyanyasa kijinsia mara kwa mara mfanyakazi wa kike wa ICC kwa muda mrefu. Inadaiwa alifanya naye ngono bila ridhaa yake ofisini kwake, nyumbani kwake, na hata walipokuwa kwenye safari za kiofisi.

Wachunguzi kutoka Ofisi ya Huduma za Usimamizi wa Ndani ya Umoja wa Mataifa (OIOS) walisema kuna viashiria vya ukweli kuhusu tuhuma hizo. Hata hivyo, majaji watatu waliopitia ripoti hiyo walihitimisha kuwa ushahidi uliopo hautoshi kuthibitisha kosa hilo "bila kuacha shaka yoyote".

Khan amekuwa akikanusha vikali tuhuma hizo, na mawakili wake wamesema uamuzi wa kumsimamisha kazi si wa kisheria, haukufuata taratibu na hauna ushahidi. Mpaka sasa, hakuna mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa dhidi yake.

Tuhuma hizi ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na mtu wa tatu mnamo Mei 2024, lakini kesi ilifungwa baada ya mhanga kukataa kushiriki. Baada ya kukosolewa kuwa uchunguzi wa kwanza uliharibiwa, suala hilo lilirudishwa tena Oktoba 2024 na kusababisha uchunguzi mkubwa wa Umoja wa Mataifa uliomsimamisha kazi. Kwa sasa atasubiri kura ya mwisho kutoka kwa nchi 125 wanachama wa mahakama hiyo.

Khan, ambaye amekuwa mwendesha mashtaka mkuu tangu mwaka 2021, alitoa hati za kukamatwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Marekani iliongeza shinikizo dhidi ya mahakama hiyo, hasa kutokana na hati ya kukamatwa kwa Netanyahu, na kuweka vikwazo kwa wafanyakazi pamoja na majaji wa mahakama hiyo.

Source: BBC, DW, Al Jazeera
Aliwahi kua wakili wa rafiki yangu sana Dr. William Samoe Ruto, wakati huo alipokua naibu wa rais, akituhumiwa kufadhili ghasia za baada ya uchaguzi 2007-2008,

na muendesha alikua serious man Muajentina Luis Moreno Ocampo wakati huo, kabla ya Fatou Bensouda kuchukua kijiti na kulemewa nacho 🐒
 
Nawashangaa mnaoihusisha marekani na tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili Khan.

Yapo mazingira ambayo mtu ungeweza connect useme kweli marekani kahusika, marekani wangeweza hata kusema hawana imani nae, hiyo ingetosha kumuweka Khan kwenye wakati mgumu.

Lakini tuhuma zinazohusisha mwanamke hilo ni balaa lake alikojitafutia mwenyewe.
We nae kweli akili zako zinameza ARV. Kwamba haiwezekani mwanamke kutumika kusuka mpango. Mbona una hoja mfu.
 
Unashindwa kujibu maswali unaleta ubishi tu, na muendelezo wa hisia zako.
Nimeweka timeline ila bado mbishi tu.
Kwani sanctions zinamzuia Khan kutenda kosa lingine? Hapa hatujadili vikwazo alivyowekewa Khan na US, tunajadili tuhuma dhidi ya Khan.
Sasa tuhuma si alikutwa hana hatia na majaji. Na kuhusu vikwazo aliwekewa kabla ya kesi ya ubakaji. Maana yake alivyomgusa tu Netanyahu ndio akawekewa vikwazo.

So hoja yangu kuwa kumgusa Netanyahu ndio kumemfanya aondolewe bado ipo valid.

Nimekuweka sheria ya Illegitimate Court act na jinsi vikwazo vilitolewa kabla ya uchunguzi wa makosa ya ubakaji.

Msomi wa law unashindwa kujua tofauti ya political and legal cases? Kashinda legally sasa anatolewa politically. Unachobisha ni nini hasa?
 
We nae kweli akili zako zinameza ARV. Kwamba haiwezekani mwanamke kutumika kusuka mpango. Mbona una hoja mfu.
Muwe na ushahidi nyie wajinga, sio kuja hapa na maneno matupu, hili sio jukwaa la wapiga ramli.

Mjinga mwenzio analeta ushahidi usioendana na tukio, kaulizwa A anajibu B, wewe njoo na huo wako kama unao, au sivyo acha kelele.
 
Nimeweka timeline ila bado mbishi tu.

Sasa tuhuma si alikutwa hana hatia na majaji. Na kuhusu vikwazo aliwekewa kabla ya kesi ya ubakaji. Maana yake alivyomgusa tu Netanyahu ndio akawekewa vikwazo.

So hoja yangu kuwa kumgusa Netanyahu ndio kumemfanya aondolewe bado ipo valid.

Nimekuweka sheria ya Illegitimate Court act na jinsi vikwazo vilitolewa kabla ya uchunguzi wa makosa ya ubakaji.

Msomi wa law unashindwa kujua tofauti ya political and legal cases? Kashinda legally sasa anatolewa politically. Unachobisha ni nini hasa?
Unanipotezea muda. Sijaona hoja yako yenye valid yoyote, hakuna hoja iliyojitosheleza isiyoacha shaka, hoja zako zimejaa ramli tu.

Kwa upeo wako ndio unajiona una hoja valid, sio upeo wangu. Hujui hats kuzungumzia jambo specific, unarukia jambo lingine lisilohusika.

Nimeshakwambia wacha wafuate taratibu zao, wewe kinachokuhangaisha nini? Taratibu zao zinataka member states wapige kura, na Khana anajua huo ndio utaratibu. sasa wewe unakataa kitu gani hapo?

Acha ubishi wa kitoto.
 
Huyu kabananishwa kisa tu alitoa hati ya mashtaka dhidi ya Netanyahu!! Hii dunia hakuna demokrasia ya kweli, ukigusa wenye nguvu unaundiwa zengwe ila cha ajabu wao ndio wanajifanya kupigania demokrasia au kupambana na ugaidi dunia nzima!!

Unafiki wa ajabu sana
Huwa nawaona watz wanaotegemea hiyo mifumo kupata haki kama wasennge wasennge.
 
Back
Top Bottom