Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa Kingono

Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa Kingono

Muwe na ushahidi nyie wajinga, sio kuja hapa na maneno matupu, hili sio jukwaa la wapiga ramli.

Mjinga mwenzio analeta ushahidi usioendana na tukio, kaulizwa A anajibu B, wewe njoo na huo wako kama unao, au sivyo acha kelele.
Wewe ni kiande tu uko too obsessed na Marekani. Wenzako tulishashtuka tukaacha unazi wa kipuuzi. Hakuna namna sijui Urusi sijui EU sijui USA watakuja kuwa wakombozi wa taifa letu. Kiazi mbatata!
 
Wewe ni kiande tu uko too obsessed na Marekani. Wenzako tulishashtuka tukaacha unazi wa kipuuzi. Hakuna namna sijui Urusi sijui EU sijui USA watakuja kuwa wakombozi wa taifa letu. Kiazi mbatata!
Huu ndio ushahidi niliokwambia uulete, hope now umeshajiona ulivyo mjinga kama mwenzako.

Another one!.
 
Unanipotezea muda. Sijaona hoja yako yenye valid yoyote, hakuna hoja iliyojitosheleza isiyoacha shaka, hoja zako zimejaa ramli tu.

Kwa upeo wako ndio unajiona una hoja valid, sio upeo wangu. Hujui hats kuzungumzia jambo specific, unarukia jambo lingine lisilohusika.

Nimeshakwambia wacha wafuate taratibu zao, wewe kinachokuhangaisha nini? Taratibu zao zinataka member states wapige kura, na Khana anajua huo ndio utaratibu. sasa wewe unakataa kitu gani hapo?

Acha ubishi wa kitoto.
I'll leave this article here, a piece of investigative journalism about israel's decade-long war against ICC and you'll realise Khan is just a latest victim.

I rest my case

 
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imemsimamisha kazi Mwendesha Mashtaka Mkuu, Karim Khan. Hatua hii inakuja baada ya uchunguzi wa miezi 18 uliofanywa na Umoja wa Mataifa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia.

Khan anatuhumiwa kumnyanyasa kijinsia mara kwa mara mfanyakazi wa kike wa ICC kwa muda mrefu. Inadaiwa alifanya naye ngono bila ridhaa yake ofisini kwake, nyumbani kwake, na hata walipokuwa kwenye safari za kiofisi.

Wachunguzi kutoka Ofisi ya Huduma za Usimamizi wa Ndani ya Umoja wa Mataifa (OIOS) walisema kuna viashiria vya ukweli kuhusu tuhuma hizo. Hata hivyo, majaji watatu waliopitia ripoti hiyo walihitimisha kuwa ushahidi uliopo hautoshi kuthibitisha kosa hilo "bila kuacha shaka yoyote".

Khan amekuwa akikanusha vikali tuhuma hizo, na mawakili wake wamesema uamuzi wa kumsimamisha kazi si wa kisheria, haukufuata taratibu na hauna ushahidi. Mpaka sasa, hakuna mashtaka yoyote ya jinai yaliyofunguliwa dhidi yake.

Tuhuma hizi ziliripotiwa kwa mara ya kwanza na mtu wa tatu mnamo Mei 2024, lakini kesi ilifungwa baada ya mhanga kukataa kushiriki. Baada ya kukosolewa kuwa uchunguzi wa kwanza uliharibiwa, suala hilo lilirudishwa tena Oktoba 2024 na kusababisha uchunguzi mkubwa wa Umoja wa Mataifa uliomsimamisha kazi. Kwa sasa atasubiri kura ya mwisho kutoka kwa nchi 125 wanachama wa mahakama hiyo.

Khan, ambaye amekuwa mwendesha mashtaka mkuu tangu mwaka 2021, alitoa hati za kukamatwa kwa viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Marekani iliongeza shinikizo dhidi ya mahakama hiyo, hasa kutokana na hati ya kukamatwa kwa Netanyahu, na kuweka vikwazo kwa wafanyakazi pamoja na majaji wa mahakama hiyo.

Source: BBC, DW, Al Jazeera
Shinikizo kutoka washington
 
Back
Top Bottom