Mwendokasi Mbagala ukikamilika utasababisha foleni ya kihistoria, Serikali ichukue hatua hizi mapema

Mwendokasi Mbagala ukikamilika utasababisha foleni ya kihistoria, Serikali ichukue hatua hizi mapema

Kwanza kuna tofauti kati ya mwendokasi ya Gerezani na maeneo mengine ya Morogoro rd ba na Gerezani na Mbagala.
Mbagala kuna gari nyingi sana, afu pia njia kuu Kilwa rd ndio inayotumia kwa daladala kupakia abiria. Mfumo huu ni mbaya sana kwani unasababisha foleni kwa sababu njia ya kupita vyombo vingine vya usafiri inabaki ndogo.

Kwa sasa askari wa usalama barabarani inabidi aruhusu magari mengine kuchepukia kwenye mwendo kasi ili kuuwa foleni. Kwa sasa barabara ya mwendokasi imefungwa na mkandarasi sababu ya marekebisho foleni inaanza Rangi3 mpaka Kipati. Kufika Rangi3 unaweza kutumia saa 2 mpaka 3 kipande cha km1 tu. Nini kifanyike ili kunusuru tatizo hilo.

Serikali ijenge kutuo kitakachomeza daladala zote kama ilivyo mbezi. Yani isionekane daladala yeyote ikipakia abiria njiani. Hii italeta manufaa kwa sababu magari mengine yatapita kwa uhuru.

Kwa sababu kituo cha mwendokasi Mbagala ni kikubwa basi serikali igawanye, kuwe na stendi ya daladala, stendi ya mwendokasi na stendi ya magari ya mikoani.
Bila hivyo tutashuhudia kero baadae baada ya kukamilisha mradi.

Mbagala hakuna mipango miji itakayowezesha magari mengine kuchepuka, njia kuu ni moja tu, Kilwa rd.
Hivi ikitokea kwa mfano Mwendokasi zikaanza kutembea halafu kukawa na foleni; una maoni gani iwapo kama NUSU YA IDADI ya daladala za Mbagala nazo zikaruhusiwa kutumia pia barabara ya mwendokasi KUBALANCE, just in case kuna foleni itakayokuja kusabishwa na magari ya mwendokasi yatakapoanza kutumia njia yake?
 
Daladala mbagala zife ndizo zinazo 7bbsha foleni! Kituo kipo barabarani na ile round about yapili kutokea mwisho kama unafuata down ya kwenda kongowe nayo ni jipu
 
Mbagala wanaishi uncivilised people

MTU mwenye akil yako huwezi kwenda kuishi Mbagala
Sema tu, ulikua hujaja dar, kipindi mwendo kasi ya kimara inajengwa, foleni ilikua kubwa sana, nakumbuka baadhi ya watu walikua wanaishi mbezi, tena wengine kwenye nyumba zao, walienda kupanga maeneo ya magomeni, kama ulikua mjini inategemea umri wako.

Ukiona wote wanaishi huko eti hawana akili, basi jua pia umewatukana wazazi wako, kwa kuto kukulea kuheshi watu.
 
Punguza mdomo wewe mbagala ni ya ovyo lakini usiongee usivyo vijua sehemu ina matawi ya bank zaidi 7 unawaita wenzako vichaa?
Kuna frem mpaka za 1.5mil kuna kichaa anaweza kupanga?
Sisi tunaongelea kadhia ya foleni na mwendo kasi lakini wewe umevuka mipaka mipaka unaanza kutukana wakazi wa mbagala.
NB:huo mji unaouita wa vichaa una mzunguko mkubwa wa pesa kuliko mbweni,tegeta na goba
Mbagala ni kubwa, ina watu wengi, inahudumia maeneo yote kuanzia mkuranga kwenda huko Kusini

Dart wenyewe wanasema mradi wa BRT ya Mbagala ukikamilika huo mradi pekee utakuwa wasafirisha watu 700,000 kwa siku
 
Sema tu, ulikua hujaja dar, kipindi mwendo kasi ya kimara inajengwa, foleni ilikua kubwa sana, nakumbuka baadhi ya watu walikua wanaishi mbezi, tena wengine kwenye nyumba zao, walienda kupanga maeneo ya magomeni, kama ulikua mjini inategemea umri wako.

Ukiona wote wanaishi huko eti hawana akili, basi jua pia umewatukana wazazi wako, kwa kuto kukulea kuheshi watu.
Uko mbezi kulikua na uncle mmoja namfahamu anapiga tax town ikifika jion anapeleka gari kulaza alaf yy anaanza kupambana na daladala kurudi mbezi, ilikua sio poa mbezi
 
Mbweni....

Acha umbumbumbu Mbweni inayo Mitaa Mingi huo ni Mtaa tu kuna Mitaa ya Maskini wa kutisha huko huko huko Mbweni ndiyo nikakueleza Kuna Mbweni Maputo hoi bin taabani ,lakini kule Mbweni Mpiji bado kumejaa mashamba tu na mapagala . Hivyo jua kuwa kila Eneo Lina maeneo choka na wenye Uwezo,Fika Mikocheni A Mtaa wa pale nyuma ya Shoppers plaza Ni kinyaa Cha kutisha wenyewe Wanaita Gezaulole . Lakini Ukiwa Mikocheni B ni Matajiri Mji umepangwa.Kwa Jiji la Dar es salaam Mji ambao unafanana ni Mtaa wa Masaki na Oysterbay tu Tena Ipo katika kata ya Msasani Ila ukifika Eneo lenyewe la Msasani maandazi road Hutoamini Kama ni Dar es salaam yaani pananuka mitaro Maji taka Ila kwakuwa ule Mtaa ni haupo Barabara kuu huwezi sikia pakizungumziwa.
Weka akilini Dar es salaam kata zote zina Mitaa ya Maskini na Matajiri.
 
Kwani huwezi kutoa hoja yako bila kutukana?... na kutumia offensive words...

I pity you...am out
 
Na jambo la kumshukuru mkandarasi wa ile njia amepatia sana kuwawekea vituo visivyozibwa kwa vioo kama njia zingine.
Bila hivo Serikali ingepata hasara.
Tena ikiwezekana wapelekewe na mabasi yenye wavu madirishani maana wale watu wanajijua.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hii comment imenivunja mbavu
 
Back
Top Bottom